Unamkumbuka Crush wako wa utotoni? That was real and only unconditional love you will ever experience

Nimemkumbuka Dotto Manyasi. Tulisoma Pamoja Iseni Primary School, Nyegezi Mwanza. Nilikuwa tukitoka Shule saa 8 mchana, jioni saa 10 nafunga safari mpaka kwao Nyegezi kijiweni, Naangalia nyumba yao mpaka saa 12 jioni narudi home. Moyo umefurahi kabisa.
Sikuwahi kumtamkia chochote zaidi ya kutabasamu kila tukigongana macho.
Nashukuru Mungu nilifanikiwa kupata picha yake siku ya Graduation ya la Saba. Mpaka sasa ninayo.
Hahahahahah
 
Dah... mtoto pendo... nisipoenda class vidudu hasomi, analia siku nzima hadi arud hom anione....

Nami nikampenda, sipandi piki piki 110 ya baba adi niwe na pendo

Pendo roho iliniuma baba angu alipoamua darasa la kwanza nikasomee kwetu milimani... huo ukawa mwanzo wa kukupoteza pendo.

Ninarud darasa la3, pendo wamehama, haijulikani wapi... naangukia kwa salma... mtoto mixer mrangi na muarabu... salma anakua serious hanipendi hadi siku nawakuta wanacheza kimama mama... nakaitwa niwe baba... penzi likawa la kweli... nikitoka shule salma lazma aje kwetu... nimuoneshe mbwa wangu simba.. mbwa anayeogopeka mtaani kwetu nyuma ya mskiti wa masjid qubah.... ah salma tukicheza kombolela twaenda jificha juu ya magunia ya mahindi yalopangwa hadi juu... tunatafutwa hadi tunaitwa tujitokeze...

Tunahamia chang'ombe hadith yangu na salma nayo inaishia hapo...

Najikuta namtaman nankumpenda mtoto anjelina... ila yuko sirias na shule, hataki ujinga... ananikataa

Maisha yanaenda kwa kasi huku na kule namaliza form4... nakuwa rafiki na jamaa mmoja... urafiki kupitia rafiki.

Naenda kumpitia nyumbani kwa jamaa twende club84, lahaulaaaah... namkuta pendo... kumbe jamaa ni kaka ake pendo... pendo hanikumbuki na mm naingia ganzi coz imekua pisi kali balaaaaaaaa.

Baada ya muda namkumbusha... dah pendo anafurah... tunaanza urafiki.... baada ya muda kidume naomba game...

Pendo anakolea kwa shoo za kibabe na kisela.... lkn anakuja gundua nina pisi nyingine..... anapata tabu sana hadi jamaa ikabidi aniombe nimsaidie dada ake asije kufa kwa tatizo la moyo... mimi usela unakua mwingi nimekolea kwa mtoto wa kiswazi mtoto wa kawaida sina ilanhana complication... mtoto wa kiswazi ila anaishi kizungu..... kuhama mkoa inakua suluhisho kwa pendo... anaenda kwao moshi....

Maisha yanaenda kwa kasi ya ajabu...

Siku nipo nam hotel, nakula zangu bia, mara zinaingia pisi kama 3 ivi kali balaa... kuchek moja naiona kumbe ni salma... dahhh.... bila kujizuia kaja tukahug.... salma kachora mitatuu... salma anaonekana kawa paka shume... anaonekana ukiingia kiboya unapigwa ela na mzigo hupati... kumbe yana apointment na mbunge fulani wakale raha..

Salma ananipa namba.... baada ya kuondoka na yule mbunge... usiku salma ananichek ananiambia amelewa sana anaomba nikamchkue nmpeleke nyumbani... dah

Kiukweli sikuweza kubisha, namkuta dodoma hotel, anaingia kwe taksi ya jamaa yangu yasin mzee wa kuwalamba... jinsi alivyo jambazi kumbe salma keshanitathmini kajua labda nna maisha... dah kumbe me kachala tu mzee wa mishe mtu wa watu... akiwa amenikumbatia ananiambia hawez kwenda kulala pekeake kwanza kwao hawatamfungulia.... dah.. kidume namwambia yassin anipeleke geto.....

Mwezi na zaidi salma anakolea... mara paap... siku anakuja na kikaratas cha hospital... kapima ana mimba, yuko pia na kipimo cha mkojo kwamba kama siamini apime tena mbele yangu... lahaulaaa

Salma uyu uyu mtoto wa mjini mwenye mambo mengi... aaah siwez zaa na mwanamke wa ivi mimi... najisemea akilini

Salama anagoma kutoa mimba anaamua kuzaa..

Mishe za hapa na pale... huku na kule tunapoteana na salma...

Maisha yanaendelea...
Umeitendea haki ID yako, ndugu storyteller.
 
Enzi hizo form one, namkumbuka sana huyu binti wa kuitwa Amina. Mtoto mweupe amejaliwa mguu na macho makubwa! Mtoto wa kitanga nilikua namuimbia wimbo wa Juma Nature Sonia mpaka leo nikiskiza huu wimbo namkumbuka
 
la tatu yeye la tano.

alikuwa mweupe na ana akili sana,tatizo malezi ya kwao ndio ilikiwa mtihani hata kuonyesha dalili kwamba anafagilia hizo habari.
nakumbuka kuna jamaa walikuwa la 6 ndio walikuwa wanampigia hesabu yeye na rafiki yake maana nao walikuwa wawili.

shida ikaja kwamba huyu alikuwa ananidharau maana kaniacha mbali,ila ilikuwa ni kama ujiko kuwa karibu na mimi,kwa kipindi hicho nilikuwa na mvuto nikiri sijui siku hizi imekuwaje,halafu huyo rafikiye ambaye ni ndugu pia alikuwa la nne yeye naye alikua msumari alikuwa akinipenda wazi wazi hafichi,ila mimi sina habari naye nikikutana nao fagio ni kwa huyo mkubwa.miaka ikakata akamaliza shule nikabaki na huyu mwingine shule,picha linaanza akapevuka.bwana wee kwanza aliwaka zaidi halafu akajaa kidogo ikawa tatizo shule nzima,ikabidi mjuba nihamishe mawazo hapo,ikawa kama nimerogwa sasa yaani mpaka natamani kengere ya kutoka isigongwe.
huyu pamoja na kupendeza hajawahi kuficha hisia zake,shida ni kwamba hatukuwahi kufanya chochote zaidi ya mapenzi ya vipepeo.

nimemtafuta fb na kumtumia sms,ili walau nimwone waapi,na picha kaweka maandishi ya quran ni kama kawa mwislam zaidi ya alivyokuwa kule mwanzo.
 
"Victoria" roho yako ilale mahala pema peponi. Nikiwa darasa la saba (nimehamia shuleni kwa akina Victoria) yeye la nne, alinipenda sana yule binti nami nikampenda sana, alikuwa mrembo hasa, mweupe, mrefu umbo lake sawia. Nilipoenda form one mawasiliano yalipungua ila nilipokuwa narudi likizo ilikuwa kama ndo tunafukuziana

Lakini alipata usumbufu mkubwa sana kijijini kipindi nipo shuleni maana hata watu wazima aliwatoa udenda, lakini mwishowe alishindwa kuhimili presha za mtaa, akanaswa na jamaa mmoja, akampachika mimba, niliporudi baada ya kumaliza form 4 nikamkuta mjamzito, alivyoniona alilia sana nikamuonea huruma ila nikakubali yaishe, niakondoka zangu kuja Dar 2005 kuendelea na masomo, huyo jamaa alimuoa lakini "Vicky" hakuishi muda mrefu sana katika ndoa yake, nafikiri aliishi miaka 4 hivi, alifariki, niliambiwa alikufa kwa HIV ambayo ililetwa na mume wake. Kifo chake kiliniuzunisha sana na nililia sana.

Hata mke wangu nilienaye leo ni mzuri lakini Vicky ilikuwa ni habari nyingine, kweli kuna watu wengine Mungu aliwaumba kwa upendeleo mkubwa sana kama Vicky.

"If you need something too much, let it go, If it comes back it is yours, if it doesnt it is bcoz it was never ment"
 
Kenneth mtoto wa kipare , form one F scene inaanza anaingia class day 1 moyo ukashtukaa. Mtoto mweupe nywele kama shombe hivi smart from head to toes mwendo sasa sijui vilikua vizuri kweli au ni kupenda kulinipofusha
Wadada wengi class walimpenda mm ndio uwih ila uwezo wa kumwambia sina kwanza nlikua mshamba tu sketi nlienda na mama kushona ndefu haivutii hizo buti sasaa hata asingeniangalia mara mbili.

Nilichora mpk jina lake kwenye sare yangu ingawa haikudumu mhula wa pili tulivyorudi kenny kahama niliumia kupita maelezo.

Nafika chuo nakutana naye anasoma medicine aliniaproach sema kipindi hicho sijui nlikua nnamuonaje tena nlimuumiza mpka alijuta kunijua nlimuacha hadi alilia mkaka wa watu
 
Richie W. aka Richie Richie ( huyu tulipendana wote hadi tunamaliza lasaba B ila wote tulikuwa tunanata hakuna aliyetaka kumsemesha mwenzake. Tukawa tukasalimiana tuu na kupeana tabasamu basi). Sekondari tulipangiwa shule jirani tukawa tunaonana njiani saa ya kutoka au asubuhi kuingia shule.... alipopangiwa Minaki tukapotezana mazima hadi leo. Nilifatilia post za A level shule yao nikajua kapangiwa Minaki.... crush ya primary ikaishia hapo.)

Nkundwe ....( huyu hakujua kama nilimzimikia ila sababu alikuwa handsome waschana wengi walikuwa wanamsonga.... sikumbuki vizuri kama alihama tukiwa lasaba B au baada ya hapo alihamia ughaibuni.

Baada ya hapo nikawa mkaksi hadi nilipoingia chuo ndo nikaanza mahanjam .
Nilijua sana ulinizimia ata Mimi nilikuzimia sema tuyarudie
Kasie Mahaba Matata
 
Upendo ni Mungu.

Upendo unapokuwa asili bila mapenzi ndani yake ni utu.

Mungu akutie nguvu, hatuijui kesho yetu, si ajabu baada ya kukuona ukampa tumaini na nguvu kutoka ndani yake ya kuinuka tena kwa kutia bidii kwenye mazoezi.

Kila la kheri.
Kasinde...

Umeandika mistari fulani ambayo natamani kila mtu angelielewa
 
Uzi mzuri sana nimesoma yote mimi wangu ni ritha Livingston na fatuma fety na Sian hawa asee huniambii kitu nishawafukuzia Sana na nikawakosa mpk najionaga na mkosi flan ila fresh
 
Anitha alinitamkia ananipenda tulikutana tuition tukiwa darasa la pili alinipenda sana nikatokea kumpenda Dah! Kwao walikuwa na duka kuna wakati yeye alikua anauza nikienda dukani kununua kitu cha mia 500 anaweka 1,500 Mama akashtuka ikabidi nimwambie ukweli nilimpenda Anitha nilikua napenda hadi magari ya Baba yake
 
Anitha alinitamkia ananipenda tulikutana tuition tukiwa darasa la pili alinipenda sana nikatokea kumpenda Dah! Kwao walikuwa na duka kuna wakati yeye alikua anauza nikienda dukani kununua kitu cha mia 500 anaweka 1,500 Mama akashtuka ikabidi nimwambie ukweli nilimpenda Anitha nilikua napenda hadi magari ya Baba yake
Kuna jamaa yeye alipenda mpaka mtaa anaoishi na kila kitu, yele mapenzi yaachwe kama yalivyo.
 
Kwa mara ya kwanza Nimepata mtu aliyetajwa humu naemfahamu, huyo nkundwe Ni mnyaki madam kasie, na amesharudi bongo ana mke wa kihaya na watoto wawili?????

Hapana ni mchaga, huyo unayemsema wewe sie huyu niliyesoma nae lasaba B.
 
Kasinde...

Umeandika mistari fulani ambayo natamani kila mtu angelielewa

Sukari shuga, nimekumisi utamu wa warembo...

Jobo imekuacha salama?

Kuna muda Mungu hututumia kama chombo kupitisha jumbe zake kwa waja wake, bila kuangalia udhaifu wetu.

Imeandikwa, kila mwenye sikio na asikie...
Bwana ayaambia mataifa.

Sikuoni sikuhizi kwa muuza matunda.... hata parking sioni alama za matairi yako....

Umeaniachia harufu ya perfume yako tuu kila nikipita naisiki ...😊

Najua utatabasamu, ndo zawadi yangu usiku huu kabla hujalala.
Tabasamu jema shuga sukari.
 
Back
Top Bottom