Unajua ni kwanini kuna watu huzaa mapooza?

Unajua ni kwanini kuna watu huzaa mapooza?

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
375,535
Reaction score
870,102
Hili neno linatajwa kwenye Bible kuwa 'na wala hakutakuwa na kuzaa mapooza tena.' Ila hatutalijadili kwa mrengo wa kidini
Mapooza yapo kwenye maisha yetu ya kila siku, mapooza kwenye kipato-una kipato kizuri lakini huna maendeleo.

Mapooza kwenye kazi-una elimu nzuri, una bidii kazini lakini hupati promotion yoyote, mapooza kwenye biashara-umewekeza vizuri tu lakini haikui, mapooza kwenye mahusiano-miaka nenda miaka rudi unaishia kwenye uchumba tu nk nk.

Lakini mada ya leo imejikita kwenye kuzaa mapooza, yaani watoto mapooza, hawana ulemavu wa viungo vyovyote vya mwili wala si kwamba ni mazezeta au mazuzu la hasha, ni watoto kamili wenye kila kitu sometimes elimu hata na kipato kizuri au kipaji nk.

Sasa upooza wao unatoka wapi? Hawa hawana msaada kwa wazazi familia wala Jamii, ni wao na umaarufu wao na kazi yao na kipato chao aasi , hata kuishi ni mpenzi ni shida.

Wana wazazi wanaohitaji msaada wao, lakini unakuta hakuna kitu, ni wasumbufu, kesi haziwaishi, ni watu wakuleta matatizo kwenye Jamii siku zote hawa ni mapooza.

Mapooza haya yanatokana na nini? Hapa tusimsingizie Mungu haya ni matokeo ya matendo mabaya ya mwanadamu mwenyewe.Ukichunguza mara nyingi watoto wa namna hiyo background yao ina mushkeli, hukosi kukuta.

-Ni mtoto wa kubambika/kubambika
-Ni mtoto wa kambo
-ni mtoto mimba ya ndugu, akabambikwa mtu mwingine
-Ni mtoto aliyepatikana bila ridhaa ya mzazi mmojawapo, kupewa mimba na kukimbiwa, au binti kulengesha ili azae na mtu nk

Mapenzi ya siri/ usaliti kati ya ndugu na marafiki, hasa kama unayemfanyia hivyo kafariki, au kapata ulemavu au matatizo ya dunia halafu umchapie.

Haya yote yatatokea kwa sababu ya roho roho inaona kila kitu hata kama haitapeleka taarifa kwenye ufahamu utaokufanya wewe ugundue jambo hilo, roho hubaki na habari kamili na huandaa malipizi yenyewe.

Kwahiyo ndugu zangu wa MMU unapokuwa na mahusiano yoyote tafakari kwa makini yale unayofanya kama hayakuachi na 'sense of guilty' kuepuka kuzaa mapooza.
 
Hii mada nimeielewa na imenifunza mengi
Katika maisha kuna mambo unaweza kufanya bila kujali lakini kumbe madhara yake ni makubwa kuliko mtu alivyochukulia
 
huwa napata shida sana kuzielewa mada zinahusisha mambo ya kiroho
 
mtaji ni halali , nguvu sijachanganya , kuhusu eneo na wafanyakazi ndio silifahamu.Biashara yenyewe ni ya usafirishaji mizigo kwenda nje ya chi kama rwanda nk
 
mtaji ni halali , nguvu sijachanganya , kuhusu eneo na wafanyakazi ndio silifahamu.Biashara yenyewe ni ya usafirishaji mizigo kwenda nje ya chi kama rwanda nk

Kama yote yako sawa basi usijali na mtangulize sana Mungu kwenye kila kitu kwakuwa kuna kuanguka mara nyingi kabla hujasimama, yote ni kukuandaa kwa jambo kubwa zaidi na la kheri, lakini vilevile kuna kipindi Mungu hutujaribu na kuona tuko imara kiasi gani kiroho
 
Kama yote yako sawa basi usijali na mtangulize sana Mungu kwenye kila kitu kwakuwa kuna kuanguka mara nyingi kabla hujasimama, yote ni kukuandaa kwa jambo kubwa zaidi na la kheri, lakini vilevile kuna kipindi Mungu hutujaribu na kuona tuko imara kiasi gani kiroho
……….Amen
 
Ile negative power ya kulalamika na kuumia humwendea yeye lakini huja kumuathiri mtoto kwakuwa tayari yeye ni sehemu ya yule baba na ndio chanzo cha yote hayo, japo wewe unaweza usiwe na tatizo kabisa na mtoto
Unapokumbana na hali kama hii mshukuru Mungu wala usiweke visasi na vinyongo rohoni

be blessed dear.
 
Back
Top Bottom