Unamiliki silaha ili iweje?

Unamiliki silaha ili iweje?

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
360,921
Reaction score
831,350
3f51220ba9b2d06ad7ab32a687ff449d.jpg
916f4135e6f9b38818f3ce8551195bbb.jpg
Kuna jibu moja rahisi sana kwenye hili swali nalo ni kwa ajili ya ulinzi binafsi (pengine na familia)...lakini si kweli hata kidogo! Silaha unayo miliki ni kifo binafsi na si ulinzi binafsi , haina tija kwako haikusaidii kwa asilimia unazofikiri inakupa kujiamini kusiko halisi

Kama wewe ni mwamini wa Mungu mmoja unayeamini uwezo na ulinzi wako kwenye maisha yako kubeba silaha ni kujichanganya kiimani kwamba sasa unaamini katika ulinzi wa Mungu au silaha?

Silaha haina matokeo mema silaha chake ni kujeruhi kuua na kuangamiza, ni sahihi Kabisa kwamba tunapaswa kujihami tunapaswa kujilinda lakini kamwe si kwa mtindo huo wa kubeba silaha nzito nzito , kwani umekuwa askari wewe? Kwani ni mwanajeshi wewe? Your mind is the most lethal weapon and your faith to the Almighty creator

Silaha ni kwa ajili ya wasiojiamini silaha ni kwa ajili ya wasio waamini, silaha ni kwa ajili ya wenye rohombaya dhulmati na wanaoogopa kifo! Silaha ni kwa ajili ya maadui...kama unajiamini kama unaamini katika ulinzi wa Mungu kama huna roho mbaya sio dhulmati na huna maadui huna haja ya kubeba silaha

Wengi wamekufa wakiacha silaha zao bila kuzitumia hata siku moja...silaha ni biashara silaha ni uchumi wa watu ili wao waweze kuishi inabidi wauze silaha? Na ili wauze vizuri inabidi wakuandae kisaikolojia na wakuandalie mazingira ya woga na kutojiamini ili tu umiliki silaha ...ni aina fulani ya kucheza na akili za watu

Naamini kati yetu tutakaosoma hapa tuna berreta zetu kwenye makabati full loaded! Lakini mbona umeendelea kuugua? Mbona kuna mazingira mengi tu umeepushiwa kifo bila ya msaada wa hilo lichuma lako ulilolinunua kwa bei ghali sana?

Mrudie Mola wako ukatubu na kuungama, kwa kutokuwa na imani thabiti juu ya ulinzi wake...! Maisha yako na mustakabali wako viko mikononi mwake na sio kwenye bunduki lako , ni yeye ajuaye kutoka kwako na kuingia wako sio bastola iliyoko kabatini chuma kisichosema

Eti hata fulani naye a nazo mbili? za nini?
Mungu wetu tunayemwamini ndio kila kitu kwenye maisha yetu
 
Uwe na silaha utakufa, usipokua nayo hali kadhalika utakufa. Cha msingi, utaacha legacy gani utakapokufa?
Na kumbuka kinachokufa ni mwili sio roho kwahiyo pamoja na ufundi mwingi mno unaotumika kutengeneza silaha ili iwe more lethal ni kwa ajili tu ya kuangamiza mwili uozao
 
Hivi ule uhakiki wa silaha kwa wakazi wa Dar uliishia wapi maana nilimuona mkuu wa Kaya peke yake akiwa anahakikiwa au movie ilikuwa inaendelea.
 
Bro Mshana nadhani roho mtakatifu amekushukia usiku wa Leo. Naona full ulokole Leo, hongera mkuu!!

Kwasisi wawindaji tunakua nazo tena mbili mbili mkuu, SMG kwa buti ya gari na Berreta kiunoni!! Kwetu haziepukiki japokua twamwamini sana Mungu.
 
Hata ombaomba dar wamerejea zaidi ya waliokuwepo awali kabla ya msako wa Makonda mkuu.

Ukifanya jambo lolote bila strategies obvious utafeli tu.
Hivi ule uhakiki wa silaha kwa wakazi wa Dar uliishia wapi maana nilimuona mkuu wa Kaya peke yake akiwa anahakikiwa au movie ilikuwa inaendelea.
 
Kwa anaeamini uwepo wa Mungu ni kweli kwamba kumtegemea Mungu ni jambo muhimu sana. Binadamu tuna matatizo mengi sana tunayopambana nayo katika maisha yetu. Kuna maradhi, maadui wetu wanaopatikana kutokana na sababu mbalimbali n.k. Wakati tunapopatwa na maradhi hatukai na kusema Mungu atatusaidia bila kwenda hospitali kupata matibabu (dawa).Vilevile katika kukabiliana na maadui hatupaswi kukaa tu na kusema Mungu yupo atatulinda bila kuchukua hatua stahiki. Ndiyo maana tunajenga nyumba, tunaweka milango na mageti na vifaa vingine vinavyotusaidia kwenye masuala ya usalama kama security lights, CCTV cameras n.k. Na hivi kwa hakika vimesaidia au kuokoa wengi. Kitu muhimu kwa anaeamini uwepo wa Mungu ni kujua kuwa pamoja na hayo yote hapo juu lakini hayawezi kufanikiwa bila nguvu ya Mungu.

Nitoe mfano mmoja kutoka kwenye biblia. Kwa wasomaji wa biblia mnaelewa kisa cha Daudi (mwisraeli) aliyemuua mfilisti Goliathi kwa kutumia kombeo (sling) na mawe. Huyu Daudi alikwenda na kombeo na mawe ili kupambana na mfilisiti Goliathi ambaye alikuwa ni jitu kubwa na lenye nguvu sana lakini Daudi akiwa na silaha hiyo na mawe yake mfukoni alimwomba Mungu wake na kisha akaingia vitani na akaweza kumshinda adui yake Goliathi. Yaani Mungu aliweza kubariki silaha (kombeo na mawe) aliyokuwa nayo Daudi.

Ukiangalia huo mfano utaona kwamba kuwa na silaha kama bunduki (kombeo) na risasi ( mawe) siyo jambo baya na haimaanishi kuwa umiliki wake unaashiria kutomtegemea Mungu. Kitu muhimu ni kwamba umiliki wa hizo silaha uwe ni kwa kufuata sheria, silaha zitumike kwa malengo halali (kujilinda) na pia umiliki wa silaha usitufanye kuwa na kiburi na kudhani kuwa kwa vile tuna bunduki hizo basi Mungu hana nafasi tena juu ya maisha yetu na hizo silaha zetu. Hayo ndiyo mawazo yangu.
 
Umenena vema kiongozi!!
Kwa anaeamini uwepo wa Mungu ni kweli kwamba kumtegemea Mungu ni jambo muhimu sana. Binadamu tuna matatizo mengi sana tunayopambana nayo katika maisha yetu. Kuna maradhi, maadui wetu wanaopatikana kutokana na sababu mbalimbali n.k. Wakati tunapopatwa na maradhi hatukai na kusema Mungu atatusaidia bila kwenda hospitali kupata matibabu (dawa).Vilevile katika kukabiliana na maadui hatupaswi kukaa tu na kusema Mungu yupo atatulinda bila kuchukua hatua stahiki. Ndiyo maana tunajenga nyumba, tunaweka milango na mageti na vifaa vingine vinavyotusaidia kwenye masuala ya usalama kama security lights, CCTV cameras n.k. Na hivi kwa hakika vimesaidia au kuokoa wengi. Kitu muhimu kwa anaeamini uwepo wa Mungu ni kujua kuwa pamoja na hayo yote hapo juu lakini hayawezi kufanikiwa bila nguvu ya Mungu.

Nitoe mfano mmoja kutoka kwenye biblia. Kwa wasomaji wa biblia mnaelewa kisa cha Daudi (mwisraeli) aliyemuua mfilisti Goliathi kwa kutumia kombeo (sling) na mawe. Huyu Daudi alikwenda na kombeo na mawe ili kupambana na mfilisiti Goliathi ambaye alikuwa ni jitu kubwa na lenye nguvu sana lakini Daudi akiwa na silaha hiyo na mawe yake mfukoni alimwomba Mungu wake na kisha akaingia vitani na akaweza kumshinda adui yake Goliathi. Yaani Mungu aliweza kubariki silaha (kombeo na mawe) aliyokuwa nayo Daudi.

Ukiangalia huo mfano utaona kwamba kuwa na silaha kama bunduki (kombeo) na risasi ( mawe) siyo jambo baya na haimaanishi kuwa umiliki wake unaashiria kutomtegemea Mungu. Kitu muhimu ni kwamba umiliki wa hizo silaha uwe ni kwa kufuata sheria, silaha zitumike kwa malengo halali (kujilinda) na pia umiliki wa silaha usitufanye kuwa na kiburi na kudhani kuwa kwa vile tuna bunduki hizo basi Mungu hana nafasi tena juu ya maisha yetu na hizo silaha zetu. Hayo ndiyo mawazo yangu.
 
Bro Mshana nadhani roho mtakatifu amekushukia usiku wa Leo. Naona full ulokole Leo, hongera mkuu!!

Kwasisi wawindaji tunakua nazo tena mbili mbili mkuu, SMG kwa buti ya gari na Berreta kiunoni!! Kwetu haziepukiki japokua twamwamini sana Mungu.
Leo ni kiimani zaidi na kukumbushana yaliyo mema
 
Back
Top Bottom