Unamkumbuka huyu mtoto?

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,789
288,015
Unamkumbuka huyu mtoto? Mwaka 2015 aliokotwa Abuja Nigeria akiwa na utapiamlo mkali. Wazazi wake walimtupa wakihisi wamezaa jini.

Raia mmoja wa Norway Anja Ringgren Lovén alimuokota, akamuogesha na kumpeleka hospitali. Akapata matibabu kisha akarudi kuishi nae. Akamlisha vyakula vyenye virutubisho ili kuondokana na utapiamlo mkali aliokua nao.

Mwaka 2017 katika ukurasa wake wa Facebok Anja aliandika maneno haya (nimefanya tafsiri isiyo rasmi);

"Siku ile nilipomuona huyu Malalika aliyetelekezwa niliumia sana. Nilipombeba ktk viganja vyangu nilijua kabisa HATAPONA. Kwa mara ya kwanza katika maisha yangu nilipoteza matumaini ya uhai kwa mtu niliyeamua kumsaidia.

Alisimama kwa shida, alipumua kwa shida, alikula kwa shida. Hata alipolia sauti ilitoka kwa shida. Kila kitu kwake kilikua shida. Kwahiyo nilijua atakufa. Lakini sikutaka afe kama mnyama. Sikutaka afe bila utu. Sikutaka afe bila jina.

Nikaamua kumpa jina. Nikamuita HOPE. Neno Hope kwangu ni la pekee. Miaka mingi iliyopita nilichora "tatoo" yenye neno HOPE mikononi. Sijaifuta hadi leo. HOPE kwangu inamaanisha.

H- Help
O- One
P- Person
E- Everyday

Kwa muujiza wa Mungu Hope alipona. Picha ya kwanza kushoto ni wakati ameokotwa. Inayofuata ni 2017 akiwa ameanza shule. Picha ya 3 kushoto ni mwaka 2018, Anja alipost kuonesha maendeleo ya Hope tangu alipookotwa hadi wakati huo. Na picha ya mwisho kulia ni December 2020 Hope akiwa nyumbani kwa Anja anapolelewa.

Kuna mengi ya kujifunza kwenye kisa hiki. Unajisikiaje ukitupia chakula mbwa wakati watoto wa jirani yako wanashindia uji wa chumvi? Unajisikiaje kila weekend unafuja hela kwenye kumbi za starehe wakati kuna ndugu yako anakufa kwa kukosa elfu 10 ya matibabu?

Mungu anapokubariki sio kwamba wewe ni bora kuliko wengine. Anakubariki ili ubariki wengine. Tunapotafakari kisa cha Anja na Hope tuendelee kukamilisha ujenzi wa nyumba ya Penina. Wewe unayesoma ujumbe huu ndiye Anja wa kuikoa familia ya Penina itoke kwenye zizi wanaloishi kama wanyama, na wawe na makazi bora.

1614566730483.jpeg
 
Sasa mkongwe kama wewe unashindwaje kutoa maelezo unganishi yahusuyo Penina

Maana hapa Penina yupoyupo tu hewani?
 
Soma kwa kituo ili uelewe vizuri badala ya KUKURUPUKA. Umewekewa namba za simu za wahusika kuhusu michango inayoendelea ya kurudisha furaha ya Penina. Kama unataka kushiriki piga simu namba husika ili upewe maelezo kwa kina. Ukongwe wangu hapa jamvini HAUHUSU KITU.

Sasa mkongwe kama wewe unashindwaje kutoa maelezo unganishi yahusuyo Penina
Maana hapa Penina yupoyupo tu hewani?
 
Soma kwa kituo ili uelewe vizuri badala ya KUKURUPUKA. Umewekewa namba za simu za wahusika kuhusu michango inayoendelea ya kurudisha furaha ya Penina. Kama unataka kushiriki piga simu namba husika ili upewe maelezo kwa kina. Ukongwe wangu hapa jamvini HAUHUSU KITU.
Mkuu umeleta maelezo marefu na picha za mtoto Hope aliyeokotwa Nigeria, unashindwaje kuleta maelezo a picha za mtoto wa Kihehe Penina wa hapa Pawaga Iringa?

Kuwa na siku njema mkuu.
 
Una UFINYU wa akili ndiyo sababu huwezi kuelewa. Huoni ajabu waliokwishasoma huu uzi HAWAJAKURUPUKA kama wewe? Narudia tena unataka details kuhusu Penina umewekewa namba za simu wahusika watakusaidia.
Mkuu umeleta maelezo marefu na picha za mtoto Hope aliyeokotwa Nigeria, unashindwaje kuleta maelezo a picha za mtoto wa Kihehe Penina wa hapa Pawaga Iringa?
Kuwa na siku njema mkuu.
 
sasa mkubwa,wote tusiende kwenye kumbi za starehe tutoe msaada,wale watumishi wanaofanya kazi kwenye kada hiyo huoni tuta hatarisha ajira zao?
 
Dada ana tatoo mwili mzima lakini ana moyo wa kipekee pengine kuliko wale wanaohisiwa kumpenda Mungu sanaaa.

NB
"life style ya mtu sometimes haihusiani na kilicho ndani ya moyo wake na ukimuona mtu mcha Mungu sana haimaanishi ana hofu ya Mungu au ni mtu bora zaidi kuliko wengine,
Kiufupi Don't judge people unless you know them especially their story".
 
Back
Top Bottom