Unakuta mtu anatembea barabarani mda wote anabofya simu

The Sunk Cost Fallacy 2

JF-Expert Member
Nov 8, 2022
7,382
8,437
Majaribu kuniuliza sipati picha kwamba ni ulimbukeni,utoto,kutojiamini au ujinga?

Haiwezekani mtu mda wote Yuko busy na simu kama kwamba ni sehemu ya kiungo cha mwili wake.Unaongea na mtu unabonyeza simu mda wote.

Watu mpaka wanagongana au wanataka kugongwa kisa simu.Kwa Sasa imefika mahala unakuta dereva anaendesha boda au gari huku anachati,hii ni dangerous habit na ulevi wa kipumbavu.

Hii tabia imeota mizizi hususani Kwa Vijana na ndio maana Huduma za jamii zinazorota Kwa simu kuwa sehemu ya uzembe.Nakumbuka Waziri Simbachawene aliwahi pendekezwa Watumishi wa Umma wasiingie kazini na simu Hadi baada ya mda wa kazi.

Tunakoelekea tutakuwa na kizazi Cha mazombie.
 
Hiyo ni nguvu ya technolojia na hakuna wa kuizuia especial katika ulimwengu wa tatu ambako wengi wa raia wake bado ni washamba na limbukeni wa mambo ya tekinolojia hivyo contents zake zinawaingiza kwenye uraibu.
 
Huenda mkuu umeyaona yaliyo tokea Hivi karibuni huku.

Wiki hii jumanne barabara ya kutoka kahama to kakola Kijiji Cha bugarama maeneo ya mabingwa coster company ya......imegonga mtu maeneo hayo alikuwa anaendesha bodaboda kijana mdogo miaka20-25. Inavyosemakana derava wa gari Hilo alikuwa anachati! Na kusababisha kugonga yule mwendesha pikpiki.
Inauma sana
 
Wengine tukiwa barabarani huwa tunatembea macho yanaangaza kulia, Kushoto na Mbele Ili tuone wapi Kuna ujenzi au kazi ngumu tujitose kuomba kazi mambo ya simu ni labda nikiwa nimekaa nimetulia maskani sina lolote lakufanya.
Wengine mkisha pata hizo kazi,naona mnapiga kazi na simu zenu mkononi huku mna chart hadi mnaharibu kazi za watu!! Smart zina uteja mkubwa!!
 
Back
Top Bottom