Unajua kwanini CHADEMA wanataka Bunge Live?

Kulingana na Katiba ya CHADEMA kuhusu kanuni za wabunge. Kwamba mbunge wa chadema sio mwakilishi wa wananchi bali ni mwakilishi wa chama. Na inasema wazi mbunge anapokuwa bungeni lengo lake kuu ni kukijenga chama na si kutetea maslahi ya wananchi.

Ndio maana hawa chadema wanataka kupitia mgongo wa haki za vyombo vya habari kwa lengo la kujijenga kichama. Hebu pitia vifungi hivi hapa chini halafu utanipa jibu:-

2.0. KANUNI ZA WABUNGE WA CHADEMA:
Bila kuathiri kanuni na taratibu za Bunge na maadili ya viongozi na wanachama wa CHADEMA kama ilivyo katika Katiba ya Chama, Wabunge kwa tiketi ya CHADEMA wanapaswa wazingatie yafuatayo:- (Tafsiri: neno Mbunge = Mbunge wa CHADEMA).

(a) Mbunge anatakiwa kutii na kutimiza maagizo anayopewa na Chama kupitia vikao halali, kama hakubaliani na maagizo hayo aeleze hivyo kupitia taratibu na ngazi zilizowekwa kwenye Katiba ya Chama.

(b) Itakuwa ni mwiko kwa Mbunge kukashifu CHAMA au kiongozi wa CHADEMA ndani au nje ya Bunge.

(c) Mbugne ni mwakilishi wa Chama, kwa hiyo katika michango yao bungeni ni lazima wazingatie na kusisitiza sera, mwelekeo na msimamo wa Chama kwa jambo husika.

(d) Mbunge anawajibika kutumia hadhi, uwezo, wadhifa na nafasi aliyonayo kama Mbunge kukijenga Chama ndani na nje ya Bunge.

(e) Mbunge anatakiwa kuwa na tabia ambayo ni mfano wa kuigwa katika jamii.
(f) Ni wajibu wa Wabunge kutoa taarifa za utendaji kazi katika Majimbo yao kwenye vikao vya Chama.

(g) Ni wajibu wa Mbunge kuchangia Chama na kushiriki katika shughuli za uenezi wa Chama kama itakavyoelekezwa na vikao halali.

Hapo kwenye rangi nyekundu ndio hapoooo sasa. Lengo lao sio kutetea wananchi bali kujijenga kichama tu.
gamba at work!!
 
Je unaongeleaje kuhusu kupiga kampeni ndani ya bunge kwa mujibu wa katiba yenu?
Hili neno "kampeni" lisikufariji kiasi cha kujitoa ufahamu! Hapa ungehoji juu ya namna inayotumiwa kupiga kampeni iwapo ungeona kasoro ungekuwa una hoja angalau kidogo. Lakini kuhoji kampeni yenyewe, hapo umeteleza. Chama chochote kinapiga kampeni kila siku na kila saa kwa kutetea sera zake, kufichua maovu yanayofichwa, na kufafanua kwa wananchi namna serikali inavyowalaghai. Zaidi viongozi wa chama wanapaswa kuwa watu safi machoni pa jamii. Tatizo lipo wapi mpaka hapo?!! Ndugu, jifunze kuelimishika. Hata kwenye uzi wako mwingne unaosema "DALILI ZA KUVUNJWA CHADEMA" tumetaabika sana kukuelewesha, na bado huelewi. Umeng'ang'ana na maneno badala ya maana yake. Badilika.
 
Ni kuulize tu swali moja. Je kazi ya bunge ni nini?
 
Basi kama hajui atumie Lugha inayotuunganisha kama taifa. Lugha pendwa ya Kiswahili.

Najua tangu mwanzo ulilenga Kiswahili, lakini kusema lugha ya Nyerere ulikosea, ila unaonekana ni mtu ambaye huwa hukubali kuambiwa "umekosea". Hata hoja uliyoileta najua huwezi kukubali kwamba umekosea. Lakini kama uko makini ukifuatilia wachangiaji, utagundua huna support yoyote.
 
Je unadhani nimeweka ili niwe na support?
 
Mbona hudai vikao vya chama chako cha chadema kioneshwe live?
Nani kakuambia mm chadema!!!!acha paniki ya kumpimia mgonjwa kwenye jua Na kudai anaumwa malaria.tofautisha vikao vya chama Na bunge mkuu.huwez kusema kikao cha CUF au ACT kionyweshwe hadharani kwa maana vikao vyao wana mission Na plan zao ila bunge lipo kwa ajili ya watanzania wote bila kujali chama au dini
 
Wabunge wa ccm wanapokaa kama kamati ya chama kupinga hoja za wapinzani hata kama jambo lenyewe lina maslahi mapana ya nchi.Nadhani mleta mada unajitekenya na kucheka mwenyewe hiyo haiitaji hata kifungu cha katiba.
 
Kulingana na Katiba ya CHADEMA kuhusu kanuni za wabunge. Kwamba mbunge wa chadema sio mwakilishi wa wananchi bali ni mwakilishi wa chama. Na inasema wazi mbunge anapokuwa bungeni lengo lake kuu ni kukijenga chama na si kutetea maslahi ya wananchi.

Ndio maana hawa chadema wanataka kupitia mgongo wa haki za vyombo vya habari kwa lengo la kujijenga kichama. Hebu pitia vifungi hivi hapa chini halafu utanipa jibu:-

2.0. KANUNI ZA WABUNGE WA CHADEMA:
Bila kuathiri kanuni na taratibu za Bunge na maadili ya viongozi na wanachama wa CHADEMA kama ilivyo katika Katiba ya Chama, Wabunge kwa tiketi ya CHADEMA wanapaswa wazingatie yafuatayo:- (Tafsiri: neno Mbunge = Mbunge wa CHADEMA).

(a) Mbunge anatakiwa kutii na kutimiza maagizo anayopewa na Chama kupitia vikao halali, kama hakubaliani na maagizo hayo aeleze hivyo kupitia taratibu na ngazi zilizowekwa kwenye Katiba ya Chama.

(b) Itakuwa ni mwiko kwa Mbunge kukashifu CHAMA au kiongozi wa CHADEMA ndani au nje ya Bunge.

(c) Mbugne ni mwakilishi wa Chama, kwa hiyo katika michango yao bungeni ni lazima wazingatie na kusisitiza sera, mwelekeo na msimamo wa Chama kwa jambo husika.

(d) Mbunge anawajibika kutumia hadhi, uwezo, wadhifa na nafasi aliyonayo kama Mbunge kukijenga Chama ndani na nje ya Bunge.

(e) Mbunge anatakiwa kuwa na tabia ambayo ni mfano wa kuigwa katika jamii.
(f) Ni wajibu wa Wabunge kutoa taarifa za utendaji kazi katika Majimbo yao kwenye vikao vya Chama.

(g) Ni wajibu wa Mbunge kuchangia Chama na kushiriki katika shughuli za uenezi wa Chama kama itakavyoelekezwa na vikao halali.

Hapo kwenye rangi nyekundu ndio hapoooo sasa. Lengo lao sio kutetea wananchi bali kujijenga kichama tu.
usilolijua wananchi wengi including CCM wenzio ndio wanataka hivyo sio chadema!

umekurupuka! au wewe ndie uliyepewa kazi ya propaganda hiyo humu na CC yenu? unapwaya!
 
Nani kakuambia mm chadema!!!!acha paniki ya kumpimia mgonjwa kwenye jua Na kudai anaumwa malaria.tofautisha vikao vya chama Na bunge mkuu.huwez kusema kikao cha CUF au ACT kionyweshwe hadharani kwa maana vikao vyao wana mission Na plan zao ila bunge lipo kwa ajili ya watanzania wote bila kujali chama au dini
Kwani chadema huwa wana mission zipi mpaka wajifiche wasiwe live?
 
Hakuna ndani ya katiba ya CCM imesema kuwa mwanaCCM kuwa mtetezi wachama pekee akiwa bungeni. Bali mbunge wa CCM ni mwakilishi wa wananchi.
Nnai amekuambia kuwa Mbunge wa mwananchi ni mwakilishi wa Mwananchi?

Wangekuwa wanafanya vikao vya kuja na sauti moja, ya kukubali jambo fulani, hata kama ni kwa maslahi ya wachache?
 
Kulingana na Katiba ya CHADEMA kuhusu kanuni za wabunge. Kwamba mbunge wa chadema sio mwakilishi wa wananchi bali ni mwakilishi wa chama. Na inasema wazi mbunge anapokuwa bungeni lengo lake kuu ni kukijenga chama na si kutetea maslahi ya wananchi.

Ndio maana hawa chadema wanataka kupitia mgongo wa haki za vyombo vya habari kwa lengo la kujijenga kichama. Hebu pitia vifungi hivi hapa chini halafu utanipa jibu:-

2.0. KANUNI ZA WABUNGE WA CHADEMA:
Bila kuathiri kanuni na taratibu za Bunge na maadili ya viongozi na wanachama wa CHADEMA kama ilivyo katika Katiba ya Chama, Wabunge kwa tiketi ya CHADEMA wanapaswa wazingatie yafuatayo:- (Tafsiri: neno Mbunge = Mbunge wa CHADEMA).

(a) Mbunge anatakiwa kutii na kutimiza maagizo anayopewa na Chama kupitia vikao halali, kama hakubaliani na maagizo hayo aeleze hivyo kupitia taratibu na ngazi zilizowekwa kwenye Katiba ya Chama.

(b) Itakuwa ni mwiko kwa Mbunge kukashifu CHAMA au kiongozi wa CHADEMA ndani au nje ya Bunge.

(c) Mbugne ni mwakilishi wa Chama, kwa hiyo katika michango yao bungeni ni lazima wazingatie na kusisitiza sera, mwelekeo na msimamo wa Chama kwa jambo husika.

(d) Mbunge anawajibika kutumia hadhi, uwezo, wadhifa na nafasi aliyonayo kama Mbunge kukijenga Chama ndani na nje ya Bunge.

(e) Mbunge anatakiwa kuwa na tabia ambayo ni mfano wa kuigwa katika jamii.
(f) Ni wajibu wa Wabunge kutoa taarifa za utendaji kazi katika Majimbo yao kwenye vikao vya Chama.

(g) Ni wajibu wa Mbunge kuchangia Chama na kushiriki katika shughuli za uenezi wa Chama kama itakavyoelekezwa na vikao halali.

Hapo kwenye rangi nyekundu ndio hapoooo sasa. Lengo lao sio kutetea wananchi bali kujijenga kichama tu.
We ulitaka iandikwe "Mbunge anawajibika kutumia hadhi, uwezo, wadhifa na nafasi aliyonayo kama Mbunge kukibomoa Chama ndani na nje ya Bunge"??????????
 
Nnai amekuambia kuwa Mbunge wa mwananchi ni mwakilishi wa Mwananchi?

Wangekuwa wanafanya vikao vya kuja na sauti moja, ya kukubali jambo fulani, hata kama ni kwa maslahi ya wachache?
Kwa matiki yako chadema wabunge wao sio wawakilishi wa wananchi bali ni wawakilishi wa matumbo yao. Ok!!! nimekupata vizuri sana.
 
Acheni mambo yenu ya uchonganishi wekeni na likatiba la Ficcm uone , na hata hivyo huu ndo utaratibu wa uandishi wa katiba yoyoyte lazima kuwe na kipengere cha kuvunja huo umoja au kikundi.

hata mkomae kuleta post za kuponda chadema bado ficccm ni chama chakavu
 
We ulitaka iandikwe Mbunge anawajibika kutumia hadhi, uwezo, wadhifa na nafasi aliyonayo kama Mbunge kukibomoa Chama ndani na nje ya Bunge??????????
Mbunge ni sauti ya wananchi pia ni mwakilishi wa wananchi. Kutoka mwanzo mpaka mwisho wa katiba ya chadema haijaeleza kuwa mbunge ni mwakilishi wa wananchi bali ni mpiga debe wa mbowe.
 
Annael, mbona sio Chadema pekee? CUF pia wamo, hata CCM wamo. Kwani hukumuona Mzee Mkinga pale Channel Ten alipokuwa akichuana na wale makada wa CCM wasiojitambua Mtela na Malik? BTW, wewe hukuwa unafurahi na kufaidika pale Bunge lilipokuwa linarushwa live?

Vv
 
Mbunge ni sauti ya wananchi pia ni mwakilishi wa wananchi. Kutoka mwanzo mpaka mwisho wa katiba ya chadema haijaeleza kuwa mbunge ni mwakilishi wa wananchi bali ni mpiga debe wa mbowe.
Weka na ya CCM tuone imeandikwaje kuhusu mwananchi
 
Hakuna ndani ya katiba ya CCM imesema kuwa mwanaCCM kuwa mtetezi wachama pekee akiwa bungeni. Bali mbunge wa CCM ni mwakilishi wa wananchi.

Umenukuu Ibara ya ngapi ya Katiba ya CCM hapo?

Vv
 
Back
Top Bottom