Emc2
JF-Expert Member
- Sep 26, 2011
- 16,808
- 16,873
Kulingana na Katiba ya CHADEMA kuhusu kanuni za wabunge. Kwamba mbunge wa chadema sio mwakilishi wa wananchi bali ni mwakilishi wa chama. Na inasema wazi mbunge anapokuwa bungeni lengo lake kuu ni kukijenga chama na si kutetea maslahi ya wananchi.
Ndio maana hawa chadema wanataka kupitia mgongo wa haki za vyombo vya habari kwa lengo la kujijenga kichama. Hebu pitia vifungi hivi hapa chini halafu utanipa jibu:-
2.0. KANUNI ZA WABUNGE WA CHADEMA:
Bila kuathiri kanuni na taratibu za Bunge na maadili ya viongozi na wanachama wa CHADEMA kama ilivyo katika Katiba ya Chama, Wabunge kwa tiketi ya CHADEMA wanapaswa wazingatie yafuatayo:- (Tafsiri: neno Mbunge = Mbunge wa CHADEMA).
(a) Mbunge anatakiwa kutii na kutimiza maagizo anayopewa na Chama kupitia vikao halali, kama hakubaliani na maagizo hayo aeleze hivyo kupitia taratibu na ngazi zilizowekwa kwenye Katiba ya Chama.
(b) Itakuwa ni mwiko kwa Mbunge kukashifu CHAMA au kiongozi wa CHADEMA ndani au nje ya Bunge.
(c) Mbugne ni mwakilishi wa Chama, kwa hiyo katika michango yao bungeni ni lazima wazingatie na kusisitiza sera, mwelekeo na msimamo wa Chama kwa jambo husika.
(d) Mbunge anawajibika kutumia hadhi, uwezo, wadhifa na nafasi aliyonayo kama Mbunge kukijenga Chama ndani na nje ya Bunge.
(e) Mbunge anatakiwa kuwa na tabia ambayo ni mfano wa kuigwa katika jamii.
(f) Ni wajibu wa Wabunge kutoa taarifa za utendaji kazi katika Majimbo yao kwenye vikao vya Chama.
(g) Ni wajibu wa Mbunge kuchangia Chama na kushiriki katika shughuli za uenezi wa Chama kama itakavyoelekezwa na vikao halali.
Hapo kwenye rangi nyekundu ndio hapoooo sasa. Lengo lao sio kutetea wananchi bali kujijenga kichama tu.