Ushauri bora kwa walio kwenye mahusiano

Llio 002

JF-Expert Member
Jul 14, 2015
1,615
2,031
Mahusiano yanatakiwa yawe daraja la maisha yako wala si ukuta wa kufupisha au kuharibu maisha yako. Ukiona mahusiano uliyonayo hayawi daraja la ukuaji wako wa kiroho, kiakili na kiafya basi si mahusiano ila shida.

Ukibaini umekosea chaguo basi usiogope kuanza upya, maana hata watu sahihi au wema hukosea chaguo kwasababu ya ubinadamu walioumbwa nao au kwa kusababishiwa na mtu

Mateso na maumivu ya kuishi na mtu asiye sahihi hayana msaidizi kuwa utawagawia mtu akusaidie utaathirika nayo wewe mwenyewe wala si baba, dada, mama yako unayemuogopa utamtia aibu ukiyachilia hayo mahusiano usiyo na furaha nayo

Kwasababu wewe ndiye unajua unapitia nini basi wewe ndiye unapaswa kuwa mwenye maamuzi. Mapenzi yamebeba hatma za watu usikubali mtu fulanifulani kwa ujinga wake aharibu hatma yako.

Si kila mtu anafaa kuwa mume/mke wengine wanatakiwa wabaki kama mapambo na mifano ya watu fulani.

Usikubali kuishi kwenye makosa yanayosahihishika na kubadilishika kwa ajili ya kesho yako njema. Tamani kumalizia kipande cha maisha yako kilichosalia hapa duniani kwa amani na tabasamu kuliko kuendelea kuishilia.

Linda moyo wako kuliko chochote kile ulindacho. Elewa neno KULIKO CHOCHOTE ina maana moyo wako ndio kila kitu kwenye roho, mwili na nafsi. Moyo ni kitu chanye thamani na ndio maisha yako yalipo. Moyo umebeba chemichemi uzima na mauti

Mimi sina cha kukufundisha ila nakutafakarisha. Unaweza kunipuuza ila usiyadharau maneno yangu. Yatakusaidia mahala hata kama sio leo
FB_IMG_1711269667652.jpg
 
Mahusiano gani kwanza unayozungumzia?

Ya kulana na kuachana?

Au ya ndoa takatifu!

Kama ni ndoa bwashee, basi mambo ni tofauti. Marriage is all about responsibilities. Ndoa ni wajibu. Ndoa imejaa majukumu. Kila mmoja akitimiza majukumu yake basi maisha yenu yataenda smoooothly. Ila mmojawenu akishadivert basi jua umeisha.
 
Mahusiano yanatakiwa yawe daraja la maisha yako wala si ukuta wa kufupisha au kuharibu maisha yako. Ukiona mahusiano uliyonayo hayawi daraja la ukuaji wako wa kiroho, kiakili na kiafya basi si mahusiano ila shida.

Ukibaini umekosea chaguo basi usiogope kuanza upya, maana hata watu sahihi au wema hukosea chaguo kwasababu ya ubinadamu walioumbwa nao au kwa kusababishiwa na mtu

Mateso na maumivu ya kuishi na mtu asiye sahihi hayana msaidizi kuwa utawagawia mtu akusaidie utaathirika nayo wewe mwenyewe wala si baba, dada, mama yako unayemuogopa utamtia aibu ukiyachilia hayo mahusiano usiyo na furaha nayo

Kwasababu wewe ndiye unajua unapitia nini basi wewe ndiye unapaswa kuwa mwenye maamuzi. Mapenzi yamebeba hatma za watu usikubali mtu fulanifulani kwa ujinga wake aharibu hatma yako.

Si kila mtu anafaa kuwa mume/mke wengine wanatakiwa wabaki kama mapambo na mifano ya watu fulani.

Usikubali kuishi kwenye makosa yanayosahihishika na kubadilishika kwa ajili ya kesho yako njema. Tamani kumalizia kipande cha maisha yako kilichosalia hapa duniani kwa amani na tabasamu kuliko kuendelea kuishilia.

Linda moyo wako kuliko chochote kile ulindacho. Elewa neno KULIKO CHOCHOTE ina maana moyo wako ndio kila kitu kwenye roho, mwili na nafsi. Moyo ni kitu chanye thamani na ndio maisha yako yalipo. Moyo umebeba chemichemi uzima na mauti

Mimi sina cha kukufundisha ila nakutafakarisha. Unaweza kunipuuza ila usiyadharau maneno yangu. Yatakusaidia mahala hata kama sio leoView attachment 2943308
Asante sana.
Hii Thread imenipa funzo sana.
Yule Jini mkata kamba naachana naye leoleo.
 
Fanya maamuzi mkuu
Ilo wo wo wo la huyo dada limefuta yote uliyonielekeza🥲
😀😀😀 kijana wahovyo
Mahusiano gani kwanza unayozungumzia?

Ya kulana na kuachana?

Au ya ndoa takatifu!

Kama ni ndoa bwashee, basi mambo ni tofauti. Marriage is all about responsibilities. Ndoa ni wajibu. Ndoa imejaa majukumu. Kila mmoja akitimiza majukumu yake basi maisha yenu yataenda smoooothly. Ila mmojawenu akishadivert basi jua umeisha.
Kwa hiyo kwenye ndoa unaweza ishi na mtu ambaye huna hisia naye? Mtu ambaye hata akikupapasa unaona kama vile anakukwangua na miba?
Tatizo binadamu wa siku hizi ni wabishi sana...

Cc: Mahondaw
Acha yawakute majambo
 
Back
Top Bottom