Unajivunia nini kuwa Mtanzania?

Najisikia aibu sana kuona watanzania wenzangu wakimuona mtu wa ngozi nyeupe (wazungu) wanamtetemekea sana, wakati hata wazungu pia wapo wa hovyo hovyo,
Swala jingine ni kwanini watanzania hawana confidence ya kuzungumza lugha ya taifa? Wakati wahindi na wachina wabakuja kwetu na wanabonga lugha yao bila wasi wasi
 
Wadau hebu tuambizane ni jambo gani ambalo ukiliona au kulifikiria kama Mtanzania unajivunia popote ulipo duniani na pia jambo ambalo ukilifikiria popote pale ulipo katika ulimwengu huu unaona aibu kabisa kujitambulisha kama mtanzania.
Mimi kwa upande wangu najivunia yafuatayo.
1.Kuwa ndani ya Nchi ambayo ina mlima mrefu kuliko yote Africa.
2.Kuwa katika Nchi ambayo ina kila aina ya vivutio vya asili vya kila namna.
Jaribu kujibu hili alafu utapata jibu lako rahisi.
JE NI KITU GANI AMBACHO POPOTEPALE UTAJIVUNIA KUHUSU FAMILIA YAKO. NA KITU GANI UKIKIFIKILIA POPOTE PALE UNAONA AIBU KABISA KUITAMBULISHA FAMILIA YAKO
 
1.Najivunia nchi yangu ina watu wastaarabu na haina mgogoro wa kijamii kama tuonavyo baadhi ya nchi kuingia kwenye migogoro ya kikabila au imani za kidini kupita kiasi tofauti na hapa kwetu,lakini (2)Napata aibu pale waTanzani sisi wenyewe unakutana na watu wanaifedhehesha nchi yao wenyewe kwa kuiponda na maneno mabaya mabaya mbele za watu wa nchi nyingine ambao wao huiona Tanzania ni nchi nzuri yenye amani na lasilimali yenye kupendeza
 
Nahisi aibu kila ninapoona hakuna maendeleo zaid ya kuomba kuomba ili hali sisi ni matajiri nyuma ya Congo
 
Nakumbuka kipindi cha maujaji ya albino, nilijisikia aibu sana, my colleagues walikuwa wananishangaa sana. "Tanzanians kill albinos to get wealth", nilikuwa najisikia vibaya nchi yangu kuwa na sura chafu duniani, halafu CNN walijitahidi sana kufanya coverage ya ile issue.
 
Najivunia kua na mkuu wa nchi mwenye misimamo na maamuzi magumu kwa manufaa ya taifa.

Pia naona aibu kua na chama kikuu cha upinzani chenye ukabila udini na ukanda lakin pia richa ya ruzuku kubwa wanayoipata lakini bado makao makuu yao wamepanga.
Naona aibu sana kua ktk nchi ambayo wapinzani ni wanafiki wazandiki lakini viongozi wao ni wakwepa kodi wakubwa mpaka wengine wanatolewa vyombo nje.
 
Kweli kabisa ile ishu ya albino ilikuwa ni aibu kubwa sana kwa Tanzania.
 
Najivunia kuishi katika nchi yenye watu wakarimu na wenye umoja wa kitaifa,
Naona sana Aibu ujinga wa wananchi wa tanzania, watz wengi wanaakili ndogo sana. Mbaya zaidi ni kua Takwimu zinaonesha 40% ya watoto ni retarded.
 
Najivunia kua na mkuu wa nchi mwenye misimamo na maamuzi magumu kwa manufaa ya taifa.

Pia naona aibu kua na chama kikuu cha upinzani chenye ukabila udini na ukanda lakin pia richa ya ruzuku kubwa wanayoipata lakini bado makao makuu yao wamepanga.
Naona aibu sana kua ktk nchi ambayo wapinzani ni wanafiki wazandiki lakini viongozi wao ni wakwepa kodi wakubwa mpaka wengine wanatolewa vyombo nje.
Duh!! Najivunia Amani, Upendo na mshikamano wa tz, pia nchi kuwa na rasilimali nyingi na Ardhi kubwa yenye rutuba. Naonea aibu kuishi nchi moja na Mtu Docile, Dumb, retarded and Brainwashed kama wewe.
 
najivunia wananchi wa tz wanapanga mipango kwa kuongea sana sana kuliko vitendo wamejawa na mambo ya kisiasa tu

kila kitu ni kisiasa sijui tutafika au ndo nn
 
Duh!! Najivunia Amani, Upendo na mshikamano wa tz, pia nchi kuwa na rasilimali nyingi na Ardhi kubwa yenye rutuba. Naonea aibu kuishi nchi moja na Mtu Docile, Dumb, retarded and Brainwashed kama wewe.
samahani mkuu wewe ni navigator au nakufananisha?
 
Hiyo Avatar inadhalilisha watoto wa Kiafrika na waafrika kwa ujumla. Kwani hakuna picha nzuri inayo onesha Africa na utamaduni wetu!? Hizo picha mbaya ndio hutumiwa na wazungu kudefine hali ya watoto wa Africa na utamaduni wetu kitu ambcho sio sahihi kabisa.
Kwa upande wako unaweza kuhisi kwamba nawadhalilisha hao watoto lakini kwa upande wangu hii anawakilisha maisha ambayo wengi tumekulia ambapo asilimia kubwa ya watoto wako katika hali kama hii.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom