Kuna jibu moja rahisi sana kwenye hili swali nalo ni kwa ajili ya ulinzi binafsi (pengine na familia)...lakini si kweli hata kidogo! Silaha unayo miliki ni kifo binafsi na si ulinzi binafsi , haina tija kwako haikusaidii kwa asilimia unazofikiri inakupa kujiamini kusiko halisi
Kama wewe ni mwamini wa Mungu mmoja unayeamini uwezo na ulinzi wako kwenye maisha yako kubeba silaha ni kujichanganya kiimani kwamba sasa unaamini katika ulinzi wa Mungu au silaha?
Silaha haina matokeo mema silaha chake ni kujeruhi kuua na kuangamiza, ni sahihi Kabisa kwamba tunapaswa kujihami tunapaswa kujilinda lakini kamwe si kwa mtindo huo wa kubeba silaha nzito nzito , kwani umekuwa askari wewe? Kwani ni mwanajeshi wewe? Your mind is the most lethal weapon and your faith to the Almighty creator
Silaha ni kwa ajili ya wasiojiamini silaha ni kwa ajili ya wasio waamini, silaha ni kwa ajili ya wenye rohombaya dhulmati na wanaoogopa kifo! Silaha ni kwa ajili ya maadui...kama unajiamini kama unaamini katika ulinzi wa Mungu kama huna roho mbaya sio dhulmati na huna maadui huna haja ya kubeba silaha
Wengi wamekufa wakiacha silaha zao bila kuzitumia hata siku moja...silaha ni biashara silaha ni uchumi wa watu ili wao waweze kuishi inabidi wauze silaha? Na ili wauze vizuri inabidi wakuandae kisaikolojia na wakuandalie mazingira ya woga na kutojiamini ili tu umiliki silaha ...ni aina fulani ya kucheza na akili za watu
Naamini kati yetu tutakaosoma hapa tuna berreta zetu kwenye makabati full loaded! Lakini mbona umeendelea kuugua? Mbona kuna mazingira mengi tu umeepushiwa kifo bila ya msaada wa hilo lichuma lako ulilolinunua kwa bei ghali sana?
Mrudie Mola wako ukatubu na kuungama, kwa kutokuwa na imani thabiti juu ya ulinzi wake...! Maisha yako na mustakabali wako viko mikononi mwake na sio kwenye bunduki lako , ni yeye ajuaye kutoka kwako na kuingia wako sio bastola iliyoko kabatini chuma kisichosema

Eti hata fulani naye a nazo mbili?

za nini?

Mungu wetu tunayemwamini ndio kila kitu kwenye maisha yetu