Unamkumbuka huyu mtoto?

Unamkumbuka huyu mtoto?

Wakati mwengine ukiyafikiria sana maisha na yanayotokea duniani sizani kama kuna furaha ya bank uwe na mipesa mingi ni bora kusaidia watu kama hawa wenye huitaji maana izi pesa tunakuja kuziacha.... Naumia nikiona ivi maana nina mtoto na huwa najiuliza ivi siku mimi sipo mama yake hayupo how is gonna care?!! Tusaidie kwa kadiri ya uwezo wetu hakuna aijuae kesho
 
Ni sawa lakini umeelewa lengo la mleta Mada? Nafikiri iyo story ameitoa kama mfano wakuigwa ili tuweze kumsadia huyo aliyemtaja hapo ambaye ni mtanzania mwenzetu soma kwa utulivu... Hajamanisha iyo story niya leo au jana umeona kwenye picha mtoto tangu aokotwe na alivyo sasa... Hapo nini huwelewi mkuu???
Hizo picha zinasambaa mtandaoni huu mwaka wa tano
 
Sasa mzeebaba huyo penina ndo huyo dada wa kithungu au ni yupi?

As a teacher hebu tupe kitu kinachosimama bana.
 
Unamkumbuka huyu mtoto? Mwaka 2015 aliokotwa Abuja Nigeria akiwa na utapiamlo mkali. Wazazi wake walimtupa wakihisi wamezaa jini.

Raia mmoja wa Norway Anja Ringgren Lovén alimuokota, akamuogesha na kumpeleka hospitali. Akapata matibabu kisha akarudi kuishi nae. Akamlisha vyakula vyenye virutubisho ili kuondokana na utapiamlo mkali aliokua nao.

Mwaka 2017 katika ukurasa wake wa Facebok Anja aliandika maneno haya (nimefanya tafsiri isiyo rasmi);

"Siku ile nilipomuona huyu Malalika aliyetelekezwa niliumia sana. Nilipombeba ktk viganja vyangu nilijua kabisa HATAPONA. Kwa mara ya kwanza katika maisha yangu nilipoteza matumaini ya uhai kwa mtu niliyeamua kumsaidia.

Alisimama kwa shida, alipumua kwa shida, alikula kwa shida. Hata alipolia sauti ilitoka kwa shida. Kila kitu kwake kilikua shida. Kwahiyo nilijua atakufa. Lakini sikutaka afe kama mnyama. Sikutaka afe bila utu. Sikutaka afe bila jina.

Nikaamua kumpa jina. Nikamuita HOPE. Neno Hope kwangu ni la pekee. Miaka mingi iliyopita nilichora "tatoo" yenye neno HOPE mikononi. Sijaifuta hadi leo. HOPE kwangu inamaanisha;
H- Help
O- One
P- Person
E- Everyday

Kwa muujiza wa Mungu Hope alipona. Picha ya kwanza kushoto ni wakati ameokotwa. Inayofuata ni 2017 akiwa ameanza shule. Picha ya 3 kushoto ni mwaka 2018, Anja alipost kuonesha maendeleo ya Hope tangu alipookotwa hadi wakati huo. Na picha ya mwisho kulia ni December 2020 Hope akiwa nyumbani kwa Anja anapolelewa.

Kuna mengi ya kujifunza kwenye kisa hiki. Unajisikiaje ukitupia chakula mbwa wakati watoto wa jirani yako wanashindia uji wa chumvi? Unajisikiaje kila weekend unafuja hela kwenye kumbi za starehe wakati kuna ndugu yako anakufa kwa kukosa elfu 10 ya matibabu?

Mungu anapokubariki sio kwamba wewe ni bora kuliko wengine. Anakubariki ili ubariki wengine. Tunapotafakari kisa cha Anja na Hope tuendelee kukamilisha ujenzi wa nyumba ya Penina. Wewe unayesoma ujumbe huu ndiye Anja wa kuikoa familia ya Penina itoke kwenye zizi wanaloishi kama wanyama, na wawe na makazi bora.

Tuma mchango wako kwenda (M-Pesa) 0743339247 au (Tigopesa) 0714639248 Gwakisa Mwakitega, au (AirtelMoney) 0783514607 Even Nassary. #RudishaTabasamu #LetLoveLead #MalisaGJ #GiftedHeart

View attachment 1714402
Sometimes nafikiria watu kama hawa watepewa favor peponi kuliko hawa wahutubiaji lakini matendo zeroo
 
Ila mabeberu wana utu sana.
Unaijua idadi ya Watoto na kina Mama waliouawa na hao Mabeberu huko Iraq? Afghanistan? Libya? Syria? Palestina na kwingineko? Unaijua idadi ya wanaouawa kwenye nchi mbalimbali kutokana na mikakati ya Mabeberu ya kupora mali hasa huko DRC na kwingineko?

Usidanganyike na hiyo picha tu,
Kila jamii ina watu wazuri na ina watu wabaya,sio Mabeberu wote ni watu wazuri na sio Race zingine watu wake wote ni wabaya,

Jipe muda,tafakari.
 
Hivi huyu mama na mtu kama Rashid Gwajima nani ana sehemu yake katika ufalme wa mungu?
 
Sometimes nafikiria watu kama hawa watepewa favor peponi kuliko hawa wahutubiaji lakini matendo zeroo
Pepo haiko hivyo hata usaidie Dunia nzima kama hujafanya katika misingi anayotaka Mungu ni ZERO.
 
Jana kuna mshenzi mmoja kapiga mbwa wangu mguu..mbwa akawa anachechemea..jiran yangu raia wa ujeruman ni daktar wa mifugo..ana deal na mbwa tu..nikampeleka pale..ile kufika na jamaa akamuona mbwa akamshika..akamlaza kitanda huku akitamka ooh bby what happened to you...akamchoma sindano..akamtundika drip....akampa tiba ya daraja la kwanza..leo asubuhi kaja kumjulia hali..wazungu wema sana...
 
Unaijua idadi ya Watoto na kina Mama waliouawa na hao Mabeberu huko Iraq? Afghanistan? Libya? Syria? Palestina na kwingineko? Unaijua idadi ya wanaouawa kwenye nchi mbalimbali kutokana na mikakati ya Mabeberu ya kupora mali hasa huko DRC na kwingineko?

Usidanganyike na hiyo picha tu,
Kila jamii ina watu wazuri na ina watu wabaya,sio Mabeberu wote ni watu wazuri na sio Race zingine watu wake wote ni wabaya,

Jipe muda,tafakari.
Ndio kuna wabaya pia.

Ila hawafikii ubaya Wa waarabu,wahindi,wachina watuchukia sana sisi ngozi nyeusi,eti wanadai ngozi nyeusi ni laana.
 
Ndio kuna wabaya pia.

Ila hawafikii ubaya Wa waarabu,wahindi,wachina watuchukia sana sisi ngozi nyeusi,eti wanadai ngozi nyeusi ni laana.
Utakua una chuki zako binafsi tu na hizo kabila ulizozitaja,So hata ukieleweshwa huwezi kuelewa coz umesha kua brainwashed,

Black wanauawa kila siku ndani ya US na Whites au wewe unaishi Dunia gani ambayo hizi habari zinakua hazikufikii?
 
Back
Top Bottom