Unakumbuka nini kuhusu hawa jamaa?

Unakumbuka nini kuhusu hawa jamaa?

1.Extra..Rogaroga,Fred Benjamin Ni moooto.
2.Defao alikuja bongo akakutana na mabingwa wa kuzibua akawa hoi bin taaban.
3.BCBG..Jb Mpiana,Alan Mpera,Braise bura nk ni motooo
4.Madilu alichukua nafasi Franco vizuri..alale anapostahili
5.Awilo kipindi kile anapiga drums mpaka leo amekuwa mwanamuziki kamili bado anakimbiza...

Hapo juu ni Fred Nelson mkuu, Defao walimfanyaje wabongo?
 
Mkuu umenikumbusha mbali sana yaani "time immemorial" enzi ambazo muziki ulikuwa mziki.... hongera sana kwa kunitendea haki kwa thread nzuri muda huu.

asante mkuu tuko pamoja...
 
hii ni miziki isiyokuwa na wabana pua na kutengenezewa mirindimo kwenye studio za miziki. wakipiga live sauti na vyombo vinatoka kama walivyorekodi.siyo kuruka ruka na kushika shika nyeti wakiwa jukwaani kwa hawa wa kizazi kipya.

bahati mbaya albums zao za siku hizi hatuzisikii maana ndiyo hivyo tena tunajua nani wamejaa kwenye radio fms na tvs.

kasoro yao kubwa ilikuwa ni kujichubua...
 
kipindi ambapo muziki wa kikongo ulikuwa unatamba...mambo ya africa bambataa na marehemu chifupa

Nimemkumbuka Marehemu Amina,kipindi chao kilikuwa juu mbaya akiwa na dj Charles na prince Baina Kamukulu...kitambooo
 
Kuna magwiji hawa wengine enzi hizo hizo walisumbua sana nao:

1:Beevans Ghatto
2:Aurlus Mabele na
3:Luciana Bokilo
 
hebu wenye majina ya nyimbo za hawa jamaa watuwekee hapa ili tuzipakue.
 
Okobanga bilo tee, okobanga nzambe na ngai Koffi olomide( Loi), this was one of my favorite, kwenye ubarikio nilikuwa nacheza mpka napewa shingi 50.
 
Duu umenikumbusha mbali utotoni, nakumbuka kuna muuza mihogo alikuwa kachumbali yake alikuwa anaiita loi uliikosa hiyo lazima unune. Kuna siku tulishindanishwa kucheza loi nikashindwa wee wacha nilie....ha ha ha natamani kurudi utoto!!
 
Hapo bado bongoman,pepe kale mbili abeli bila kusahau yondo sista mwana mama oh mama....
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom