Unataka kuolewa na mwanaume wa aina gani?

Unataka kuolewa na mwanaume wa aina gani?

Kasiano Muyenzi

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2018
Posts
13,972
Reaction score
22,933
Mpendwa taja kila kitu, kwa mfano...

Urefu wake, rangi yake, lugha yake, elimu yake, wadhifa wake kazini, mwenye dimples, utu wake, hobbies zake, maadili yake, umri wake, nk.

Hayo utakayoyataja yawe ni maombi yako ya kila siku, nakuhakikishia utapata huyo mwenye sifa uzitakazo.

Maombi yako kwa Mungu wako yawe mahususi, maana maombi yasiyoeleweka huwa hayana majibu sahihi.

Kumbuka imani ni kuwa na uhakika kwa mambo yatarajiwayo, bayana na yasiyoonekana - Waebrania 11:1

Imani ina mrejesho mzuri, imani ni matumaini, imani inahitaji tamaa yenye nguvu.

Andika kwenye karatasi sifa 10 unazozitaka awe nazo mumeo mtarajiwa, zibandike kwenye dressing table yako chumbani kwako, halafu kila siku zisome na umwambie Mungu akupe huyo handsome wako mwenye sifa uzitakazo.

Mtegemee Mungu atajibu maombi yako.

Nasubiri shuhuda zenu mabinamu.

Mbarikiwe
 
Back
Top Bottom