Unaponunua viwanja vya mradi wa viwanja, unaweza kufahamu ujirani?

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,595
215,273
Unaponunua nyumba au kiwanja ni uwekezaji wa kudumu. Ni muhimu ufahamu;
Kiwango cha uhakifu,
Utoro na mahudhurio ya watoto ma shuleni,
Kiwango cha kelele na udhibiti wake.

Haya mambo uyafahamu wakati umehamia, yanaweza hata kuathiri thamani ya nyumba au kiwanja unapotaka kukiuza. Mfano tu majirani wanapiga Mdundiko kila Jumamosi, au sherehe za kumtoa mwari kila mwezi, hamlali usiku mzima ni ngoma.

Unaweza kusema watoto wangu wanasoma Feza kwahiyo tatizo la utoro halinihusu. Ukifanya sherehe utaalika majirani na mtoto anaiga tabia za watu wanaomzunguka.

Kwenye viwanja vya miradi haya mambo utayafajamu vipi?
 
hahahaha, tuache na mdundiko wetu sisi wazaramo wewe nenda kanunue huko Masaki, mikocheni na msasani ukae....hahahahaha.
 
Unajikuta ni wewe tu mwenye fens mtaa mzima wanaelekezana ile nyumba yenye gate.

sasa wewe unakuja uzaramuni kwetu geti la nini, tutakuroga....huko wewe uwe mwenzetu tu utakuwa salama tu....mdundiko twende, singeli twende hukabwi wala huchaniwi nyavu..
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom