Unamiliki silaha ili iweje?

Unamiliki silaha ili iweje?

Mkuu ukiwa na silaha mkafanyiwa timing, labda bar au popote kwenye kusanyiko, usije hata siku moja ukathubutu kutoa silaha hata kama unayo, the grave mistake tht even a trained commando would thnk twice, sababu hao majambazi wameweka kwenye plan yao kuwa upo uwezekano kukawepo na watu wenye silaha, bora ingekuwa raia tu mwenye silaha, lakin wanaogopa zaid kuwa anaweza kuwepo askar au polis au mjeda, au hata usalama na akawa pia na silaha so wanakuwa wanawa monitor wote.
Niliona pale mawela sinza jamaa walivamia, mlinz akijidai eti hawamuon akaanza kupiga simu, ww, hee jamaa alimtungua kutokea mbali kishenzi, wale jamaa nadhan huwa ni askari.
Me naongelea watu wachache wameingia sehem wana mapanga, au vibaka wale wa mtaani wanakuja na silaha ndogo ndogo.
Ni kweli mkuu hapo Ni mambo ya timing sasa
 
Hata wale waisrael walikuwa wanamiliki mapanga shaa, ingawa walikuwa taifa la sir god. Sembuse sie wabongo. Nikiwa na mpunga AK47 inanihusu na mpunga ujimwagija zaidi hata ya wa siria ntatafuta
 
Huwezi kujilinda mwenyewe kwa silaha yako mkuu...labda umlinde mtu mwingine kwa silaha yako.ni wengi wenye silaha wanavamiwa na kuuawa bila kutumia silaha zao.
Pengine sijakupata vizuri unaposema kwamba huwezi kujilinda mwenyewe kwa silaha yako. Kule kuvamiwa na kuuawa kwa baadhi ya watu kwa kushindwa kutumia silaha zao ndiyo kunakokufanya uhitimishe kwamba hauwezi kujilinda mwenyewe kwa silaha yako? Je haujawahi kushuhudia au kusikia kuwa kuna watu wameokoa maisha yao (kujilinda) kwa kutumia silaha hizo hizo wanazomiliki?
 
Ila kuna point wengi hamkuizingatia kuhusu powerful mind..hebu tujaribu kuwa na mitazamo yote

umesema kweli mshana ukiwa unajua utaibiwa au unawaza sana utahangaika sana na hii dunia. mi mwaka jana nililala kwa zaidi ya mwezi kwenye nyumba siyokuwa na geti tena nairobi nikaambiwa nitavamiwa na majambazi nikawaambia watu sitaingiliwa na yeyote na ninalala na amani kabisa kwa sababu najua kuna mlinzimkuu ananilinda. chukulia mfano wa mfanyabiasha maarufu aliyeu wawa kenya mwezi huu Jacob Juma wkt anauwawa alijuwa na gun na alishindwa kujilinda. ukiwa na kitu ndani naamini kuna roho itakusukuna ukitumie na ukute uko na malaana ya ukoo au yako mwenyewe utashangaa murder case ndio hiyo.
 
Kuna hii habari iliripotiwa na vyombo vya habari 2012 pengine itatusaidia kutafakari:

Tarehe 6 Desemba 2012, bibi wa miaka 61 aitwae Mwajuma Said Marwa Masaigana alivamiwa nyumbani kwake usiku wa kati ya saa 5 na saa 6 Bagamoyo Pwani Tanzania, majambazi walikua nane wakiwa na silaha kama bunduki na mapanga, na yeye alikua na bastola ambayo ilimsaidia kupambana nao kwa risasi kwa dakika kama 20 mpaka alipofanikiwa kumuua mmoja wao kwa risasi kupitia mlango ambao walikua wamekaribia kuuvunja.
 
mshana jr katika ubora wake. Maneno yako yamechoma kama ya mhubiri mwenye upako. Nakubaliana na wewe kabisa. Ulinzi pekee na wa uhakika ni wa Mungu peke yake. Neno la Mungu linasema;
'Bwana asipoulinda mji yeye alindae akesha bure'
 
JIBU:- Ili niku Tandike ukija ki FALA FALA kwenye Anga Zangu-
 
Tushukuru Mungu ametuweka kama jamii yenye imani na amani ingawa usalama bado ni mdogo kwa kuwa serikali imeshindwa kutimiza kifungu cha katiba cha kulinda raia wake kwa kutumia vyombo vya usalama hasa polisi.

Katika nchi zingine kuwa na silaha haiepukiki kama Marekani, South Africa nk, ni kwa vile uhalifu wa kutumia silaha uko katika kiwango cha juu sana kiasi kwamba raia wema wameamua nao wabebe silaha pia kama njia za kukabiliana na wahalifu. Nakumbuka hata Obama ameshindwa kupitisha bunge la Congeress sheria mpya ya umiliki wa silaha. Serikali ya South Africa walianza kuzikusanya silaha kwa kutoa zawadi kama baiskeli na pikipiki lakini raia waafrika akagundua wazungu hawazirudishi silaha zao na wao wakagoma kuzitoa.

Kwa hiyo kuwa na silaha sio vibaya, hata hivyo wanaozimiliki hawajawahi kusema kuwa wana uhakika wa usalama wao kwa 100% bali ni namna ya kujijengea confidence kwa wale wanaoishi kando ya miji na ndio maana leo hii Kariakoo wanaishi Wahindi kama njia ya kujilinda ingawa uwezo wa kujenga nyumba za kuishi wanao.

Sijajua kama serikali hii itaweza kurudisha hali ya usalama iliyokuwepo enzi hizo baada ya uhuru. Nakumbuka ulikuwa unawakuta watanganyika wenye asili ya kihindi na kiarabu wanaishi Pugu Kajiungeni, Mkuranga, Bagamoyo nk huku wakifanya biashara zao bila wasiwasi wa kuvamiwa na vibaka na majambazi.

Kuwa na silaha ni kama detarrent tu ya kuvamiwa na sio uhakika wa usalama wa mmiliki. Tuiombe serikali yetu ijenge mazingira salama kwa raia ikiwa ni.pamoja na kuhakikisha kila mtanzania mwenye umri unaozidi miaka 18 awe na kitambulisho cha uhakika kinyume na hapo uhalifu utaendelea kutuangamiza.
 
Dah...kwenye hii dunia ya fujo...yaani kabla sijalala lazima nikumbatie tochi na rungu langu
 
Elimu ya matumizi ya silaha yatolewe na vyeti vitolewe-
Ukifeli hupewi hata kama una hela kiasi gani-
 
Back
Top Bottom