Unataka risiti ya TRA au risiti "ya kawaida"??? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Unataka risiti ya TRA au risiti "ya kawaida"???

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by The Inquisitive, Apr 15, 2011.

 1. The Inquisitive

  The Inquisitive Senior Member

  #1
  Apr 15, 2011
  Joined: Oct 27, 2010
  Messages: 178
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Nilienda duka moja hapa DSM (jina nalihifadhi). Nikachagua nilivyotaka, nikauliza bei. Nikaambiwa bei inategemea kama nataka risiti ya TRA au risiti "ya kawaida". Nikauliza tofauti ya bei ya risiti ya TRA na hiyo nyingine. Muuzaji akapiga hesabu ktk calculator akanionyesha jumla ya risiti ya TRA (ambayo ndio bei halisi) na "ya kawaida" - amepunguza kama 10% hv. Lakini hapo hapo akasema kuwa kwenye ile risiti "ya kawaida" ataandika figure XXX ambayo ilikuwa kama 1/3 ya bei halisi!!! Sikuelewa mchezo uliokuwa unachezwa hapo, nikamwambia anipe risiti ya TRA.

  Kwa mnaojua haya mambo, hii ni dili ya namna gani?
   
 2. Mazingira

  Mazingira JF-Expert Member

  #2
  Apr 15, 2011
  Joined: May 31, 2009
  Messages: 1,837
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Hili ni dili la kukwepa kulipa kodi mkuu. Ndo maana TRA wanasisitiza wafanyabiashara wote watumie mashine ili kuepuka huu ukwepaji wa kodi. Mimi niliwahi kwenda duka la mhindi mmoja nikanunua bidhaa baadaye ananiuliza kwa lafudhi ya kihindi "iko andika pesa yote au iandike kidogo". Nikamwambia andika kiasi nilicholipa. Yaani alitaka eti aandike kidogo kuliko nilivyolipa ili yeye akwepe kodi. Mbaya kabisa hii.
   
 3. Mpasuajipu

  Mpasuajipu JF-Expert Member

  #3
  Apr 15, 2011
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 838
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Sidhani km TRA watafaulu kwa zoezi lao hili, watu wengi hawana uelewa kabisa, na wafanyabiashara wanachukulia mwanya huu kuinyonya nchi yetu.

  Lakini wakati mwingine ukifikiria sana, unaona hakuna haja ya kulipa kodi inayoishia ktk MATUMBO YA MAFISADI.

  UNAKUTA FISADI A KAVIMBA TUMBO KM CHURA anahemea kifuani kakaa bungeni akipiga meza kugandamiza wananchi, akitoka hapo CHIPS KUKU NA BIA, NA POSHO YA ZAIDI YA LAKI 100 KWA SIKU.

  WATU WENYE TAALUMA KM MADAKTARI, MAFAMASIA, MAINJIANI, WAALIMU N.K wanaambulia pesa ya mkate.

  hakuna usawa, wapiga domo wanasiasa wanamaisha poaaa, wataalam hata bajaj hawana sasa ndio nini.

  Mie naona sawa tu wacha wakwepe kulipa hadi pale uwiano utakapokuwa na nafuu.
   
 4. Mzalendo80

  Mzalendo80 JF-Expert Member

  #4
  Apr 16, 2011
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,385
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Kulipa kodi ni muhimu kwa sababu kodi inaleta maendeleo ya nchi, lakini hatua tulifikia hapa Tanzania ya kodi zetu hazitumiki katika sehemu muhimu matokeo yake zinatafunwa na Mafisadi Kikwete na Majambazi aliyoyaajiri ili yamsaidie kuiba badala ya kodi yetu kuleta maendeleo. Mi naona ni sawa tu ukilipa usilepe hakuna tofauti yoyote kwa sababu maendeleo hatuyaoni.
   
 5. mfianchi

  mfianchi JF-Expert Member

  #5
  Apr 16, 2011
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 7,953
  Likes Received: 1,509
  Trophy Points: 280
  Kwa nyongeza tu pia TRA wangewezesha wafanyabiashara wauziwe mashine za EID,EFD ziuzwe kwa bei nafuu sasa mimi mwenye kiosk hiyo milioni moja hadi tatu nitapata wapi hata kama watanirudishia hao TRA itakuwa ni vigumu kila mfanyabiashara kununua hizo mashine,sheria zinasema kuanzia July kila mfanyabiashara hata asiyesajiliwa kwenye VAT lazima anunue hizo mashine
   
 6. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #6
  Apr 16, 2011
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 0
  etijina nalihifadhi

  kwa faida ya nani?
   
Loading...