Nataka nichukue simu ya mkopo wa kishua naomba ABC za simu hizi

Anikajema

JF-Expert Member
Mar 2, 2014
605
530
Habari wakuu.
Mimi najiona siko sawa akilini mwangu, maana nimejiona Niko tofauti sana tangu nianze maisha yakukosa mpaka pesa ya kula.... Nikiri Tu hapa katikati nimepitia wakati mgumu baada ya kupoteza pesa nyingi kweny biashara yangu mpya ambayo nimeianza na mwisho wa siku nikawa sina hata mia na biashara ikafeli, nikajikuta Nina madeni kila sehemu, hadi Mwenye nyumba akaniletea shida nikauza baadhi ya vitu nikapata nauli yakwenda Nyumbani na nia yangu nilienda Nyumbani kuipeleka familia yangu kwa mama maana naona kama hadi watoto wangekosa hela ya kula na mahitaji mengine , nilipo enda Nyumbani nikakaa huko week mbili nikarudi town sasa toka nirudi naona kabisa siko saw kiakili kwasababu hizi hapa...
...nimekuwa mnyonge hadi najitenga na watu
...kuna mda sisikii vitu vizuri,
Mtaa niliopo nimekuwa kama mgeni naona watu wanaongea kiluga sana na huu mtaa sikuwa mgeni kivile .
Naona kama Niko nyuma sana kujua vinavyoendelea duniani, ingawa simu ninayo.
...sina amani ,sina hela sina rafiki
...nimekosa kujiamini kabisa alafu nimekuwa mgumu kabisa kuelewa na nimekuwa msahaulifu mno, yaani kuna vitu vingine naweza kufanya lisaa limoja nyuma lakini naweza kukuambia nilifanya Jana.
....yaani sina swaga I mean sina point yeyote ya kuongea na watu.
....nimekuwa MTU wa kujistukistukia tu bila sababu.
....sipendi kuongea na simu kabisa na mitandao imekaa kushoto kwangu.
Kikubwa unaweza niongelesha hichi nikakujibu kingine kabisa nakurupuka hovyo na nikikaa mda wote nashika tama hata kama hakuna nachowaza, geto sipataki hata kwenda kuna siku nimelala na mlinzi kwenye kiofisi hichi nachofanyia kazi nimekuwa sijijali kabisa..... Sasa hapa naona kama vile nipo dunia nyingine au kama vile nimeamka usingizini nikakuta watu wameshaondoka tuliopanga kwenda nao safari.

Kiufupi sijielewi wakuu sasa sijui napaswa kusaidiwaje hapa.

Samahanini Mimi sio mwandishi mzuri Sana ila nafikir nimefikisha kile kinanitesa.
 
Hizo ni hallucinations tu... mbona hapa umeandika vizuri as if huna tatizo

Ushauri muone mtaalam wa saikolojia, padre,au waliokuzidi umri na wenye busara wakupe canceling.
 
Baba yangu mzee Mohammad Jabir, anamsemo wake mmoja iv kwanba 'Angalia, tazama, chungulia, hakikisha kisha Amua...
Huu msemo alikua anautumia hasa akiwa yupo maji... mwanzoni sikua namuelewa ila nilipo jitambua nkagundua una maana kubwa sana...
anyway kaka tuliza akil...
changamoto ktk maisha sio adhabu... ila ni sehem muhim ktk ukuaji. bila changamoto huwez kukua kaka...
EM FANYA KU ANGALIA, UTAZAME, UCHUNGULIE, UHAKIKISHE KISHA UAMUE KWENDA HATUA NYINGINE KUBWA ZAIDI... kwa kukubali kwamba kilicho potea kimepotea... ila kiwe somo kwa yale makubwa unayotaka kuyajenga kwa somo la kupoteza...
 
Nakushukuru kaka
 
Back
Top Bottom