Unaongea lugha ngapi? (Binafsi Ninaongea Lugha saba(7)

Gumilapua

Gumilapua

JF-Expert Member
711
500
Naweza kusalimia na kupiga porojo kwa lugha za makabila yote ya tz isipokuwa kisukuma tu
Ukienda huko mwanza ndani ndani ukasema hujui kisukuma wanashangaa sana, maana wanaamini kisukuma ndio lugha kuu ya watanzania. Unajuwa hawakuelewi!!
 
princemikazo

princemikazo

JF-Expert Member
2,217
2,000
Kisukuma,Kichagga,Kimaasai cha longido,English
 
B

BRN

JF-Expert Member
1,319
2,000
Kwa kifupi pia. Ninaongea lugha zote saba ila kimchanganuo mzuri ni nne za kimataifa (kireno,kispania,kingereza, na kiswahili) hizi nyingine tatu naweza ziita national dialects sababu hazijavuka sana mipaka. Asante.
Mkuu kimakua kimevuka mipaka japokuwa baadhi ya matamshi yanatofautiana kidogo saba lakini haina madhara...nnonkwelelha!?
 
Hawachi

Hawachi

JF-Expert Member
12,126
2,000
Naongea kiswahili, kisomali,kizigua,Arabic.
 
Cameroan

Cameroan

Member
19
45
Oya jamaa nahitaji
mkuu mimi sijui kifaransa japo naelewa kidogo kwa kuwa nayo ni romance language ila naweza kupa msaada katika spanish
Nahitaji kujua kireno ntakupataje
 
Cameroan

Cameroan

Member
19
45
Habari zenu wakuu, natumai mu wazima wa afya.
Embu tufahamu ni lugha ngapi tunazozungumza.
Binafsi ninaongea jumla ya Lugha saba (7).

1.Kiswahili (swahili)
Ni lugha ambayo ninaongea na kuandika kwa ufasaha zaidi ya asilimia 90% ukizingatia pia ni lugha mama.

2.Kireno (Portuguese)
Hii pia ni Lugha ambayo ninaizungumza na kuandika pia kwa ufasaha sana kama ilivyo kwa lugha mama hapo juu.

3.Kingereza ( English)
Kutokana na kuwa lugha ya kufundishia (language of instruction) katika ngazi ya sekondari na pia ni second official language. Hapa kuna utofauti kidogo maana ninaweza kuelewa, kuandika na kusoma vizuri sana lakini linanitatiza kidogo suala la kuzungumza kwa ufasaha zaidi na ndio maana nimeiweka katika nafasi ya tatu. 70% fluency.

4. Kimwani (mwani)
Hii ni Lugha inayozungumzwa kaskazini mwa nchi ya msumbiji na pia ni lugha inayoshabihiana misamiati kwa zaidi ya asimilia 80% na kiswahili ndio maana imekuwa rahisi sana kuielewa na kuzungumza lakini katika uandishi wanatumia mfumo wa kireno.

5. Kimakuwa (makhuwa, macua, eMakhuwa)
Hii ni lugha inayozungumzwa na jamii kubwa takribani watu ml.3 katika mkoa wa Nampula nchini msumbiji (wazee wa mtupweshi watakuwa wananielewa vizuri hapa). Ninaongea na kuelewa kwa ufasaha lakini kuandika sifahamu maana ni lugha inayotumia sana "tone" katika matamshi.

6. Tsonga (Changana)
Hapa nazungumzia lugha inazungumzwa kusini mwa nchi ya msumbiji (katika mikoa ya Gaza, nyambani na Maputo) , kaskazini mwa nchi ya Afrika ya kusini (south africa) na zimbabwe. pia ni lugha inayoendana kiasi fulani na lugha ya kizulu. Ninaongea na kuielewa vizuri japo kuandika sio sana.

7.Kihispania (Spanish)
Ni lugha iliyopo katika kundi la Romance languages pamoja kireno, kiitaliano, kiCatalan, kifaransa n.k
Kihispania ni lugha ambayo imeshabihiana sana na lugha ya kireno na hapa ni tofauti kabisa na lugha nyingine maana hii Sikujifunza nimejikuta tu naielewa vizuri ingawa kuandika sifaham sababu sijawahi kufanya hivyo kutokana na utofauti katika Lahaja zake.
Nahtaji kufhamu kireno nitakupatje
 

Forum statistics


Threads
1,424,986

Messages
35,078,036

Members
538,184
Top Bottom