Unapotoka kusaliti (kuchepuka), unapokutana na mwenza wako hivi unajisikiaje?

Kwakweli sitokaa nisahau kilichotokea mwaka jana. Niliandamwa na mapigo na mojawapo kubwa kabisa pigo la kwanza ni kujua mume wangu wa miaka kumi alikua ananicheat. Nilimwamini sana toka uchumba hadi ndoa. Yaani na yeye alikua anajua jinsi ninavyomwamini so akatake advantage. Nilifaham baada ya mchepuko kunipigia kimakosa...uchungu nilioupata hauelezeki. Nina miaka 30s lakini uzito uliporomoka mpaka 47 kg. Nilipata pressure ya kushuka mpaka nilikua nashindwa kutembea kwa kizunguzungu na kuishiwa nguvu. Nilikua nilitaka niondoke, kikwazo kikaja sikua na kazi. Mpaka leo sijakaa sawa.wanawake na wanaume mnaochepuka mnaumiza sana sana wenzi wenu. Hata kama mtasameheana na kuamua kuendelea, ndoa kamwe haitakua kama mwanzo hata ufanye nini. Hamjui tuuu. Hiki kitu kinanitesa hadi leo nikikumbuka jinsi nilivyokua najitahidi kutimiza majukunu yangu kama mke,mama na mlezi wa familia.
Samehe hizo ni hatua katika maisha. Mungu atakusaidia
 
Stress alizompa umesoma lakini?..
Inabidi ajipe thamani na yeye kidogo

Ndio nimsoma, ila haifai pia ludharau au kumuta jina lolote... Haileti majibu... Maana mme akiwa kenge hata mke nae ankuwa kenge... Mtoto wa mwandamu ni mwadamu na mtoto wa kenge ni kenge...
 
Ungekua mwelewa sana usingemsaliti mkeo
Unafki at its' best

Hapana nilikosea na ilitokea hivyo kwasababu ya utani utani na mtu ila sio tabia yangu wala si tabia ya wife... Nimeacha... Na tunayajenga na wife maisha yanaenda flesh... Nikutumie ka selfie... Huoni tunavyo furahia
 
Ulishamdharau mkeo toka mapema ndo maana huoni shda yoyote kuchepuka huna aibu sababu hiyo.
Kwangu mimi ni ishu ndogo sababu tangu kabla sijaoa nilikuwa na wapenzi wawili kwa muda mrefu(mmoja ndiye akaja kuwa mke wangu) ambao walikuwa wanajuana vizuri na wote watoto wa kishua ila walikuwa hawana jinsi......hivyo nilikuwa nawachovya wote ndani ya muda mfupi yaani mmoja kwenye gari mwingine geto...nk nk....hiyo imenifanya niwe sugu mpaka leo nikitoka kuchepuka wala sioni tatizo lolote
 
Well said mkuu
Umeongea point sana
Bora wewe unahisi tu. Wengine ukiwa huko huko unaambiwa amka usali,huyo uliye nae ni shetani. Jasho linakutoka unadhani yupo dirishani.
Au mwingine utasikia siku hizi una kona za hapa na pale, na ujue sipendi. Huku yupo home na wewe unajivinjali na kimada.

Nahisi ikiwa too much, Mola anakuaibisha kiaina.
 
Kwakweli sitokaa nisahau kilichotokea mwaka jana. Niliandamwa na mapigo na mojawapo kubwa kabisa pigo la kwanza ni kujua mume wangu wa miaka kumi alikua ananicheat. Nilimwamini sana toka uchumba hadi ndoa. Yaani na yeye alikua anajua jinsi ninavyomwamini so akatake advantage. Nilifaham baada ya mchepuko kunipigia kimakosa...uchungu nilioupata hauelezeki. Nina miaka 30s lakini uzito uliporomoka mpaka 47 kg. Nilipata pressure ya kushuka mpaka nilikua nashindwa kutembea kwa kizunguzungu na kuishiwa nguvu. Nilikua nilitaka niondoke, kikwazo kikaja sikua na kazi. Mpaka leo sijakaa sawa.wanawake na wanaume mnaochepuka mnaumiza sana sana wenzi wenu. Hata kama mtasameheana na kuamua kuendelea, ndoa kamwe haitakua kama mwanzo hata ufanye nini. Hamjui tuuu. Hiki kitu kinanitesa hadi leo nikikumbuka jinsi nilivyokua najitahidi kutimiza majukunu yangu kama mke,mama na mlezi wa familia.
Mmmh umeongea kwa hisia sana mkuu, pole.
Kweli uchepukaji siyo dili.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom