Unakumbuka nini ukiona hii

Unakumbuka nini ukiona hii

Mani H

Senior Member
Joined
Mar 25, 2011
Posts
180
Reaction score
46
Me nakumbuka kipindi cha mama na mwana kilikuwa mchana mara nyingi wakati huo nilikuwa nawait chakula, na mother yuko jikon anapika.
 

Attachments

  • 124.jpg
    124.jpg
    21.8 KB · Views: 640
Wimbo huo wa Ntombi ulinifanya niwe mlevi kupita kiasi, ukitoka huo anakuja Mzee wa ende inde, inde moniii-Kanda Bongoman, halafu Arlus Mabele; ila sasa nakunywa kidogo tu

By then hata ule wimbo wa vunja mifupa ulikuwa kwenye chati.
 
1987 braza angu alileta kanda ya alpha blondy enzi hizo nyimbo km idjidja, afrique, intepranetary revolution, brigadier sabare kwa kweli mimi kwangu alpha blondy ni zaidi ya lucky dube! Nyimbo zake zinanipa raha mno! Ile afrique bd inaleta burudani. Mbili miaka ya mwanzo ya tisini yaani kuanzia 1989 nikuwa Iringa nilipenda sana kusikiliza idhaa ya kingereza ya kenya, walikuwa wana vipindi vizuri sana na miziki ya kizungu waliipiga sana. Namkumbuka mtangazaji wa reggae time kbc nairobi akiitwa jeff mwangeni aka crucial jeff jamaa alinifanya nisikikose hicho kipindi kila alhamis saa mbili kamili asubuhi mpaka saa tatu. Tatu miaka hiyo family yetu hatukuwa vizuri sana mzee wangu alipenda sana kusikiliza redio kenya ya kiswahili siku za jmosi na jpili akiwa home, wakati huo tulikuwa tunakamua ndondoz daily, kenya ni wataalam sana wa kutangaza bidhaa zao, lile tangazo la roiko mchuzi mix lilituokoa ndondoz zetu zikatafutiwa mchuzi mix sasa tukawa tunatafuna ndondoz kwa flavor tofauti. Nne ilikuwa ikifika saa tatu kasorobo mzee anazima radio yake anaichuku room kwakee utasikia tu tatu kamili kale ka mziki ka majira enzi hizo radio Tanzania.
 
By then hata ule wimbo wa vunja mifupa ulikuwa kwenye chati.

We acha tu, akina Luciana na wengine, RIP Pepe Kale. Siku hizi watu wapo bize na miziki hewa ya keyboard aka bongo fleva, hovyo kabisa na siburudiki kabisa. Kuna bar chache ninazotembelea ambazo hayo mabongo fleva ni marufuku na hapo huwa naburudika kweli.
 
tano kombe la dunia 1990 Italy. Simba wa nyika Cameroun walipoweka historia kwa kufika robo fainali za michuano ile. Hakukuwa na runinga basi taarifa tukizipata kupitia radio Ujerumani na BBC. Ikifika kumi na mbili tupo sitting room na dingi alipenda sana bbc na radio ujerumani. Kulikuwa na mtangazaji wa kipindi cha michezo cha radio ujerumani akiitwa Ramadhani Ally sauti yake nzito ilikuwa tamu mno! Hasg pale alipokuwa akisema simba wa nyika Cameroun wameweka historia mpya! Hasa pale Rogger Milla alipopigilia msumari wa mwisho ktk jeneza la Argentina!
 
sita sista angu mkubwa na blues za juddy boucher, sista angu mdogo aliporekodi twaarab za Nasma kidogo akiwa na tot kwenye kanda yangu mpya ya Bob Marley ikiwa ni ktk collection ya kanda kumi na sita nilizokuwa nazo, nyumbani hapakukalika siku hiyo!
 
mmesahahu majira na kombora na kila j1 kipindi cha salam za wagonjwa mahospitalini pamoja na kipindi cha chakula bora

mchezo wa redio je??
 
last but not least 1980 ndipo mzee aliponunua hiyo radio ilikuwa na vitaa taa vinawaka, sumbawanga huko ndipo nilipo fall in love na DDC mlimani park orch, ile saa kumi na moja kipindi cha jioni njema wanapiga wimbo wa ddc duniani kuna mambo bitchuka na stereo sauti yake inapanda mpaka mawinguni ..nyimbo km selina, mamaaa nimesahau masantula ngoma ya mpwita arrgh jamani maisha yalikuwa matamu sana, kubasi aka makatambuga ndo fasheni, wajanja wanazamia meli kwenda ugiriki, ulaya kunaitwa mtoni nna mengi mno ngoja niishie hapo
 
Ule wimbo/mziki kabla ya Majira Radio Tanzania Dar es Salaa (RTD) ulikuwa unanikosha sana ka kuna mtu anao please wekeni hapa!
 
We acha tu, akina Luciana na wengine, RIP Pepe Kale. Siku hizi watu wapo bize na miziki hewa ya keyboard aka bongo fleva, hovyo kabisa na siburudiki kabisa. Kuna bar chache ninazotembelea ambazo hayo mabongo fleva ni marufuku na hapo huwa naburudika kweli.

hapo congo ya kinshasa kwa papaa mobutu wacha kabisa kuna wanamuziki walilkuwa balaa
tukianza na,wazee wa nyuzi kina daly kimoko,diblo dibala,lokasa ya mbongo na nene chaku,wazee wa sauti nyiboma mwangido,papy tex ,shimita,wazee wa sokous na kwasakwasa, hapo unamkuta pepekale,alein konkou,bongomani,damien aziwa,evoloko,boziboziana,gina wa gina,arlus mabele,
bongo enzi za......
..
Wowowooooopoooooo! Tukunyema mpaka chini,.waaaaaa!
enzi hizo ukiambiwa mambo vipi? unajibu mambo waaaaaa! hakukuwa na mambo vipi halafu unajibu poa, kama ilivyo sasa.
 
Me nakumbuka kipindi cha mama na mwana kilikuwa mchana mara nyingi wakati huo nilikuwa nawait chakula, na mother yuko jikon anapika.


Vijana Jazz, Maques,Bayankata na Kalala, Urafiki Jazz, DDC Mlimanmi, Msondo na Lucky Stars!
 
Back
Top Bottom