Unakubaliana nayo au unaikataa vipi hii?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,738
109,174
" Intelligent people are full of doubts while the Stupid ones are full of confidence "

Tafsiri

" Watu Werevu mara nyingi huwa na Mashaka juu ya mambo lakini ile Mipumbavu ( Mipopoma ) na Mijinga ( Mingumbaru ) ndiyo huwa inakuwa inajiamini kabisa "

Kwa mfano Baba Nyumbani ukiwa unataka Kuanza Kununua Mkate au unapenda Mkate ila ukaona Wanafamilia wako wanakupinga na Kukuambia kuwa Baba ni kheri tununue Kwanza Sukari kwani ndiyo ina umuhimu halafu bado Wewe Baba ukawa unabisha tu kwakuwa umeshazoea Ubishi wako basi hapo jua ya kwamba Wewe ( Baba ) ni Ngumbaru ( Mjinga ) na Popoma ( Mpumbavu ) ila hao Wanafamilia wako ambao wameonyesha ' Mashaka ' mapema tu ndiyo Werevu / Vipanga sana.

Chanzo: Psychological Facts.

Nawasilisha.
 
Uko sahihi 90%

Kwahiyo Mkuu unataka kusema kwamba Mimi GENTAMYCINE nikitaka labda Kununua Baiskeli wakati hata Shuka tu la Kulalia sina au Godoro halafu Watu wakanishauri na bado nikawakatalia tena kwa ' Kuwabishia ' na Kununua hapo namaanisha kwamba Mimi ndiyo Ngumbaru na Popoma na hao walionishauri ndiyo Werevu au?
 
Hujawahi kusikia ile story ya Aesop jinsi jamaa kapoteza punda kwa kusikia ushauri ya watu. Jamaa kamkalisha mtoto juu ya punda, wakamwambia kijana amekosa adabu, mzee anatembea na kijana amekaa. Wakabadilishana, wakamwambia mzee ni katili anamtesa mtoto. Wakapanda wote wawili, wakamwambia wajinga, wanamchosha punda bila huruma. Wote baba na mtoto wakapiga miguu, bado watu wakawaiita wajinga, wanajitesa wakati usafiri wanao. Mwisho wakaamua kumbeba punda, wakapigwa teke ile kali na punda kasepa!

Lesson - kama hujiamini basi ushauri ya watu itakupeleka pabaya!
 
Mwerevu anapima kutafuta rational outcomes kwanza, mjinga hana hiyo.

Ndio maana genius Osama hakuwahi kudhubutu kujiua kwa kujilipua, ila mapopoma yake yalijilipua kwa kuaminisha mbinguni yatakuta zawadi ya wanawake 100 bikira kila mmoja.
 
Kuna mtu aliwahi kusema:

The test of a first-rate intelligence is the ability to hold two opposed ideas in mind at the same time and still retain the ability to function.

Niliwahi kuisoma hii sehemu na mpaka leo naitumia kupima uwezo wa akili wa mtu.
 
Kuna wanaokishauri ununue sukari kwa sababu ni tamu,ili wailambe.

Hawajui kwamba mkate unaweza kula bila chai,hata na maji tu na siku ikapita.

Hawajui kwamba mkate unauzwa bei ndogo ukilinganisha na kilo ya sukari.

Hawajui sukari ina madhara kwako sababu ya uzee wako sasa,wanajiangalia wao tu.
 
Back
Top Bottom