unakumbuka ulianza kunywa bia wakati una umri gani?

Bondpost

JF-Expert Member
Oct 16, 2011
6,602
9,345
Guys leo nimejikuta nakumbuka siku niliyoonja pombe kwa mara ya kwanza! Ilikuwa standard 2 wakati tunaiba za mzee then tunajazia maji akaja kustukia kitu hakiwi na ladha akatuzingua balaa ila kuanzia kipindi hicho ni ulanzi kwenda mbele enzi za boarding Iringa huko!
 
Mi nakumbuka nilipokuwa darasa la tatu nilitishia kutokwenda shule ningenyimwa gongo! nakumbuka mama angu alinipa toti moja tu nilipochangamka niliwahi shuleni...........................
Bia nilianza kunywa nilipojua mambo ya Bongonyoooooo!!!!!!!
 
Za kienyeji siwezi kumbuka manake tangu nkiwa mtoto mdogo nimekunywa sana.

Bia nilikunywa kwa mara ya kwanza siku nafanya graduation ya form six, nadhani nilikuwa na 20 yrs of age!
 
Bia nilianza kunywa baada ya kuanza kazi, early 20s ila Choya,Kangala na Wanzuki sikumbuki ni lini manaake nyumbani kulikua na mapipa kabisa mi mwenyewe opareta kabla ya kwenda boarding hiyo
 
Mi bado sijaanza kula hiyo kitu na ninaomba Mungu anisaidie nisitumie..
 
Baada tu ya kumaliza std 7! Hiyo ni bia na nilinunua mwenyewe. Za kienyeji sina kumbukumbu!
 
Biya?? Kwangu NOT YET... Labda NDYOFU KONYAGI NA GRANT'S. MSINYWE BIYA KABISA.
 
kuna ile kunywa bia ka mtu mzima unamaliza chupa na kuna ile ya kuonja wakati ukiwa mdogo unaonjeshwa so we unaongelea kuonja au kunywa kumaliza chupa
 
Mi tangu nikiwa tumboni mwa mama yangu alikuwa ananirushia humo ndani.
 
Baada tu ya kumaliza std 7! Hiyo ni bia na nilinunua mwenyewe. Za kienyeji sina kumbukumbu!
Mi biya nlianza kuzigida nikiwa nasare skul. Nlikuwa namsindikiza mzee kwenda kucheza darts (nadhani na kukutana na nyumba ndogo yake) Wakati yuko bize na vishale, mie nagida Pilsner yake tartiiiibuuuu..
 
Mi biya nlianza kuzigida nikiwa nasare skul. Nlikuwa namsindikiza mzee kwenda kucheza darts (nadhani na kukutana na nyumba ndogo yake) Wakati yuko bize na vishale, mie nagida Pilsner yake tartiiiibuuuu..

humu Kuna vioja
 
mimi sikumbuki mara ya kwanza ni lini ila kabla ya kuanza skonga nilikuwa nikipewa nusu glass.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom