Haya ndio madhara ya kukaa na silaha ndani
1.Jamaa mmoja hapa Dar aliwakurupusha majambazi waliotaka kuiba kwa jirani yake kwa kupiga risasi tatu juu
Siku iliyofuata usiku wa saa mbili jamaa walimvamia jamaa akiwa kakaa sebuleni na kumtoboa macho mbele ya familia yake
2. Jamaa mwingine yeye alipishana lugha na mkewe usiku wakiwa wamelala jamaa akatishia kumpiga mkewe risasi, ni katika purukushani za kupokonyana silaha jamaa alimpiga ya tumboni mkewe na kufa muda mfupi baadae, mpaka leo yupo segerea
3. Hii niliishuhudia live tulienda kumtembelea jamaa yetu siku moja jumapili mchana , tukiwa tumekaa sebuleni akatoka chumbani mwanae wa kiume wa umri wa miaka 5 hivi kaelekeza bastola kwa baba yake
Mwanzoni tulidhani ni toy lakini kumwangalia jamaa alivyotoa macho ya woga tukajua kuna hatari
Mtoto akawa anamwambia babaake Dad hands up wote tulikuwa kimya
Aliyeokoa jahazi ni mdada wa kazi aliyekuja kwa nyuma na kuikamata silaha na kuelekezea juu ambapo ili fire

Kumbe jamaa analala na ile silaha na kuiweka tayari kwa kupiga ila asubuhi huirudisha kabatini lakini siku hiyo akapitiwa, siku iliyofuata jumatatu jamaa aliipeleka police ikauzwe
Tunapaswa kujihami tunapaswa kujilinda lakini ulinzi wetu Usiwe chanzo cha maafa na matatizo
Tunajenga nyumba na kuziwekea ulinzi mkali mpaka zinageuka gereza la kifo badala ya nyumba
Tunakuwa na silaha za hatari ndani ya nyumba kwa ajili ya kujilinda lakini ni silaha hizo hizo hutuletea maafa wenyewe
Tunakuwa na mazindiko mbalimbali na mahirizi makubwa yanayotufanya tuingie kwenye maagano yenye madhara makubwa halafu Tunakufa na malaria
Bado ulinzi wa Kimungu ndio ulinzi bora kuliko mwingine wowote ule..vyovyote iwavyo usisahau Mungu ndo mweza wa yote na vyote