unalionaje wazo la adhabu mbadala?

TANZANNIA

JF-Expert Member
Sep 29, 2015
1,047
384
kuna wazo limejitokeza siku mbili hizi linalotaka hukumu ya kifungo kwa makosa madogo yasiyo na athari kubwa kwa jamii mfano kutukanana,iondolewe na badala yake mkosaji apewe kazi ya kuitumikia jamii kwa ujuzi alionao, uzalishaji mali au usafi masokoni,mahospitalini nk, unakubaliana na wazo hilo?
 
Ni wazo zuri Ila mimi nitaongeza kidogo Serikali Kuu au Wilaya zingekuwa na mashamba makubwa ya mazao ya chakula na biashara pia ili hao watuhumiwa wapelekwe sehemu Kama hizo kulima. Na kusafisha mabarabara ya katikati na nje ya Mji.

Halafu hizo jela ziwe chini ya uangalizi wa JKT ili kusimamia nidhamu na kuongeza ufanisi. Wakati huo huo wakitayarishwa kwa mafunzo ya Uraia ili wakirudi kwenye jamii wawe Raia wema na mchango katika jamii kwa ujumla.
 
hilo nalo neno
 
Ni wazo zuri sana
 
Back
Top Bottom