Mwenyeminazi
Senior Member
- May 24, 2012
- 194
- 67
Ilikuwa kama utani uliponipigia simu na kuniambia una mpenzi mwingine. Ulijua ni jinsi gani nilikupenda na ukanipa maneno ya kuniumiza ili ujue kuwa nakupenda au lah.
Nilijikaza kisabuni na kukuambia kuwa sikupendi tena. Moyo uliumia na nilidhani kuwa ni utani na kuna siku utaniambia kuwa unanitania kama kawaida. Hukusema na siku zikawa ninaenda huku ukinifuata kila siku kana kwamba hakuna neno lolote ulilosema kwangu. Nilipoenda likizo ulinifuata mkoa na kunibembeleza ila nilikaza kamba kana kwamba sikupendi.
Uko wapi siku hizi?
Mbeya au Tanga kwa Kaka yako?
Bado nakumbuka sauti yako ulipokuwa ukiniambia "" Mbona bado naumia, si uliniambia kuwa nikizoea nitaacha kuumia?
Tulitoka Mbeya 2002 tukaachana DSM 2005.
Nakukumbuka saana. Natamani nikuone nikusaidie kimaisha kama hauko sawa maana nilikuchanganya kwa mapenzi yangu na hukuwaza shule zaidi ya kuniwaza mimi. Ulisumbua kwenu kwa kubadili shule kunifuata. Ulifanya hivyo wakati baba yako alikuwa mgonjwa. (Unakumbuka?) familia ilikutegemea kwa akili za darasani ila nilikuharibia masomo yako kwa mapenzi yangu.
Uko wapi nirekebishe makosa yangu katika maisha yako! Kama uko tayari kusoma kama hukumaliza masomo nitakusomesha kama kumbukumbu ya mapenzi yetu na majuto ya matendo yangu katika kuharibu masomo yako.
Uko Wapi?