Unataka heshima! Kaa mbali na watu

Unataka heshima! Kaa mbali na watu

uvugizi

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2012
Posts
1,351
Reaction score
1,100
Je unataka kumaintain heshima katika jamii , KEEP DISTANCE. Nikimaanisha usiwe wewe unapatikana popote wakati wote na kwa watu wote..

Distance ndiyo inatengeneza hadhi ya Mtu, usiwe mtu wa kujumuika na watu hovyo hovyo, angalia unaweza kuwa na tija kukusanyika hapo, jitahidi na penda kuwa na wewe siyo na watu.

Ukiwa mbali na mwanadamu ni rahisi kumpenda na kumfurahia na kuwa na kiu nae zaidi, hata dharau na machukizo hutaona.

Mungu mwenyewe yupo mbinguni nani anaweza kumfikia na kila mtu anamuheshimu, lakini tuliletewa yesu, tulimdharau mpaka tukamuua.

Katika falsafa ya tamaa kitu chochote kinachopatikana kwa nadra kinathamani kubwa, Madini yanapatikana kwa nadra sana na yapo ardhini.

Hata mtangazaji wa TV tungekuwa wote, tupo pale studio, asingweza kutangaza vizuri, kuna wengine wangecheka na kumdhihaki morphologically.

Kaa MBALI na nguru mbili (wanadamu). Na wengine tuishi nao kwa akili.

Thanks

Be inspired
 
Attachments

Asante Sana kwa ujumbe mzuri,hii ndio kanuni yangu siku zote. Ukikaa mbali heshima inakuja. Pia uwe mtu ambaye sio rahisi kupatikana yaani mpaka mtu akutane Na wewe basi iwe Ni kwa mambo ya msingi Sana.
 
Haswa, ukiwa unapatikana kirahis, basi watu wanakuzoea na jnachokwa haraka.
 
NOTED

bibafsi ninahako katabia mkuu
hili bandiko nadahani linazidi kunisisitizia umuhimu wa kuendelea kuwa hvyo..
 
Watendeeni wengine kama ambavyo mngependa wao wawatendee ninyi.

Unaweza kutafsiri au kuelezea kwa upana huo umbali unaousema na wa kiwango gani?

Vilevile sio sawa kusema watu walimchukia Yesu hadi wakamuua, alikuja ili afe atimize andiko na kuwa chanzo cha wokovu.

Unaweza kujiweka mbali na watu ikatafsiriwa vingine na ikawa na matokeo hasi kabisa.

Cha msingi ni kama ulivyomalizia, kuishi kwa akili na kujua nini kifanyike na kifanyike wakati gani. Wakati wa kunyamaza, wakati wa kusema, wakati wa furaha na wakati wa huzuni..
 
Jamii humtafsiri mtu wa aina hiyo kuwa anaringa,anajiskia au mjivuni.
Napo ni mtihani mkubwa kwa jamii inayokuzunguka.
 
kuna ukweli lakini hapa bongo watakuona "unanata"!!
 
Kuna ukweli hapa....ukitaka uheshimike hata kama huna chochote jambo na kwanza ni kuwa na Mipaka baina yako na Jamii inayokuzunguka...

Kw mfano Mimi nikiwa Chuon kuna baadhi ya watu wamenizidi Umri na kipato lakininwananiheshimu na nalijua hilo...na heshima waliyonayo ni tofauti na ninavyoona wakiwafanyia wengine....

Wale wanaokuzunguka wakikuzoea sana watakuwa wananakuona wa kawaida...

perfect 100%
 
Je unataka kumaintain heshima katika jamii , KEEP DISTANCE. Nikimaanisha usiwe wewe unapatikana popote wakati wote na kwa watu wote..

Distance ndiyo inatengeneza hadhi ya Mtu, usiwe mtu wa kujumuika na watu hovyo hovyo, angalia unaweza kuwa na tija kukusanyika hapo, jitahidi na penda kuwa na wewe siyo na watu.

Ukiwa mbali na mwanadamu ni rahisi kumpenda na kumfurahia na kuwa na kiu nae zaidi, hata dharau na machukizo hutaona.

Mungu mwenyewe yupo mbinguni nani anaweza kumfikia na kila mtu anamuheshimu, lakini tuliletewa yesu, tulimdharau mpaka tukamuua.

Katika falsafa ya tamaa kitu chochote kinachopatikana kwa nadra kinathamani kubwa, Madini yanapatikana kwa nadra sana na yapo ardhini.

Hata mtangazaji wa TV tungekuwa wote, tupo pale studio, asingweza kutangaza vizuri, kuna wengine wangecheka na kumdhihaki morphologically.

Kaa MBALI na nguru mbili (wanadamu). Na wengine tuishi nao kwa akili.

Thanks

Be inspired
Naunga mkono hoja,watu wakikujua sana wanaanza dharau,bora kujiweka mbali kidogo no matter hata wakuone unaringa but wakuheshimu
 
16 katika kitabu cha "the 48 laws of power by robert greene kimeeleza wazi kua ... USE ABSENCE TO INCREASE RESPECT AND HONOUR.

"Too much circulation makes the price go down: The more you are seen and heard from, the more common you appear. If you are already established in a group, temporary withdrawal from it will make you more talked about, even more admired. You must learn when to leave. Create value through scarcity."
 
Back
Top Bottom