Unamkumbuka Crush wako wa utotoni? That was real and only unconditional love you will ever experience

Mwana wa Shabiri Primary Dom sikumwambia chchte japo alionesha kila dalili ya kunipenda (au alikua anazuga tu ata cjui kwa kweli)

Secondary alikua mwana wa Sovella apo apo K Bata pia sikuambulia kitu

Yan ata nikiwa bafuni nlikua naoga kistyle kwa kuhisi pengine ananiona huko kwao

Dah ila nilikuaga mjinga mm
 
Josefine Mwakililo sitamsahau, babaake alikua tajiri tu anatupeleka shule daily na gari 5×4 miaka ya 80.Daah alikuja kufa kwa ajali ghafla familia ikaparaganyika mbaya.

Mdingi wangu akaingilia kati kumtetea mke naye akamalizwa.
Sijamuona Josefine mpk leo maana tulihama baba alipokufa.
Ila tulipendana sana na yule mchumba
Kumbuka tuko 8-10 yrs
 
Elizabeth popote ulipo,Kama Bado uko hai Mungu azidi kukupa afya na furaha tele maishani.Nilikupenda Sana japo haukuwahi kujua Kama ninakupenda Sana,hata nilipo maliza Drs la saba nilikuwa nikija mara mojamoja shuleni ili angalau nikuone na nilipokuwa nikikuona basi roho yangu kwatuuu!narudi nyumbani na furaha tele.Mara ya mwisho kukuona

Ni kwenye mahafali yako ya drs7 nilikuja kwenye mahafali hayo kukuuona wewe tu.Nilipohisi kuwa Sasa ninaweza kukwambia kuwa ninakupenda,nikakutafuta mtaani kwenu nikaambiwa umechukuliwa na baba yako kwenda mkoani Kilimanjaro.Dah huu Uzi umenifanya nikukumbuke japo ni miaka mingi Sana imepita.
 
Asante kwa kuleta uzi huu hapa mkuu! Nina mengi ya kuandika kuelezea stori ya crush wangu lakini acha tu nifupishe maana huwa nikisimulia huwa kama ni love story inafaa hata kuchezewa movie! #Huyu dada kwa mara ya kwanza nilikutana naye kanisani, nilikuwa darasa la tatu, na umri wangu wa miaka kumi! Kwa mara ya kwanza moyo ulipasuka kwa mapenzi, yule dada aliingia moja kwa moja kwenye chumba cha moyo akakaa humo nakuishi. #Dada huyu alikaa moyoni kwa miaka 14 bila kutoka na kwa muda wote huo sikuwahi kumwambia ingawa wakati ule wa utoto aliweza kunigundua kama nipo nyang'anyang'a kwake coz body language zetu ziliongea hususani macho kila tulipokuwa tukikutana hasa kanisani, hakuna mahubiri yalikuwa yakiingia, yeye ndo alikuwa hubiri langu! Shida katika utoto ule wa kishule ya msingi ilikuwa ni uoga( udomo zege). # Uncondition love yangu kwa huyo dada ilikuja kushuka asilimia zake nikiwa na miaka 24. Kwa sasa yupo kwenye ndoa yake! Na mchango nilitoa, na tu marafiki.
 
Kipindi nipo primary std 6 niltokea kumpenda mwanafnz mwenzang aitawe L, yaan nilkua nikimuona bas najawa na furaha na tabasamu, uzuri wake tulikua viongozi idara 1, bas nilkua namuonea aibu flan tukiwa pa1 tunasimamia wanafunzi lol
 
Mimi nlimpendaga winifrida bahati mbaya alianzishwa primary nyingine mbali na mm...Kama ningelijua kuandika ningemuandikia barua kipenz changu yule


Mwingine Mariam yani nilimpenda sana imagine nanunua kachori 3 ila nakula moja nataman nmuone lkn kila nkimuulizia simpati
 
Nimekumbuka mbali Sana asee crush wangu alikua mcheshi Sana yule mtoto na Mungu amtunze tu I miss moments z kununiana tukiwa tunatoka pale queen victoria
 
Mimi nlimpendaga winifrida bahati mbaya alianzishwa primary nyingine mbali na mm...Kama ningelijua kuandika ningemuandikia barua kipenz changu yule


Mwingine Mariam yani nilimpenda sana imagine nanunua kachori 3 ila nakula moja nataman nmuone lkn kila nkimuulizia simpati
Utakuwa mwanaume wa Dar, unakula makacholi
 
mimi mpaka leo napenda sana matured women....iko hivi mimi crush wangu wa utotoni na mpaka leo hajui kama nilimpenda kiasi kwamba eti ilibaki kidogo nimwambie ukweli, wakati huo mimi nina kama miaka 9 kuelekea 10 yeye ana miaka 30 kasoro sijui nilikuwa na mashetani gani...

ila mpaka sasa sina interest na wasichana wadogo i always feel comfortable with them ladies wakubwa....na moyo wangu unapata tulizo kabisa na kuhisi amani zaidi...
 
Back
Top Bottom