Unapotoka kusaliti (kuchepuka), unapokutana na mwenza wako hivi unajisikiaje?

Ethical Ninja CEH

JF-Expert Member
May 16, 2011
3,695
5,032
Binafsi nilijaribu kuchepuka ( dhambi kwa mujibu wa imani yangu, na nimetubia hii dhambi sitoirudia tena hadi nakufa).

Huwa anajua nikibanwa na majukumu sana na muda ukiwa umeenda huwa nachukua hotel napumzika na huwa nampa taarifa, ni mwanamke na mama aliyetokea kuniamini sana kama mimi ninavyomuamini.

Sasa usiku mmoja sikuridi na nikawa nimepiga mechi ya nje ( demu wa kuota huko duniani ), wakati narudi home asubuhi, nikamuona mchumba anapita njia ya juu sijui alikuwa anaenda madukani, ikabidi mie nipite njia ya chini kumkwepa, nikakosa kabisa confidence ya kukutana nae wala hata kumsalimia uso kwa uso ( sijui aliona au hakuniona )...

Nikafika home nikaoga, nikawasha laptop nikaanza kupitia mambo mawili matatu, akarudi wala hakuniuliza kitu, akaniandalia chai akaniwekea mezani nae akaja kukaa pale tukaanza kupiga story mbali mbali huku tunakula ( moyoni mwangu nikawa nasema huyu kama akijua nilichofanya usiku wa leo sijui itakuwaje hapa, na cha ajabu mapenzi yake kwangu ndio yakazidi kweli kweli, utani mwingi, cheko nyingi na furaha iliyotamalaki moyoni mwake, ndio nikawa nakosa kabisa amani nikawa nafumba fumba macho kama usingizi vile umenipitia ili nimkimbie nikalale, kabla ya kunipa ruhusu ya kwenda kulala, anapotaka kutoka huwa lazima tupige magoti kidogo tuombe kwa pamoja ndio aendelee na issue zingine.. na kwenye kuomba ukawa mtihani mkubwa zaidi...

Kwa wengine mlipokutana na mazingira haya mlikuwa katika hali gani na mliweza kumudu vipi?
 
Akiii na mimi najiulizaga sana wanaoishi na wenzi wao huwa wanajisikiaje wakitoka kuchepuka.
Nilishawahi kuachana na bf miezi kadhaa nikapata mwingine. Yani kitendo cha kulala na yule kaka roho iliniuma namcheat mtu ninaempenda wakati hata hatuko wote.
Nililia usiku kucha.

Sent using Jamii Forums mobile app

Pole sana, ukiwa na upendo wa dhati kwa mtu ni lazima ikuhukumu, na kama una akili ya kibinadamu huwezi rudia kuchepuka kwa maumivu ya nafsi ambayo unayapata
 
Sinfull naona maombi yenu hayafanyi kazi shetani kakuzidi nguvu ee anaway

Usirudie tena na kama uliweka viapo vya kutokuchepuka na ukachepuka jua mshahara utaupata

Sent using Jamii Forums mobile app

Hakuna mwadamu alie kamilika, ( wote wamefanya makosa na hata kupungukiwa na utukufu ). Nilifanya makosa na dhambi, na nilitubia... ila namuandaa kisaikolojia nije ku confess kwa mwenzangu ili niwe na amani, siku mkaza kwa mda mrefu sana.. kwa hofu ya kumchafua na uchafu wa mwingine
 
Binafsi nilijaribu kuchepuka ( dhambi kwa mujibu wa imani yangu, na nimetubia hii dhambi sito irudia tena hadi nakufa).

Huwa anajua nikibanwa na majukumu sana na mda ukiwa umeenda huwa nachukua hotel napumzika na huwa nampa taarifa, ni mwanamke na mama alie tokea kuniamini sana kama mimi ninavyo muamini.

Sasa usiku mmoja sikuridi na nikawa nimepiga mechi ya nje ( demu wa kuota huko duniani ), wakati narudi home asubuhi, nikamuona mchumba anapita njia ya juu sijui alikuwa anenda anaenda madukani, ikabidi mie nipite njia ya chini kumkwepa, nikakosa kabisa confidence ya kukutana nae wala hata kumsalimia uso kwa uso ( sijui aliona au hakuniona )...

Nikafika home nikaoga, nikawasha laptop nikaanza kupitia mambo mawili matatu, akarudi wala hakuniuliza kitu, akaniandalia chai akaniwekea mezani nae akaja kukaa pale tukaanza kupiga story mbali mbali huku tunakula ( moyoni mwangu nikawa nasema huyu kama akijua nilicho fanya usiku wa leo sijui itakuwaje hapa, na cha ajabu mapenzi yake kwangu ndio yakazidi kweli kweli, utani mwingi, cheko nyingi na furaha iliyotamalaki moyoni mwake, ndio nikawa nakosa kabisa amani nikawa nafumba fumba macho kama usingizi vile umenipitia ili nimkimbie nikalale, kabla ya kunipa ruhusu ya kwenda kulala, anapotaka kutoka huwa lazima tupige magoti kidogo tuombe kwa pamoja ndio aendelee na issue zingine.. na kwenye kuomba ukawa mtihani mkubwa zaidi...

Kwa wengine mlipokutana na mazingira haya mlikuwa katika hali gani na mliweza kumudu vipi ?
Hapo ndipo watu wanapokuwaga wanafiki mkuu.
 
Daahhh mwanangu una bonge la mwanamke.

Kama anakushirikisha kusali kila anapotoka???


Usirudie Kumsaliti...ZUNGUKENI JUU CHIN ,KULIA KUSHOTO..KWENYE KUOA, OENI WACHA WAMUNGU KAMA HAWA SIO WAIGIZAJI.

MKE AMCHAYE MUNGU NDIO MKE.

The Devil puts a spoonful of honey into neighbor's Wife
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom