Unamfahamu mjusi kafiri?

Mtoboasiri

JF-Expert Member
Aug 6, 2009
5,101
1,946
Mjusi Kafiri ana tabia ya kukaa kwenye jiwe na/au kupigapiga kichwa chake juu na chini. Kwa kawaida ni muoga mno kwa binadamu. Ila ukimfukuza hadi akachoka uoga wake huisha na kugeuka na kuanza kukufuza wewe mwenyewe.

CCM wamewafikisha Watanzania mahali pa kuacha kuwaogopa tena watawala. Siku isiyokuwa na jina YATATOKEA kwingine yanayotokea leo Arusha, Mbeya, Mwanza, Tarime na kwingineko. Kina fulani mnaojijua mjiandae!??
 
Aaaah... Mkuu yaani unatufananisha tutakaoandamana na mjuusi kafiri aliyefukuzwa, akachoka na amegeuka kumfukuza aliyekuwa anamfukuza... lol. Mi simo
 
Mjusi Kafiri ana tabia ya kukaa kwenye jiwe na/au kupigapiga kichwa chake juu na chini. Kwa kawaida ni muoga mno kwa binadamu. Ila ukimfukuza hadi akachoka uoga wake huisha na kugeuka na kuanza kukufuza wewe mwenyewe.

CCM wamewafikisha Watanzania mahali pa kuacha kuwaogopa tena watawala. Siku isiyokuwa na jina YATATOKEA

Hahahahahaha lol! umenikumbusha mbali sana kuhusu mjusi kafiri, niliuliza maswali mengi sana kuhusu mjusi kafiri lakini sikupata jibu lililoniridhisha. Ni kweli kwamba idadi ya Watanzania ambao woga dhidi ya vyombo vya dola umeanza kupotea na pia kuna dalili kwamba hata baadhi ya waliomo ndani ya vyombo vya dola wameanza kuwa upande wa Watanzania walio wengi. Kama hawa waliopo madarakani hawatasoma alama za nyakati na kubadilisha mwenendo wao haraka sana basi cha moto watakiona mara tu wenye nchi watakapoamua kuchukua nchi yao. Mdharau mwiba....
 
Mjusi kafiri ni mtu kuwadi,mnafki,mshambenga,fisadi,mshenzi,nk ndio mana wakaita kafiri manayake haramu, sasa kwa maisha halisi ni magamba ndio wajusi kafiri wanajua wamechemka lakini wanabisha ndio wajusi kafiri.
 
Aaaah... Mkuu yaani unatufananisha tutakaoandamana na mjuusi kafiri aliyefukuzwa, akachoka na amegeuka kumfukuza aliyekuwa anamfukuza... lol. Mi simo

Kwa kauli yako hii ina maana uoga wa kinyonge umeshaupiga chini!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom