Unamkumbuka Crush wako wa utotoni? That was real and only unconditional love you will ever experience

haszu

JF-Expert Member
Oct 10, 2017
837
1,550
Asikwambie mtu, yule crush wa utotoni hasa mara nyingi inakua shule ya msingi ni mapenzi ambayo yanavuruga sana hasa ukizingatia mara nyingi mtu mabae unampenda anakua hana ata habari au aanajua unampenda ila hana habari na wewe yuko busy na yeye na crush wake.

Nakumbuka nilipokua darasa wa tano ndo nilikua na crush huyo then kwao alikua kuna duka, bas kama siku sijaenda shule na sijamuina ni lazima nitoke nikamuone hata kama sikua na nia ya kununua kitu, bahati mabaya ilikua ni kijijini kwao hadi ufike unapita kwenye mapoli ila ilikua niko radhi, nakumbuka kuna siku nyingine nakwenda dukani usiku ili nimuone lakini nikitifika unakuta hayuko dukani unakuta mama yake au ndugu zake wengine, ila hata nikisia sauti yake tu huko ndani basi nakua na furaha.

Sikuwahi kumueleza kua nampenda mana nilikosa lakusema nilipokua karibu yake, now ameolewa na hatuna mawasiliano ila mpaka sasa sijawai kuona ile hali tena.

Hakika yale yalikua true unconditional love.
 
Secondary's Crush Sophia Mungu anakuona.
Alijua kabisa mimi ni domo zege ila akawa anajifanya haoni richa ya kumwandikia sana noticies za Biology na michoro kama yote. Nimeandika sana vinemo katikati ya daftari lake la Bios ila anauchuna tu. Nilimpenda sana nikapenda mwandiko wake nikapenda hadi mtaa aliokua anaishi. Kuna wakati nilikua Natamani sana niisukune nyumba yetu hadi mtaani kwao niwe namuona....Nilimchukia baba kwakutokununua kiwanja mtaani kwa Sofia😆

2019 alinitafuta baada ya miaka mingi kupotezana ila sikua nampenda hata robo .
Mkuu yale mapenzi ni mapenzi ya kipekee sana, bahati mbaya wengi wa macrush wale huwa ni ngumu kua ano
 
Secondary's Crush Sophia Mungu anakuona.
Alijua kabisa mimi ni domo zege ila akawa anajifanya haoni richa ya kumwandikia sana noticies za Biology na michoro kama yote. Nimeandika sana vinemo katikati ya daftari lake la Bios ila anauchuna tu. Nilimpenda sana nikapenda mwandiko wake nikapenda hadi mtaa aliokua anaishi. Kuna wakati nilikua Natamani sana niisukune nyumba yetu hadi mtaani kwao niwe namuona....Nilimchukia baba kwakutokununua kiwanja mtaani kwa Sofia

2019 alinitafuta baada ya miaka mingi kupotezana ila sikua nampenda hata robo .
Wacha we!!!
 
Back
Top Bottom