Unakumbuka Mwaka ule Mbwa alipoitwa "Shemeji"?

Unakumbuka Mwaka ule Mbwa alipoitwa "Shemeji"?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Posts
34,251
Reaction score
44,586
Nilikuwa napiga stori na ndugu yangu mmoja kuhusu kesi ya Strauss-Kahn na kukumbushana jinsi wale wanajeshi wa Uingereza waliotuhumiwa kubakwa walivyoachiliwa kwa moyo mkunjufu na serikali yetu ili "tusichafue jina la Tanzania". Ndipo nikakumbuka kisa kile cha yule mbwa wa Wajerumani ambaye baadaye aliitwa "shemeji" na kusababisha mbwa kuitwa "mashemeji". Kilikuwa ni kisa cha kusikitisha sana sijui kama watu wanakikumbuka.

... nikiacha kupata kichefuchefu nitawasimulia...
 
nakumbuka vizuri sana....yule dada alikuwa wa iringa() na kama kumbukumbu zangu nazichanganya alitetewa na ISSA SHIVJI, hii ikanikumbusha ksa kingine cha mbwa aliyepandishwa kizimbani kwa kuitwa "UHAMIAJI"
 
Lakini alikuwa ni dada aliyekuwa anajiuza....aliulizwa kama anaweza na akakubali....na alilipwa kulingana na kazi aliyoomba
 
Pia miaka kama mitatu minne iliyopita kuna afisa ubalozi wa Saudia (tena ngazi ya chini kabisa) alimbaka housigeli akapiga makelele walinzi na some people waliokuwa around walishuhudia. Kilichoendelea yule jamaa adhabu yake ilikuwa ni kufukunzwa nchini. Hakuwahi kufikishwa hata ktuo cha polisi kuhojiwa.

Sasa ukiangalia huyo bwana Strauss na heshima ya licheo lake, na historia yake na pia future prospects sheria inafuata mkondo wake pingu kama kawaida, dhamana inagoma kama walalahoi and no complains from the public. Eti sijui anadhalilishwa.....
 
huyu bwana mkubwa wa IMF amekuwa denied bail, hapa kuna somo tujifunnze,utawala wa sheria na uhuru wa mahakama.....kwani mambo ya kisiasa na kidiplomasia kuingilia uhuru wa mahakama bado ni tatizo kubwa
 
Kwa tukio hili hana kinga ya kibalozi kwa sababu kwa policy za IMF unapata immunity ukiwa kwenye "official duties" ambazo zimegharimiwa na IMF pekee. Sasa kule New York alikwenda kwa matembezi yake binafsi na kwa gharama zake. IMF haikumlipia gharama za hotel na usafiri. Nadhani hapa IMF policy ziko tofauti kidogo na sheria za kinga ya kibalozi kwa mabalozi wa nchi chini ya mkataba wa Geneva.
 
hizi kinga za kibalozi at times sizielewi....ni kuwa these people can not be prosecuted even after committing serious offence au ni vipi ?
 
Ukishaendekeza kuwa ombaomba, Yule unayemtegemea hata akikufanya nini utanyamaza ili usimuuzi. Ndivyo tulivyo.
 
Nakumbuka sana kisa cha mbwa.
Hapa ndipo kitu utawala wa sheria kilipo na kinafanya kazi. Huyu DSK ameshtakiwa na state ya New York wala si Federal.
Leo ameonekana na pingu kama marehemu Michaek Jackson, Martha stewart,milionea Ben madoff na bilionea Conrad Balck n.k.
Wenzetu sheria kwanza na haki kwa wote hadi itakapothibitika vinginevyo na vyombo husika.

Tunasafari ndefu sana.
 
Na unakumbuka wanajeshi wa Uingereza waliopelekwa mahakamani kwa kosa la kubaka na kumuua mdada wa Kitanzania pale Kunduchi? Kisha wakapewa VIP treatment kurudi kwao na si Keko mpaka kesi yao itakapokwisha. Hata kama dada huyo alikuwa 'working girl' bado yeye ni binadamu tena Mtanzania mwenzetu. Tanzania bado inafanya mambo ya 'Shamba la wanyama'. Zaidi ya yote, tuna sifa ya kusahahu haraka sana...!
 
nakumbuka vizuri sana....yule dada alikuwa wa iringa() na kama kumbukumbu zangu nazichanganya alitetewa na ISSA SHIVJI, hii ikanikumbusha ksa kingine cha mbwa aliyepandishwa kizimbani kwa kuitwa "UHAMIAJI"
Huyu "IMMIGRATION", alinyongwa kabisa!!
 
Mkuu hebu tukumbushe kidogo kuhusu huyu UHAMIAJI
 
Ingelikuwa kwetu kama tungeona aibu na kuendelea kumshikilia, basi Ukonga pangelipatiwa bonge la V.I.P. upgrade (kubwa kuliko la akina Liyumba au Mramba), kwa ajili ya diplomat huyo!!
 
Nilikuwa napiga stori na ndugu yangu mmoja kuhusu kesi ya Strauss-Kahn na kukumbushana jinsi wale wanajeshi wa Uingereza waliotuhumiwa kubakwa walivyoachiliwa kwa moyo mkunjufu na serikali yetu ili "tusichafue jina la Tanzania". Ndipo nikakumbuka kisa kile cha yule mbwa wa Wajerumani ambaye baadaye aliitwa "shemeji" na kusababisha mbwa kuitwa "mashemeji". Kilikuwa ni kisa cha kusikitisha sana sijui kama watu wanakikumbuka.

... nikiacha kupata kichefuchefu nitawasimulia...[/QUOTE]

Still nauseatic? lete vitu bana
 
Kwa utawala wa CCM na vibaraka wao hakuta kuja kuwepo utekelezaji wa sheria ulio wa haki. Msiende mbali yule mcanada aliye mtemea mate askari polisi pale banana aliachiwa na akaenda zake bila hata kupigwa kibao.
 
Na unakumbuka wanajeshi wa Uingereza waliopelekwa mahakamani kwa kosa la kubaka na kumuua mdada wa Kitanzania pale Kunduchi? Kisha wakapewa VIP treatment kurudi kwao na si Keko mpaka kesi yao itakapokwisha. Hata kama dada huyo alikuwa 'working girl' bado yeye ni binadamu tena Mtanzania mwenzetu. Tanzania bado inafanya mambo ya 'Shamba la wanyama'. Zaidi ya yote, tuna sifa ya kusahahu haraka sana...!
Ndo maana mi napenda sana China, hakuna mambo hayo....wacha waseme eti hawana Human Rights...Tena ukipatikana na hatia kifungo kwenda mbele na 'forced labour' juu......:dance:
 
Huyu "IMMIGRATION", alinyongwa kabisa!!

Katavi na Mahesabu, hebu iwekeni hii 'Uhamiaji' katika mtiririko ili tuelewe kilichojiri na kuingiza katika kumbu kumbu zetu.
Siikumbuki vizuri. Kwa ufupi tu.

Ahsante
 
Katavi na Mahesabu, hebu iwekeni hii 'Uhamiaji' katika mtiririko ili tuelewe kilichojiri na kuingiza katika kumbu kumbu zetu.
Siikumbuki vizuri. Kwa ufupi tu.

Ahsante

Kule Rukwa kuna mwananchi mmoja alikuwa na mbwa wake, na akamwita jina IMMIGRATION. Idara ya uhamiaji na ama polisi wakamkamata huyo mbwa na akafikishwa mahakamani pamoja na mmiliki wake kwa kosa la kudhalilisha idara ya uhamiaji kwa kumwita mbwa jina Immigration. Ila baadaye yule mbwa aliuwawa kwa kupigwa risari na polisi. Sina uhakika kama ilikuwa ni hukumu ya mahakama. Nadhani kesi haikufika mahakamani.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom