๐—จ๐—ป๐—ฎ๐˜๐—ฎ๐—ธ๐—ฎ ๐—ธ๐˜‚๐˜๐—ฒ๐—ป๐—ด๐—ฒ๐—ป๐—ฒ๐˜‡๐—ฎ ๐—ฐ๐—ฎ๐—ฏ๐—น๐—ฒ ๐˜†๐—ฎ ๐—ถ๐—ป๐˜๐—ฎ๐—ป๐—ฒ๐˜๐—ถ ๐—ก๐˜†๐˜‚๐—บ๐—ฏ๐—ฎ๐—ป๐—ถ ๐—ธ๐˜„๐—ฎ๐—ธ๐—ผ ?

Teknolojia ni Yetu sote

JF-Expert Member
Apr 28, 2020
445
754
Umeshawahi kujiuliza unafanyaje kutengeneza Cable za Ethernet Leo nakujuza kwa kuwa Teknolojia ni Yetu sote.

images%20-%202023-09-28T084604.371.jpg


Najua unaweza kwenda kununua Cable ya Ethernet ambayo imeshatengezwa complete lakini unajua unaweza kutengeneza mwenyewe hizo cable.

Labda inawezekana cable uliyonayo imechoka, au unahitaji waya mrefu au bulk connector kimekufa ndo mpaka waje watu wa network seriously hapana Uzi huu ni wako.

Muhimu zaidi hakikisha vifaa vifuatavyo unavyo
  • UTP CABLE (UNSHIELDED TWITTED PAIR CABLE)
  • Modular connector (8P8C plug au jina jingine nj RJ 45
  • crimping tool pamoja na
  • cable Tester (sio lazima ila muhimu).



Bulk Ethernet cable huu ni waya ambayo utatumika kusafirisha data zako toka point A kwenda B ambapo zenyewe huwa zimegawanyika Kuna CaT5e au category 5e na cat6b ambapo cat6 ndo best alafu imara.

Ethernet cable zimegawanyika makundi mawili kuna straight through ambao ndo unatumika sana Kwenye local area network kwa Ajili ya kuunganisha kompyuta Kwenye network ni Kama aliternative solution ikitokea wifi imezingua unaweza tumia Cable.

View attachment 2764789

Crossover Sasa ni uwezo wa kutengeneza Cable ambayo inaunganisha kifaa kimoja na kingine yani kompyuta moja na nyingine PC to PC bila kwenda Kwenye router , switch au hub.

View attachment 2764788

Unafanyaje kutengeneza Cable ya Ethernet kwa Ajili ya intaneti
โ€ข chukua waya wako ya Ethernet cable
โ€ข kata gamba la nje Kama inch 2.5cm Kisha achanisha waya zilizopo ndani ziko 8 ila zimeundwa mbili mbili utazikuta 4.
โ€ข Anza kupangilia Sasa kama hivi
1) white orange
2) orange
3) white green
4) blue
5) white blue
6) green
7) white Brown
8) Brown ๐ŸŸค

networkz84.jpg


Zinyooshe waya zako ziwe Zimenyooka kabisa ziko (straight) Kisha zipunguze kwa kuzikata labda na crimping tool, mkasi zifikie mpaka inch 1.3cm unaweza weka RJ 45 Yako kuangalia Kama itafiti.

Weka waya wako full Kwenye RJ 45 ukianzia 1 mpaka 8 kuanzia kushoto Kwenye kulia kwaiyo namba 1 ni white orange na namba ya 8 ya mwisho ni Brown.

View attachment 2764786

Angalia kama waya zako zote zimefika Kwenye RJ 45 na hakuna waya mfupi ambao ujafika Kwenye pin za Rj45 pangilia waya vizuri.

View attachment 2764790

Angalia picha jinsi mtu alivyokosea kuweka Kwenye mpangilio sahihi

View attachment 2764785

Ukifanikiwa kuweka Kwenye mpangilio mzuri Sasa chukua crimping tool Yako wekq cable Yako Kwenye tundu la Rj45 crimp Sasa.

View attachment 2764791

Ukimaliza utaweza ku test cable Yako Sasa utaweza kutumia kwa Ajili ya kusafirisha data .View attachment 2764787
 
Back
Top Bottom