Unatafuta ndoa safi asilimia 100? Haipo

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,956
22,138
Unatafuta ndoa safi asilimia 100? HaipoDISMAS, LYASSA
HIVI karibuni nilitembelea mikoa ya Arusha, baadaye Dodoma ambapo pamoja na mambo mengine nilikutana na baadhi ya watu na kuzungumza kuhusu mambo tofauti yakiwemo ya ndoa.

Karibu watu wengi niliokutana nao walizungumzia kero katika ndoa huku baadhi yao wakiomba kujua mbinu za kuachana kutokana na kile walichosema kwamba ndoa zimekuwa ni za shida, badala ya faraja waliyoitarajia wakati wanaingia.

�Kaka Lyassa, mimi ni muumini wako, nimekuwa nikisoma sana vitabu na makala ambazo umekuwa ukiandika kwenye magazeti, niliposikia unakuja, nikaona nije nikuone,� alisema mama mmoja ambaye aliomba uandikwe mkasa tu, si jina lake.
�Nisaidie la kufanya ili niachane na mume wangu maana sioni faida ya kuwa naye.�
Swali:Ulitarajia faida gani wakati unaingia kwenye ndoa?
Jibu: Nipate mtu ambaye naweza kusaidiana naye katika maisha,sasa amekuwa ni kero, mambo mengi anajifanyia, kwa mfano sina kazi, yeye ameajiriwa na pia ana biashara, sijui hata huo mshahara wala chochote kuhusu biashara yake, niko tu nyumbani, maisha yangu siyaelewi yanakoelekea.

Swali: Kwa hiyo kuachana ni tiba?
Jibu:Eeeh, bora nijue moja kwamba sina mtu.
Kuna watu wengi ambao matarajio yao kwenye ndoa yamekwenda tofauti. Tafiti zinaonyesha kuwa hali imekuwa mbaya zaidi siku hizi, idadi ya ndoa inaongezeka.
Huenda wewe ukawa ni mojawapo wa waathirika wa matarajio ya ndoa, ulitarajia mazuri, sasa mambo unaona yanakwenda mrama. Fahamu kuwa wewe si mtu wa kwanza.

Tafiti zinaonyesha kuwa asilimia kubwa ya ndoa hazina amani au matarajio yaliyokusudiwa. Kwa mujibu wa utafiti wa hivi karibuni wa chuo kikuu cha Loveology kilichoko eneo la West Hollywood, California, Marekani hakuna ndoa ambayo haina mikwaruzo.

Tofauti iliyoko ni akili za watu waliomo kwenye ndoa, kwamba wengine wanapokuwa na mikwaruzo wanaimaliza mara moja wakati wengine wanaikuza.

Mtafiti maarufu katika masuala ya uhusiano Dk D.Ava, ambaye ni kati ya wakufunzi wa uhusiano anasisitiza kuwa jambo la msingi kwa wanandoa ni kufahamu kuwa mikwaruzo ipo na kinachohitajika ni kwa wanandoa wenyewe kuwa na kawaida ya kukaa pamoja kuondoa tofauti zao.

Aidha utafiti mwingine wa chuo kikuu cha Curtin cha Australia, unaeleza kuwa siri ya wanandoa kuwa na maisha bora, kwanza kujuana kwa kina kabla ya kuanza uhusiano.

Tofauti na ilivyokuwa miaka mingi ya nyuma kwamba watu walikuwa wakijuana kabla ya kuanzisha uhusiano, siku hizi wengi wanakurupuka, na hicho ndicho kinachosababisha ndoa nyingi kuvunjika.

Inasikitisha sana kuona watu waliooana tena wengine kwa harusi za kifahari sana, ndoa zao hazina matunda wala kudumu. Kiapo kile walichokula pale mbele ya Watumishi wa Mungu kwamba tutapendana katika raha na shida kinakuwa batili, leo wala hakikumbukwi tena na badala yake kunatokea vitu vinavyoitwa nyumba ndogo na kubwa.

Kwa Wakristo ambao kimsingi kwao hakuna talaka, baadhi ya wanaume wamekuwa wakihama nyumbani na kuhamia nyumba ndogo au wanafanya siri na wengine wanalala pamoja hakuna tendo la ndoa wala kusemezana. Wengine tendo la ndoa wanapata baada ya kutumia nguvu, maana mwenzake hana hamu naye hata kidogo.

Matajiri, wenye vyeo, wasomi n.k nyumba zao zinatisha. Wengi wao wanaigiza tu kuwa wanapendana lakini hakuna ndoa. Sasa tufanyeje ili kuziponya familia hizi zinazosambaratika.

Inawezekana wewe au mimi ni mmoja wa wenye tatizo hili tufanyeje? Kuna baba mmoja ambaye ameoa lakini akawa ana msichana amempangishia na kumhudumia kwa kila kitu, kanisani ni mzee wa usharika kwa sababu ni tajiri, je wewe kama mwenye kuona hali hii unafanya nini?

Ni watu wangapi wanaimba kwaya leo wanafanya huduma mbalimbali kanisani na hata misikitini lakini nyumbani hakukaliki? Tunawasaidiaje watu wa aina hii au tunaishia kusema chini-chini tu basi? Tafakari chukua hatua.

MUHIMU KUZINGATIA:
*Ni muhimu kwa wanandoa kuepuka mazoea, yaani wawe wabunifu, kwa mfano wanaweza wakawa wanapeana zawadi za kushtukiza, au wanaandaliana safari za kushtukiza, hii inamfanya mwenzi wako aone kwamba unamkumbuka.

*Ni muhimu kuwa muwazi. *Mme/mke amsaidie mwenzake kutimiza malengo yake *Utayari wa kusamehe ni jambo jingine muhimu katika kuimarisha ndoa

*Usikumbushie makosa yaliyopita, lakini zaidi ya yote ukikosea kubali na kuwa tayari kuomba msamaha. *Usilale kabla hujamaliza kulizungumza tatizo au kero inayowasumbua kiasi cha kufanya msielewane.

*Kama kuna umuhimu, wa kupinga hoja ya mwenzako, basi fanya hivyo kwa upendo. *Ndugu yangu mmeoana kwa maana kwamba mnapendana, ni vizuri mshirikishe mwenzake mipangilio yako ya kila siku.

Zaidi ya yote jitahidi kutokasirika au kuendekeza tabia za kununa-nuna, kuna tatizo lizungumzwe yaishe.

Ambacho nataka kifahamike katika makala haya ni kwamba matatizo ni sehemu ya maisha, ndoa kama ndoa ni sehemu ya maisha, elewa kuwa utakuwa na mikwaruzo ya hapa na pale, cha msingi ni kujua namna ya kusuruhisha kasoro hizo, hatimaye muweze kwenda sawa.

Dismas Lyassa ni mtaalam wa uhusiano aliyesajiliwa na Serikali (Social Welfare Counselor) 0653777700
 
Siri moja ya msingi sana katika maisha yetu ni kuhakikisha tunakuwa na mawazo kwamba inawezekana. Ukiamini, kwanza ni jambo la msingi, halafu mambo mengine yanafuatia. Ukiamini kwa uhakika kwamba nataka kuwa fulani, kisha ukaanza kuchukua hatua za kuelekea kule ambako unataka, kwa hakika hakuna jambo ambalo litakushinda.

Ninachotaka kieleweke hapa ni kwamba msingi wa maisha ya watu wengi ni nafsi zao, kama unakata tamaa, ndio kusema ni sawa na kifo, ni sawa na kusema aaah basi inatosha, kwa hiyo inakuwa ni mwisho wa kuendelea kuwaza tofauti juu ya kile ambacho umekuwa ukikiwaza.

Wakati fulani miaka minne iliyopita niliwahi kukutana na jamaa mmoja akawa anaomba ushauri juu ya namna gani anaweza kufanya ili kuhakikisha anaishi vizuri kwenye ndoa yake hasa baada ya kumfuma mkewe akiwa na wanaume wengine katika nyakati tofauti wakifanya ngono.

Watu wengi wanapokuwa kwenye uhusiano na wanapoona wenza wao labda wamekuwa na uhusiano na mtu au watu wengine, wanafikiria kutalakiana, lakini huko ni kukosea, unapaswa kukaa naye na kuzungumza naye, ili kujua msingi wa yeye kuwa vile, kisha angalieni mbele, namna gani mnaweza kwenda mbele katika hali ya mafanikio.

Kabla ya kuwa naye, kwa watu walio wengi ni kwamba waliwahi kuwa na watu au mtu mwingine, ni kweli inauma kusikia au kuona ana mwingine, lakini si sahihi kufikiria kutalikiana, cha msingi ni kukaa na kuangalia ni namna gani uhusiano wenu unaweza kuendelea kuwa mzuri, kwa kuondoa msingi wa mmoja kuwa hivyo, yaani kuanzisha uhusiano na mtu mwingine.

Katika uhusiano kuna mambo mengi ambayo unapaswa kuyazingatia, lakini leo tutayaangalia mambo 20, ambayo naamini kwamba kama kweli utayafanyia kazi kwa dhati, kwa hakika uhusiano wako utakuwa mzuri na wenye kuvutia, wala hutakuwa na majonzi tena, baadhi ya mambo hayo ni yafuatayo;

1. Ufanye ubongo wako kutafakari kwa makini yale malengo ambayo umekuwa ukiyawaza kabla ya kuoana kwenu. Je, umewahi kutaka ndoa ya namna gani na sasa unafanya nini?

Waza namna gani unaweza kuwa na ndoa nzuri. Kwa hakika ukifikiria hilo, utafanikiwa. Maisha yetu yanajengwa na fikra, ukiwaza mabaya, utapata mabaya, ukiwaza mazuri, kwa hakika utayapata.

2. Kama kwa mfano ndoa yako tayari imeingia shida, endelea kutafakari kwanini ina matatizo na nini nifanye iwe nzuri?

3. Zaidi, penda kufanya mazuri kwa mwingine, acha kuwaza aaah mbona mimi namfanyia mazuri, halafu yeye ananifanyia mabaya. Endelea kufanya mazuri mengi kwa mwenzi wako hata yeye anaonekana kufanya mabaya, hatimaye naye atakuwa mzuri, kwa maana ya kukufanyia mazuri pia.

Atawaza aaah huyu mtu mbona namfanyia mabaya tu, wakati yeye ananifanyia mazuri, mwishowe atabadilika, ndivyo inavyoaminika kitaalam.

4. Mfanye mwenzi wako ajione ni mwenye thamani na umuhimu mkubwa katika maisha yako. Je, unamthamini mwenzi wako? Tafakari, chukua hatua.

5. Mara zote tafakari ni nini ambacho nikimueleza mwenzi wangu atakuwa mwenye furaha?

6. Tafakari kabla ya kufanya au kuzungumza jambo. Wengi wa watu wanaharibu uhusiano kwa midomo na mikono yao, wakati mwingine unaweza kufikiri unamfanyia mtu kitu kizuri, kumbe sio.

Ni vizuri sana kulizingatia hili. Wakati mwingine kama huna la kuzungumza, ni vizuri kukaa kimya, kuliko kuzungumza 'utumbo'.

7. Shukuru kwa kile unachofanyiwa. Wakati mwingine yawezekana mwenzi wako anakufanyia kitu au anakununulia kitu, hata kama hukipendi, mshukuru kisha sema; �Lakini ukininunulia na kitu Fulani siku ukipata fedha nitapenda pia� Usionyeshe kudharau, hata kama labda amekununulia kitu ambacho kutoka moyoni hujapenda.

8. Uwe msikilizaji mzuri. Tena wakati mwingine kama mwenzi wako anazungumza jambo, tulia msikilize hata kama labda ulikuwa unachezea simu nk. Ni makosa makubwa kwa mfano mwenzi wako anazungumza halafu wewe uko bize na kitu kingine ambacho labda wakati huo si cha lazima kukifanya.

9. Jali hisia za mwenzi wako.

10. Acha kauli za kulaumu au kutusi waziwazi, kama mwenzi wako amekukosea, pata muda wa kukaa naye faragha. Ni makosa makubwa kumtusi au kumsema mtu waziwazi, hapo ndipo huzaliwa mabaya mengi, baadhi yake ni vile unaweza kuona watu wakati fulani wakipigana waziwazi�kitaalam watu huwa hawako tayari kudharauliwa hadharani.

11. Acha kuwaza mambo yasiyowezekana. Kwa mfano ni makosa kuamini kuwa katika ulimwengu huu unaweza kumpata mwanamke au mwanaume ambaye ni msafi au mzuri asiye na makosa kwa asilimia mia. Kama unafikiria hilo, ni vizuri ukakaa pasipo kuoa au kuolewa, kwa sababu hayuko, hata Mungu anajua hilo.

Wakati mwingine baadhi ya mambo si makosa, bali yako tofauti na vile ambavyo tungependa iwe, kwa mfano wako watu wangependa kuona dunia haijaumbwa kama hivi ilivyo leo nk, japo ndio uamuzi wa Mungu.

12. Usitoe menno yenye kusababisha maumivu. Kama inatokea mwenzi wako anazungumza maneno yenye kusababisha maumivu, zungumza maneno mbadala, usikuze maumivu. Ongeeni kama watu mliokomaa, acheni kuendekeza migogoro.

13. Zifahamu vema tabia za mwenzi wako na namna gani unaweza kufanya ili kuhakikisha uhusiano wenu unakwenda mbele.

14. Badala ya kuwa na kitabu cha makosa ambayo mwenzi wako anayafanya, ni vizuri ukawa na daftari la mambo mazuri, ambayo mwenzi wako anakufanyia. Tafakari mazuri, zaidi kuliko makosa.

15. Andika tabia nzuri za mkeo au mumeo, badala ya labda sura yake mbaya nk.
16. Angalia ni namna gani unaweza kumfanya mwenzi wako kuwa na tabia nzuri zaidi ya alivyo sasa.

17. Uwe tiba kwa matatizo ya ndoa na uhusiano wenu kwa ujumla. Acha tabia ya kulalamika, kuipiga kelele ovyo.

18. Kumbukeni nyakati zile za furaha na fikra ambazo mmekuwa nazo kuhusu uhusiano wenu. Ongezeni manjonjo yale ya kupendana, na si kufikiria mabaya tu kama ilivyo kwa baadhi ya watu.

19. Angalieni ni namna gani mnaweza kushirikiana katika kuimarisha uhusiano wenu, pia angalieni namna ya kushirikiana katika kazi mbalimbali hasa biashara nk.

20. Ishi kana kwamba unakufa kesho. Mabaya yaliyofanyika jana acha yabaki kuwa ya jana, wala msiyape nafasi kuendelea kuwaumiza vichwa na akili zenu.

Waza leo na kuendelea mbele, achana na jana. Kumbuka watu walikuwa wanatambaa, leo ni watu wazima wanatembea, maisha ni mabadiliko, mtu anaweza kuwa mbaya leo, kesho akawa mzuri, na kinyume chake.
 
Tatizo nadhani ni kwamba watu tunapooana tunasahau kwamba tunaenda kuishi na mtu ambaye humfahamu kabisa. mmetoka familia tofauti, malezi tofauti, kila kitu tofauti, mnaanzisha familia yenu. kutegemea kuwa utamkuta mtu perfect 100% ni kujidanganya. kama unaweza kutofautiana na mama yako ambaye umetoka kwake, sembuse mtu mliyekutana barabarani?
la muhimu ni kujitahidi kusomana kwa upole, migongano lazima inatokea na sidhani kama kuna wanandoa ambao hawajawahi kuwa na migongano kabisa. kufarakani kunatokana na jinsi wanandoa mnavyoweza kukabili migongano inayotokea. na mara nyingi sana (mimi naamini hivi) migongano inaweza kutatuliwa vizuri sana na wanandoa wenyewe bila kushirikisha third part; mkishaanza kuingiza watu kwenye migongano yenu mjue mambo yameshaharibika.
 
Tatizo nadhani ni kwamba watu tunapooana tunasahau kwamba tunaenda kuishi na mtu ambaye humfahamu kabisa. mmetoka familia tofauti, malezi tofauti, kila kitu tofauti, mnaanzisha familia yenu. kutegemea kuwa utamkuta mtu perfect 100% ni kujidanganya. kama unaweza kutofautiana na mama yako ambaye umetoka kwake, sembuse mtu mliyekutana barabarani?
la muhimu ni kujitahidi kusomana kwa upole, migongano lazima inatokea na sidhani kama kuna wanandoa ambao hawajawahi kuwa na migongano kabisa. kufarakani kunatokana na jinsi wanandoa mnavyoweza kukabili migongano inayotokea. na mara nyingi sana (mimi naamini hivi) migongano inaweza kutatuliwa vizuri sana na wanandoa wenyewe bila kushirikisha third part; mkishaanza kuingiza watu kwenye migongano yenu mjue mambo yameshaharibika.


Kwa kuwa hakuna binadamu ambaye yuko perfect basi pia tujue hakutakuwa na ndoa ambayo iko perfect. Ni lazima kutakuwepo na misuguano ya aina moja au nyingine, mingine inavumilika na kuweza kuendelea na ndoa yenu na mingine haivumiliki na hivyo kusababisha ndoa kuvunjika.
 
wale waliosema kuna penzi/kupenda asilimia 100 sijui wapo wapi leo..?
 
Unaweza kumpenda mtu asilimia mia pamoja na mapungufu yake kama uko tayari kuyakubali. Hebu fikiria kama wewe mpenzio anakwambia nakupenda asilimia 50% utajisikiaje?
 
Unaweza kumpenda mtu asilimia mia pamoja na mapungufu yake kama uko tayari kuyakubali. Hebu fikiria kama wewe mpenzio anakwambia nakupenda asilimia 50% utajisikiaje?

kwa hio kwako bora mtu akuambie anakupenda 100%..ilhali unajua ni uongo?...
 
Afadhali wangu alinpa 70 % akasema 30 tukikaa vizuri kwenye ndoa ingawa akasema ajawahi na atawahi kutoa 100% ila akasema 99.99 anaweza kunifikiria so mkidanganyana nakupenda asilimia mia guna kimyo moyo.....ama nakupenda kuliko mama yangu mzazi we mi nakukimbiza kabisa..maana huu ni uongo w wazi
 
kwa hio kwako bora mtu akuambie anakupenda 100%..ilhali unajua ni uongo?...

Mwambie mumeo kwamba unampenda 70% tu halafu uone vumbi utakayotimuliwa. Ukimpenda mtu unapenda na mapungufu yake kama binadamu ndiyo maana kuna ile methali isemayo ukipenda basi chongo utaita kengeza. Mapenzi yangekuwa hivyo unavyotaka wewe nakupenda lakini sipendi hiki kile na hiki na hiki basi hakuna mapenzi ambayo yangedumu lakini watu wanafahamu kwamba ukipenda unapenda jumla jumla na kuyasahau mapungufu ya umpendaye.
 
Watu wengi wanadhani kupendana ni hisia, la kupendana ni uamuzi mtu unaotakiwa utawale mambo unayofanya.
Mfano, nimekutukana ila kwa kuwa nimeamua kukupenda, nakujibu kwa upole pamoja na kuwa nimeumia moyoni.

au labda nyumbani kuna njaa hunisemeshi kwa upole, mie nitakujibu tu kwa busara na kukufanyia mambo mema. Huo ndio upendo.

hizo hisia ambazo watu wanazichanganya na upendo ni (eidher shukrani, woga, admiration, desire, tamaa n.k) na zinakuja as a response ya kutendewa kwa upendo.

UPENDO NI MATENDO JAMANI SIO HISIA!!!!!!
TUNAPOAPA KUWA TUTAPENDA HADI SHIDA NA RAHA, NI KUWA TUTATENDEANA MATENDO MEMA, SIO TUTAJISIKIA TUNAPAA HATA KATIKA SHIDA!!!
amani mulio nje ya ndoa musikie,
Upendo ndo maana kujitoa kwa mtu na mwenzie ni vizuri kujuana, na kujiweka tayari kujitoa kimatendo na kujua tabia za mwenzio na uelekeo wake ili maadili anayoamini esp katika fedha, gender issues nk ili ujui kama unaweza kujitoa kwake.
 
Una uhakika gani? research hiyp imechukua muda gani na nchi ngapi? Zipo ndoa bora 100%
 
Pia ieleweke kuna tatizo kubwa la maangamizi ya uadilifu siku hizi. Tuna waalimu wengi, na kwa wingi wao wapo wanaopotosha ama kwa makusudi au kwa kutokujua. Nimewahishuhudia vijana wadogo ambao hata hawajafikiria kuoa wakijaribu kufundisha somo la mahusiano katika ndoa. Na nikagundua walikuwa wakiyazungumzia ya kusikia na wala sii waliyoyapitia kwa uzoefu katika maisha. Mda ulipofika na mwalimu yule wa mahusiano kuoa ndoa yake haikudumu miezi 6. Ninachomaanisha hapa ni kwamba kawaida ya mtu kusema ni jambo moja lakini utekelezaji kwa vitendo ni jambo jingine. Twapaswa fahamu suala la ualimu ni zaidi ya tunavyolifikiria, kwani kawaida ya watu ni kama computer ambae hujiendesha kwa kile alichoingiziwa(installed). Uliwahi kujiuliza ni kwa nini baadhi ya wanawake huridhia ndoa za mitala bila tatizo lolote huku kukiwa na wengine ambao ndoa ya mitala na sababu tosha ya kuvunja mahusiano?. Huu ni mfano mzuri wa software walioingiziwa maana kimsingi wate ni wanadamu wa nyama na mwili bali tofauti ni itikadi waliyoingiziwa. Pia nimeshughudia wanawake wengi wafanya biashara kule dubai na china wakifanya mambo ambayo hayajuzu kuandikwa hadharani na ni waliowaacha waume zao ubongoni. Sio wake tu hata waume nao ambao waliwaacha waume zao Tz, halikadhalika. Sasa nashindwa kuelewa nini tatizo maana kuna mawazo kuwa umasikini ndio tatizo kubwa. Lakini hawa wanayoyafanya haya sii masikini kiasi hicho. Wala hawakuachwa nyumbani wawe walinzi wa nyumba. Naamini hakuna tatizo lisilokuwa na suluhisho.
 
Back
Top Bottom