Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 58,636
- 220,438
Robert alizakiwa na pacha mwenzake wa kike Roberta. Walisoma vizuri ila matokeo ya kidato cha nne yaliwatenganisha. Robert alipata div 1ya point saba wakati Roberta alipata div 4 ya masister do wa town.
Robert alikwenda form five na Roberta alijifunza kozi ya ukatibu muhtasi. Baada ya miaka miwili Roberta aliajiriwa kwenye kampuni flani. Katika kipindi cha miaka mitano Roberta alipata watoto wawili wa Baba tofauti akiwa bado anaishi nyumbani kwao.
Robert alimaliza chuo na kuanza kazi kama mhandisi kwenye kampuni ya kigeni iliyosifika sana kwa malipo mazuri. Alipewa na nyumba ya kampuni, alinunua gari na alimudu kununua mavazi ya gharama kila akienda workshop nje ya nchi.
Roberta alipata redundancy kazini. Pesa aliyolipwa aliwekeza kwenye biashara ambayo haikwenda vizuri. Baada ya muda akiwa na ujauzito wa mtoto wa tatu aligundulika na HIV. Roberta alipata matatizo wakati anajifungua, alipoteza damu nyingi, alifariki na mtoto alibaki akiwa hana maradhi.
Baada ya msiba Robert aliamua kuwachukua watoto wote wa Roberta na kuishi nao. Aliweka mfanya kazi na dereva wa kuwapeleka watoto wakubwa shule. Watoto walisoma English medium. Robert alipokwenda kusoma shahada ya uzamili, mama yake alikaa na watoto yeye akiwa anawahudumia kwa kila kitu.
Kule chuoni Robert alikutana na mtoto wa waziri. Moyo wake ulipenda. Alimposa binti na kukubaliwa. Sasa mke wa Robert hataki ghasia nyumbani, anataka aanze familia safi yeye na mumewe. Robert aliambiwa aache kulipa ada ya English medium waanze kuweka pesa kwa future ya watoto wao.
Kuleta amani nyumbani Robert aliwapeleka watoto kwa wazazi wake ambao ni wastaafu. Watoto walisoma shule za kata na Robert kwa kujibana sana mkewe asijue alipeleka laki au laki na nusu kwa mwezi. Pesa hii ilitosha nauli tu ya watoto kwenda shule na kurudi.
Baraka nyumbani kwa Robert zilianza kupeperuka. Pigo la mwisho ni ajali aliyopata kazini na kumpa upofu. Pamoja na marupurupu aliyopewa, Robert hakuweza tena kufanya kazi. Pesa zilipokwisha mke alisogea pembeni.
Sasa hivi Robert analelewa na wazazi wake pamoja na watoto wa Roberta.