Monyiaichi
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 1,826
- 508
Stori zalongi sana duh! tuliokuwa tunasoma shule za mbali unapita msituni unafika Shule roho uko mikononi, nilikua nakimbia kutoka nyumbani mpaka Shule
Umenikumbusha Forodhani Primary.
Enzi hzo tuko drs la 3.
Kuna gari flani la Red Cross liliingia pale shule kwa minajiri ya kugawa First Aid Kit kwa mwl mkuu Bw. Saiwad.
Sasa pata picha kilichotokea...afu sasa yule baba mhindi alikuwa amevaa gloves na nguo nyeupe, akaja moja kwa moja kule juu darasani.
Kama si busara za masista siku hiyo...sijui kama mngemjua Madame B.
Tulipagawa mpaka wengine tulizima chali.
Khaa@ madame B kumbe ni wa forodhani primary...unamkumbuka mwalimu chuma...mwalongo..mwalimu asenga...we ni la saba la mwaka gani
Umesoma mlimani nini?maana dah msitu ulikuwa mkubwa..lazima tukimbizwe.
Yani ilikuwa tabu kweli..tulikuwa kama tunakatiza kipori lazima tuwe wengi pale sheli..maana dah wale wajinga walikuwa wanatuvizia kweli..unakumbuka mpaka mama mmoja wa kihaya alianzisha daladala konda yeye ndio kama unaogopa kukatisha kipori anatubeba..ukichelewa inakula kwako.
Asanteni wote mliochangia huu uzi. Nimecheka sana nikikumbuka Mumiani. Nakumbuka siku moja na wadogo zangu twatoka mafundisho ya kumunio mitaa ya Ukonga, mzee mmoja alikuwa anaitwa BOGI (walikuwa wanasema ni mumiani - RIP ) akatuuliza njia ya kwenda FFU Ukonga iko wapi huku anatusogelea.
Wadogo zangu wakawa wanamuelekeza, nilistukia nimeanza Marathon, kutahamaki wadogo zangu wakanipita ktk hizo mbio. Tulikutana nyumbani umbali wa kama 2kms nakuanza kusimuliana.
Nimeamini we born intown....it was a niiice school....full kipupwe cha bahari ya hindi...kwenye miaka hapo tupaache kwakweliiChuma, Mwalongo, Asenga, Mushi, Kimathi...wote hao walimu wangu.
Sasa huko kwenye miaka ndio hatarishi mazee.
Ila mie mkubwa.
Wewe ni wa mwaka gani kwani?
Dah niko hoi kwa kucheka..unanikumbusha mbali watu walivyokuwa wanakimbizwa mabwawa saba..haaa beach kidimbwi lol jamani tumetoka mbali.........hahahaaa,mlimani primary school!!daahhhh,nyonya damu zilizingua sana mixer na komando yosso kule vichakani mabwawa saba na beach kidimbwi palikua hapapitiki enzi zile.
....ahhh,kulaaaleki!Mrs Rwiza yule anakaa sinza A,alikua anafundisha UDSM na mzee Rwiza ni mwalimu UDSM(prof).
Umenikumbusha Forodhani Primary.
Enzi hzo tuko drs la 3.
Kuna gari flani la Red Cross liliingia pale shule kwa minajiri ya kugawa First Aid Kit kwa mwl mkuu Bw. Saiwad.
Sasa pata picha kilichotokea...afu sasa yule baba mhindi alikuwa amevaa gloves na nguo nyeupe, akaja moja kwa moja kule juu darasani.
Kama si busara za masista siku hiyo...sijui kama mngemjua Madame B.
Tulipagawa mpaka wengine tulizima chali.
Nimeamini we born intown....it was a niiice school....full kipupwe cha bahari ya hindi...kwenye miaka hapo tupaache kwakwelii
binafsi nikiwa darasa la kwanza ilitoke huo uvumi. na nlikuwa mdogo class nzima si kubanwa mlangoni.
ila lawama zangu nazielekeza kwa waalimu sikuwahi sikia.walimu wakitwambia kuwa hakuna kitu kama hicho
Dah! hii ni moja ya 'hoax' ambazo zilishika hatamu miaka hiyo tukiwa bado makinda...
Nakumbuka nikiwa Mbeya kuna jina la Msekwa(sio Pius Msekwa) lilikuwa maarufu sana...
Na kipindi kile mji haukuwa umejengwa sana kwani kulikuwa bado na ule uoto wa misitu ya mikaratusi...
Sasa ilikuwa inasemekana huyu bwana ni nyonya damu na anatembelea kibito chekundu na hakitoi mlio...
Suala la kwenda shule asubuhi na mapema au kurudi nyumbani kigiza kikiwa kimeingia ilikuwa tafrani sana...