Unakumbuka Tulivyoachana?

Mwenyeminazi

Senior Member
May 24, 2012
194
67
Ilikuwa kama utani uliponipigia simu na kuniambia una mpenzi mwingine. Ulijua ni jinsi gani nilikupenda na ukanipa maneno ya kuniumiza ili ujue kuwa nakupenda au lah.

Nilijikaza kisabuni na kukuambia kuwa sikupendi tena. Moyo uliumia na nilidhani kuwa ni utani na kuna siku utaniambia kuwa unanitania kama kawaida. Hukusema na siku zikawa ninaenda huku ukinifuata kila siku kana kwamba hakuna neno lolote ulilosema kwangu. Nilipoenda likizo ulinifuata mkoa na kunibembeleza ila nilikaza kamba kana kwamba sikupendi.

Uko wapi siku hizi?

Mbeya au Tanga kwa Kaka yako?

Bado nakumbuka sauti yako ulipokuwa ukiniambia "" Mbona bado naumia, si uliniambia kuwa nikizoea nitaacha kuumia?

Tulitoka Mbeya 2002 tukaachana DSM 2005.

Nakukumbuka saana. Natamani nikuone nikusaidie kimaisha kama hauko sawa maana nilikuchanganya kwa mapenzi yangu na hukuwaza shule zaidi ya kuniwaza mimi. Ulisumbua kwenu kwa kubadili shule kunifuata. Ulifanya hivyo wakati baba yako alikuwa mgonjwa. (Unakumbuka?) familia ilikutegemea kwa akili za darasani ila nilikuharibia masomo yako kwa mapenzi yangu.

Uko wapi nirekebishe makosa yangu katika maisha yako! Kama uko tayari kusoma kama hukumaliza masomo nitakusomesha kama kumbukumbu ya mapenzi yetu na majuto ya matendo yangu katika kuharibu masomo yako.

Uko Wapi?
 
Tatizo wazazi wetu hawatupi tahadhari tukiwa tunabalehe na kuvunja ungo kuwa kuna kitu kinaitwa mapenzi, mapenzi yanaumiza moyo na yanaweza kukutoa kabisa katika mstari wa maisha.
 
chance-love-quote-regret-text-Favim.com-407056.jpg
 
"In this life you get few chances, and if you are not smart enough to grab those chances by the Balls, you will always wounder how you ended up second rated in this life!!!!!!!!!"

Huu msemo ni bonge ya inspiration kwangu! Kila nitaka kuzubaa nikikumbuka few chances, second rated nakurupukaje kukaza kwenye mishemishe!
 
kazi kwelikweli ntaje basi jina maana hapa najihisi bt am not sure , am rede now kukupa chace urekebishe makosa yako, kweli milima haikutani bainadam hukutana, ckutegemea kama ntakupata tena
 
face your ghost before you move forward ,because the past has always a way of cripping into your future you can run but you can never hide the past will fin d you.
 
"In this life you get few chances, and if you are not smart enough to grab those chances by the Balls, you will always wounder how you ended up second rated in this life!!!!!!!!!"

Huu msemo ni bonge ya inspiration kwangu! Kila nitaka kuzubaa nikikumbuka few chances, second rated nakurupukaje kukaza kwenye mishemishe!
ni kweli kabisa ,sikufanya kosa ,
 
Wameshakutenda
walimwengu mpaka unakumbuka zilipendwa? jitahidi waweza mpata ila
nahisi kama imekula kwako maana sidhani kama alikusubili
 
Wameshakutenda
walimwengu mpaka unakumbuka zilipendwa? jitahidi waweza mpata ila
nahisi kama imekula kwako maana sidhani kama alikusubili

Nimeokoka jamani niko katika toba atii. narudisha pesa zoooote za ushuru!!!!!
 
kazi kwelikweli ntaje basi jina maana hapa najihisi bt am not sure , am rede now kukupa chace urekebishe makosa yako, kweli milima haikutani bainadam hukutana, ckutegemea kama ntakupata tena

Jina lako la kwanza ni refu na linaanza na T na sir name yako inaanza na M
 
Tatizo wazazi wetu hawatupi tahadhari tukiwa tunabalehe na kuvunja ungo kuwa kuna kitu kinaitwa mapenzi, mapenzi yanaumiza moyo na yanaweza kukutoa kabisa katika mstari wa maisha.

Nikweli kabisa kwani huwa tunajifanya tunayajua kumbe hatujui kitu. siku hizi mitindo chungu mbofuuu sijui nani kafundisha haya. sasa mbele giiiiiza totoro
 
Jina lako la kwanza ni refu na linaanza na T na sir name yako inaanza na M

sijui kwanini nimekuwa interested na hii thread
ngoja nikuulize we jina lako linaanza na SH
nahisi kuna mtu anafanana na story yako hasa note hizi
mbeya,baba yake mgonjwa,ana jina refu la T na surname ni M
jus curious tu!
 
Usiniambie baba yake anaumwa hadi leo?
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom