Unampenda lakini hakupendi

Unampenda lakini hakupendi

jangala

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2014
Posts
1,583
Reaction score
2,383
Habari wana JF,

Umemtumia mtu text lakini hajakujibu, meseji imepokelewa lakini hajajihangaisha kukujibu. Ukaamua kuiweka simu pembeni kuendelea na mambo mengine baadae unarudi bado unaona kimya hajakujibu.

Lakini ukitizama WhatsApp unaona yuko online busy akichati na kubadili DP na status. Unabaki ukijiuliza ana chat na nani mpaka asizione meseji zako na kuzijibu? Unabaki ukiendelea kujiuliza umemkosea nini?

Unaanza kujiambia kuwa labda amekuchoka. Inauma sana kupuuzwa na mtu umpendae kwa moyo wote. Je unajua kuna uwezekano nae anapitia kipindi kigumu kama hicho? Sawa anaweza akakwambia anakupenda au amekumiss, lakini anae mtu mwingine ambae anampenda haswa.

Unavyohangaika kumpigia, kumtumia meseji na asizijibu nae aweza kuwa anafanyiwa hivyo na ampendae. Anamtumia meseji, anamcall lakini nae simu zake hazipokelewi kama wewe. Nao wanapitia magumu kama wewe!

Kufikia hatua hii, unafikiri kukata tamaa juu ya huyo mtu lakini inakuwa sio rahisi. Unafikiri kumuacha huyo mtu, kumblock hata kum "unfriend" Fb lakini bado unaona moyo wako bado unampenda. Na unamatumaini ipo siku atarudi.

Kila muda unapotaka kuichukua simu yako unaomba Mungu ukute meseji yake lakini ukishika tu simu unakuta meseji ya TIGO wakikukumbusha kulipa deni ulilokopa kwa ajili ya muda wa maongezi.

Unajikuta unaichukia simu yako na unamchukia kila mtu anaye kuongelesha, unatamani uipasue simu vipande vipande. Lakini kwanini ifikie hatua hiyo? Kwa hali kama hiyo inaonesha kabisa wewe hupendwi labisa. Kwanini upoteze muda wako kumpenda mtu asiyekupenda?

Usimlazimishe akupende, wewe sio mzee kiasi kwamba huwezi kupata mtu mwingine. Usijipe stress kwa asiyekupenda kuwa na ujasiri wa kumuacha aende na wewe enenda na maisha yako.

Hata iwe vipi maisha lazima yaendelee.
 
Hiii IPO ,Soma moja INAitwa Mwaache Eendee ,,hiyo ilinipa ujasiri ni mwacha akaenda na kila kitu nilicho mnunulia ILa Leo Anajuta maana wengine Hawakawii Kumyanga'nya walivyo mnunulia ,Na siku hizi hata kifurushi sirushi ila kila siku anapiga tofauti na pale narusha kifurushi MB yupo Online hakuna hata asante WhatsApp
 
Ukifika hiko kipindi... jitafakar.. je ni haki kufanyiwa hivyo vituko?
Si rahis kufanya maamuzi kama haya.. lakini inakubidi kwa ajili ya mustakabal wa maisha yako. Akiuchuna.. na wewe kaa kimya kabisa.. wala usihangaike... Muombe Mungu akupe amani ya moyo na akusahaulishe huyo mtu. Then utasonga mbele
 
ila mapenzi bhana,
we unamuwaza kutwa nzima matokeo yake usiku kucha unamuota yeye tu..ukishtuka usingizin mawazo tayar yanarudi kwake...wakati yeye kwa upande wake hatumii hata sekunde moja kufikiria au kuhisi uwepo wako kwake
 
Habari wana JF,

Umemtumia mtu text lakini hajakujibu, meseji imepokelewa lakini hajajihangaisha kukujibu. Ukaamua kuiweka simu pembeni kuendelea na mambo mengine baadae unarudi bado unaona kimya hajakujibu.

Lakini ukitizama WhatsApp unaona yuko online busy akichati na kubadili DP na status. Unabaki ukijiuliza ana chat na nani mpaka asizione meseji zako na kuzijibu? Unabaki ukiendelea kujiuliza umemkosea nini?

Unaanza kujiambia kuwa labda amekuchoka. Inauma sana kupuuzwa na mtu umpendae kwa moyo wote. Je unajua kuna uwezekano nae anapitia kipindi kigumu kama hicho? Sawa anaweza akakwambia anakupenda au amekumiss, lakini anae mtu mwingine ambae anampenda haswa.

Unavyohangaika kumpigia, kumtumia meseji na asizijibu nae aweza kuwa anafanyiwa hivyo na ampendae. Anamtumia meseji, anamcall lakini nae simu zake hazipokelewi kama wewe. Nao wanapitia magumu kama wewe!

Kufikia hatua hii, unafikiri kukata tamaa juu ya huyo mtu lakini inakuwa sio rahisi. Unafikiri kumuacha huyo mtu, kumblock hata kum "unfriend" Fb lakini bado unaona moyo wako bado unampenda. Na unamatumaini ipo siku atarudi.

Kila muda unapotaka kuichukua simu yako unaomba Mungu ukute meseji yake lakini ukishika tu simu unakuta meseji ya TIGO wakikukumbusha kulipa deni ulilokopa kwa ajili ya muda wa maongezi.

Unajikuta unaichukia simu yako na unamchukia kila mtu anaye kuongelesha, unatamani uipasue simu vipande vipande. Lakini kwanini ifikie hatua hiyo? Kwa hali kama hiyo inaonesha kabisa wewe hupendwi labisa. Kwanini upoteze muda wako kumpenda mtu asiyekupenda?

Usimlazimishe akupende, wewe sio mzee kiasi kwamba huwezi kupata mtu mwingine. Usijipe stress kwa asiyekupenda kuwa na ujasiri wa kumuacha aende na wewe enenda na maisha yako.

Hata iwe vipi maisha lazima yaendelee.
This is my current situation Ila wanawake wakijua wanapendwa hua wanazingua kinoma
 
Back
Top Bottom