Unakumbuka Mwaka ule Mbwa alipoitwa "Shemeji"?

Mazee, hata angelikuwa Mtanzania huko UK na anafanya kazi ubalozini, kingelitokea hikihiki.

Ila wenzentu kwa sababu wana hela, wanachoweza kukufanya kwanza ni kuwatuma POLISI wa Madiplomat wanakudaka na kuandika barua nyumbani kwenu ili urudishwe......

Ukisharudi tu, unakuta Chenge anakusubiri akupeleke Mahakamani maana kashachukua hela kutoka kwa jamaa. Ukiwa nje kama Diplomat, huwezi shitakiwa ila watakufukuza na kuja kwenu kukufungulia kesi..................

Ahhh, yule dada wa Iringa? Wahehe wakaanza kumla shemeji yao. Nakumbuka jamaa mmoja pale Kibaha alimzaba mbwa kibao na kusema "mnatuharia dada zetu........." Masikini mbwa yule...........

Ule msemo wa akina dada wa "Hapendwi mtu......" wanaume waliupenda sana wakati huo na jibu likawa "........yeahhh, anapendwa Dog".
Pia miaka kama mitatu minne iliyopita kuna afisa ubalozi wa Saudia (tena ngazi ya chini kabisa) alimbaka housigeli akapiga makelele walinzi na some people waliokuwa around walishuhudia. Kilichoendelea yule jamaa adhabu yake ilikuwa ni kufukunzwa nchini. Hakuwahi kufikishwa hata ktuo cha polisi kuhojiwa.

Sasa ukiangalia huyo bwana Strauss na heshima ya licheo lake, na historia yake na pia future prospects sheria inafuata mkondo wake pingu kama kawaida, dhamana inagoma kama walalahoi and no complains from the public. Eti sijui anadhalilishwa.....
 
Katavi na Mahesabu, hebu iwekeni hii 'Uhamiaji' katika mtiririko ili tuelewe kilichojiri na kuingiza katika kumbu kumbu zetu.
Siikumbuki vizuri. Kwa ufupi tu.

Ahsante
Mkuu Nguruvi3 kuna mbwa huku Sumbawanga vijijini alipewa jina la "IMMIGRATION" na mmiliki wake. Jina hili liliwakera maafisa uhamiaji wa kule na kuamua kumshitaki yule mbwa. Hakimu akatoa hukumu mbwa yule anyongwe na hukumu ikatekelezwa. Habari za kunyongwa mbwa zilimfikia jaji mkuu(Nyalali....sina hakika) na akaamuru mwenye mbwa alipwe mbwa mwingine! Hii ilikuwa katikati ya miaka 90....... Hayo ndio ninayokumbuka kumuhusu "IMMIGRATION".
 
Kule Rukwa kuna mwananchi mmoja alikuwa na mbwa wake, na akamwita jina IMMIGRATION. Idara ya uhamiaji na ama polisi wakamkamata huyo mbwa na akafikishwa mahakamani pamoja na mmiliki wake kwa kosa la kudhalilisha idara ya uhamiaji kwa kumwita mbwa jina Immigration. Ila baadaye yule mbwa aliuwawa kwa kupigwa risari na polisi. Sina uhakika kama ilikuwa ni hukumu ya mahakama. Nadhani kesi haikufika mahakamani.
Ilikuwa ni hukumu ya mahakama, baada ya mwenye mbwa kulalamika na vyombo vya habari kuandika ndipo jaji mkuu akaamuru mwenye mbwa alipwe mbwa mwingine!
 
Ilikuwa ni hukumu ya mahakama, baada ya mwenye mbwa kulalamika na vyombo vya habari kuandika ndipo jaji mkuu akaamuru mwenye mbwa alipwe mbwa mwingine!
Na huyo hakimu aliyetoa hukumu ya kifo naye ikawaje?
 
Mazee, hata angelikuwa Mtanzania huko UK na anafanya kazi ubalozini, kingelitokea hikihiki.

Ila wenzentu kwa sababu wana hela, wanachoweza kukufanya kwanza ni kuwatuma POLISI wa Madiplomat wanakudaka na kuandika barua nyumbani kwenu ili urudishwe......

Ukisharudi tu, unakuta Chenge anakusubiri akupeleke Mahakamani maana kashachukua hela kutoka kwa jamaa. Ukiwa nje kama Diplomat, huwezi shitakiwa ila watakufukuza na kuja kwenu kukufungulia kesi..................

Ahhh, yule dada wa Iringa? Wahehe wakaanza kumla shemeji yao. Nakumbuka jamaa mmoja pale Kibaha alimzaba mbwa kibao na kusema "mnatuharia dada zetu........." Masikini mbwa yule...........

Ule msemo wa akina dada wa "Hapendwi mtu......" wanaume waliupenda sana wakati huo na jibu likawa "........yeahhh, anapendwa Dog".

......Mkuu kumbuka vyema na neno WO...WO....WOOO ndipo lilipoanzia..........baadaye kidogo kwa wakati huo naibu waziri waziri mkuu wa wakati huo naye alitoa onyo na nina mnukuu "nisisikie mtu kasema neno wo.......... mara tatu"

Wowowo lilishakuwepo mapema zaidi na zile picha za Homeboy Rashid "RADI" Washokera kama sikosei akiitangaza matamasha ya MK Group enzi wakiwa na Shem Kalenga wa Tabora Jazz.

Kulikuwa kunachorwa mimama mirefu na ma-wowowo makubwa, halafu vidume vifupi vimeshikilia wowowo ila mikono haifungi, hihihiiii :)
......Mkuu kumbuka vyema na neno WO...WO....WOOO ndipo lilipoanzia..........baadaye kidogo kwa wakati huo naibu waziri waziri mkuu wa wakati huo naye alitoa onyo na nina mnukuu "nisisikie mtu kasema neno wo.......... mara tatu"

Similar Discussions

Back
Top Bottom