Unajivunia nini kuwa Mtanzania? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Unajivunia nini kuwa Mtanzania?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by STK ONE, Sep 12, 2012.

 1. STK ONE

  STK ONE JF-Expert Member

  #1
  Sep 12, 2012
  Joined: Dec 31, 2011
  Messages: 628
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Watz tuna safari ndefu sana kuelekea kufika kule tunakotaka. Kwanza, hakuna nia ya dhati ya kutaka kutekeleza kwa vitendo kauli zetu. Hili linajirudia mara kwa mara katika utendaji wa viongozi serikalini na hata katika taasisi zake. Tumekuwa watu wa kuongea tu bila ya kuwa na strategies of implementing what we say. Yaani kila kitu kimekuwa politicized. Hakuna hata sekta moja ambayo tunajivunia kuwa tumepiga hatua na sasa tunaweza kufikiria mambo mengine.

  Bado tuna lalamika na barabara, bado tuna lia shida ya maji nchi nzima, bado tunalia wodi na vitanda mawodini havitoshi, bado tunalia ubora wa elimu ni duni na watoto wanahitimu elimu ya msingi hawajui kusoma wala kuandika lakini wanachaguliwa kuingia kidato cha kwanza. Bado tunalia maliasili hazitunufaishi, tanzanite, dhahabu, almasi, shaba, makaa ya mawe, gesi na mafuta vyote vipo, lakini umaskini unaongezeka kila siku. Bunge letu limejikita kupitisha bajeti yenye nyongeza za kodi kwenye bia na soda.

  Serikali imefilisika kimawazo na hakuna ubunifu wa miradi ambayo italiongezea taifa mapato ya ndani. Hatuna viwanda vya ndani vya kutengeneza nguo, pamba kanda ya ziwa inadoda, hakuna wanunuzi, wanaonunua wanajipangia bei kana kwamba walilima wao. Wakulima wa tumbaku huku Mpanda hawajalipwa, tangu walianza kulima tumbaku mwaka jana mwezi wa tisa, hadi mwezi wa tisa mwaka huu wameanza msimu mpya wa kilimo, fedha za soko la tumbaku ya mwaka jana hawajaipata.

  Ni kipi tunajivunia kama watz? JK anazindua vyuo vikuu vipya, lakini nani atafika kusoma huko? Masharti ya mikopo yamekuwa magumu, watoto wa masikini lini watafika chuo kikuu? Shule za sekondari ambazo zilikuwa zinafaulisha watoto kwenda advanced level, zilipewa hadhi ya kuwa za A LEVEL tu, lakini leo hii shule kama MPANDA GIRLS imebaki na wanafunzi mia mbili tu wa advance, wengine wanahama na wengine hawaripoti kabisa. Shule haina waalimu, miundombinu mibovu, imefikia hatua mkuu wa shule ameomba halmashauri impelekee watoto wa O level tena, maana madarasa na mabweni ni matupu. Nini serikali inafanya?

  Kilimo kwanza kimeshindwa vibaya, pembejeo ni ghali sana, mvua zenyewe hazitabiriki hata kidogo, japo kuwa tumezungukwa na vyanzo vya maji kila mahali, lakini bado tunategemea mvua za Mungu ilihali tunakata miti na kuchoma mkaa kila siku. Ni miti mingapi inakatwa kwa ajli ya mkaa Tz nzima kwa siku? Lakini bado serikali inatuaminisha kuwa mvua itanyesha na tuendeleze sera za kilimo kwanza. Sote tunajua, sehemu ambayo haina miti, hakuna mvua kabisa au kuna mvua za kusua sua, na kila siku miti inakwisha, serikali haina njia mbadala ya kuwafanya watz watoke kwenye matumizi ya kuni na mkaa ili kulinda misitu iliyopo kwa ajili ya kuendelea kupata mvua, umeme na gesi ambavyo vingelitumika kama nishati mbadala ya kupikia, ni ghali sana, na wengi hatuwezi kumudu. Kipi tunajivunia?

  Maji ya ziwa Tanganyika, mto malagalasi, mto pangani, bahari ya hindi, ziwa victoria, ziwa nyasa (Japo wamalawi wanalitaka lote), ziwa rukwa na mito na mabwawa chungu zima vingeweza kutumika kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji ili kuondoa utegemezi wa mvua na watu wangezalisha mazao ya chakula na biashara mwaka mzima, umasikini ungelipungua kwa kiasi kikubwa, lakini wapi, ni aibu sana nchi kama JAPAN ambayo inaingia tz kama mara kumi kutuuzia mchele ilihali tuna mabonde mengi sana ya kulima mpunga karibu kila kona ya nchi hii. Eti, mwenzangu unajivunia nini kuwa Mtz?

  Hifadhi za taifa zenyewe zimegawanywa kwenye vitalu, vitalu vinamilikiwa na viongozi na/au wafuasi wao. vitalu vingine vimeuzwa kwa wazungu kwa ajili ya uwindaji na utoroshaji wa wanyama wetu. Ndani ya hifadhi, (kwa mfano Katavi National Park) kuna camp sites, ambazo wazungu wanazimiliki na wao ndio wenye dhamana ya kuleta wageni kutoka katika nchi zao na wao wanalipa vikodi kiduchu katika hifadhi zetu. Lini hifadhi hizi zitajiendesha? Huko kwenye camp site, haruhusiwi mtu yoyote kuingia, imefikia hatua kuna viwanja vya ndege, kinachoingia na kutoka katika camp site hizo hakuna anayefahamu. Watu wanabeba madini, pembe za ndovu, ngozi za simba na chui kinyume cha taratibu. Tunajivunia nini katika nchi yetu?

  Uongozi umeoza. Hakuna uwajibikaji. Ni kama familia ya kambare, baba ana ndevu, mama ana ndevu, mtoto na waijukuu wote wana ndevu, huwezi kutofautisha baba wala mkuu wa kaya ni nani. Kuanzia kwenye Urais hadi uenyekiti wa mtaa, hakuna ambaye anaweza kumuwajibisha mwenzake. kila mtu ana mamlaka katika eneo lake, na mamlaka hayo, hayaingiliwi na mwingine. Matukio makubwa ya mauaji yanatokea katika nchi, lakini mkuu wa kaya kama hayupo vile, eti ni upepo tu, utapita. Nchi ni kama haina mtendaji mkuu wa serikali, Pinda hayupo, Kikwete yuko ughaibuni kila siku, sijui lini Kibaki alikuwa na ziara ya kiserikali nje ya nchi? Hata Sina kumbukumbu, pengine kwa sababu niko pembezoni mwa nchi.

  Rushwa imetamalaki kila idara ya serikali na chama tawala. Tumeshuhudia juzi hapa kwenye uchaguzi wa mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya mpanda, fedha zilitolewa kuhongwa wajumbe kana kwamba ni uchaguzi mkuu. Lini ccm watasimamia maneno yao? Lini takukuru watakuwa na meno ya kutafuna waliowaweka kwenye madaraka? Lini bias itaisha katika nchi hii kutoka kwenye vyombo vya dola? Watendaji wote wa serikali wako bize na harakati za kujiimarisha kwa ajili ya uchaguzi wa 2015 kana kwamba huu ni mwezi wa sita 2015. Kila mmoja yupo ki maslahi zaidi, minyukano kila kona na vijembe visivyoisha. Eti, ni kipi unajivunia kuwa mtz?

  Hata baada ya miaka 50 ya uhuru, bado watz zaidi ya % 70 wanafikiria watakula nini leo. Maendeleo yanayosemwa kwenye tafiti mbali mbali na kwenye utekelezaji wa ilani ya ccm hayaendani na hali halisi vijijini na mijini. Hali ni mbaya sana vijijini. Watu wanaishi kwenye makazi mabovu, miundo mbinu ni mibaya, mavazi ya hovyo, chakula kibovu, kifupi, watu ni maskini sana. Bei za vifaa vya ujenzi inazidi kupanda, cement, bati, nondo, rangi, misumali havishikiki, lini watu wataishi maisha bora? Lini watu wataishi kwenye nyumba za bati zenye sakafu? Hadi leo hii naandika waraka huu, watu hawajawahi kulalia kitanda chenye godoro. Ni tz hii hii. Watu wanalalia vilago (Misengele) vinavyotengenezwa kwa matete yanayomea kando ya maji. Mtu akiamka asubuhi anaondoka na mistari ya matete kwenye uso na sehemu nyingiine za mwili wake. Ni Tz hii ambayo rais kila siku anazurura kuomba misaada ya maendeleo. Ni nchi hii ambayo rais anasafiri na msafara wa watu zaidi ya hamsini kwenda nje ya nchi. Ni nchi hii ambayo rais anatumia zaidi ya Tsh. mil. 200 kwenye safari yake moja, lakini wananchi wake, bado wanawaza watakula nini leo. Aibu sana. Sijui hata nijivunie nini kuwa Mtz.

  Yaani wtz tulio wengi tumekuwa kama vichaa, tunatembea tunaongea wenyewe barabarani, tunawaza kila siku tunaona afadhali ya jana, hakuna unafuu wa maisha japokuwa nchi yetu ina kila neema ya raslimali na utajiri mkubwa. Tunaishi kifukara na kimaskini katika nchi tajiri. Maisha ni magumu hata hayasimuliki. Juzi nimepita kwenye kijiji kimoja hapa Mpanda kinaitwa Kasokola, kulikuwa na mkutano wa kukusanya maoni ya katiba mpya. Japokuwa kijiji kina wakazi wengi sana, lakini waliohudhuria kwenye mkutano walikuwa wachache sana. Nilipata fursa ya kuongea na wachache ambao walikuwa bize na shughuli zao kando tu ya mkutano. Niliwauliza kwa nini hawatoi maoni yao ya katiba mpya? Majibu niliyoyapata. "Katiba nini? Hapa nilipo hata sijui jioni nitakula nini, halafu nikapoteze muda kuongelea kitu ambacho kitawapa wengine chakula na maisha mazuri?" Watu wamekata tamaa, hata hawana muda wa kushiriki kwenye mambo ya msingi ya Taifa kwa sababu tu hawajui nn watakula.

  Hakuna kitu kibaya kama njaa. Huwa tunapata mawazo ya kujenga, kuvaa vizuri, kununua magari na kujenga maghorofa, baada ya kushiba. Kama mtu una njaa, wazo pekee linalokuwa kichwani ni "Wapi nitapata chakula." Kama serikali yetu hata baada ya miaka 50 ya kuwa huru imeshindwa kuwahakikishia wananchi chakula cha uhakika, nini imeweza? Maana mahitaji ya msingi ya binadamu (Human basic needs) ni chakula, mavazi na malazi. Vyote hivi, bado ni tatizo kwa Mtz wa kawaida. Chakula ni issue, mavazi usiseme, ni aibu tupu, malazi ndiyo hayo, ukiiona nyumba tu kwa nje, unajua humo ndani hakuna kitanda wala godoro, watu wanajifunika kanga, hata shuka hakuna. Ni nini unajivunia kuwa mtz?

  Binafsi, sioni hata moja la kujivunia. Pengine ni kutokana na aina ya maisha ninayoishi na aina ya maisha ambayo nawaona wengi wa watu wanaonizunguka wanaishi. Nikisikia kuwa hapa Mpanda kuna utajiri wa dhahabu, almasi, chuma, Galena, wanyama pori, misitu ya mbao kila aina, halafu nikilinganisha na aina ya maisha ambayo wakazi walio wengi wa mji wanayoishi, kweli kutoka moyoni mwangu, nashindwa kupata kitu cha kujivunia kuwa Mtz. Ardhi ni zuri, inastawisha karibu kila zao la chakula na mengi tu ya biashara kama mpunga, tumbaku, na mengine mengi. Maji ni mengi sana, kuna chem chem nyingi sana maeneo ya Katuma, Katobo, Sibwesa, Ngomalusambo, na vijiji vingine vingi sana. Kuna mito ya uhakika mwaka mzima, kama mto katuma na mto Mpanda na mingine mingi ambayo hata siifahamu. Tuna ziwa rukwa karibu tu hapa, lakini karibu zaidi, tuna ziwa Tanganyika, lakini bado tunalima msimu mmoja tu wa mwaka, tena kwa kubahatisha mvua. Kweli serikali imeshindwa kutuletea maji kutoka ziwa Tanganyika tukalima mwaka mzima? Au hata imeshindwa kushusha bei vifaa vya umwagiliajia kama water pump na mipira ya kumwagilia ili tumudu japo kununua water pump tutumie chem chem na mito midogo iliyopo kumwagilia? Na mwenye nguvu ya kumwagilia hekari moja ya mahindi kwa kubeba maji kwenye keni? Kweli Binafsi, mimi kama STK ONE, sina kitu cha KUJIVUNIA KAMA MTANZANIA, kutokana na hali ya maisha ya kifukara niliyonayo na ya watu wanaonizunguka. SIJUI, MWANA JF MWENZANGU, NIAMBIE UNAJIVUNIA NINI KUWA MTZ?

  STK ONE, KATAVI.
   
 2. K

  K.Msese JF-Expert Member

  #2
  Sep 12, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 1,467
  Likes Received: 271
  Trophy Points: 180
  • Najivunia amani yetu inayotokana na uelewa mdogo wa watanzania juu ya haki zetu na kutokuwa na ujasiri wa kuzidai.
  • Najivunia kuwa mapato yoote tunayopata, yanaishia kununua mashangingi v8, safari za viongozi, warsha na makongamano.
  • Najivunia mwizi wa kuku anafungwa miaka mingi, mwizi wa mabilioni anaundiwa tume au anaombwa kwa upole arudishe alichoiba.
  • Najivunia Tanzania nchi yangu, kwakuwa Ukiwa kiongozi Tanzania, inalipa kuliko biashara yeyote duniani.
  • Ni nchi ya kifalme, madaraka kwa kupeana..Nnauye, Kawawa, Mwinyi, Karume, Nchimbi, Msuya, hadi vijukuu watapata vyeo.
  • Najuvunia TAKUKURU, ni ka-mbwa koko, kanakula tu vifaranga vyakuku vyenye mdondo na kufyata mkia kwa wakubwa.
  • Najivunia nchi yangu kwakua intelijensia, haina mpango na rasilimali za taifa wala mikataba mibovu......chezea kuchakachua kura weye...utaijua intelijensia.
  • Najivunia nchi yangu ni SHAMBA la BIBI, natamani niwe mzungu nipewe kitalu au mgodi......nshaanza kutumia karolait.
  • Vijana maskani wanasemaga....."mwanaaaa....bora vita ije......kila mtu achukue chake.....maana huu ujinga, wachache wanajirundikia...!"

  Kibanga Msese
   
 3. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #3
  Sep 12, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
 4. STK ONE

  STK ONE JF-Expert Member

  #4
  Sep 12, 2012
  Joined: Dec 31, 2011
  Messages: 628
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Very good, Kweli unayo mengi ya kujivunia, nashngaa kwa nini sikuyaona yote hayo. Hongera sana.
   
 5. h

  hippocratessocrates JF-Expert Member

  #5
  Sep 12, 2012
  Joined: Jul 1, 2012
  Messages: 3,612
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Mkuu, umeni_pre-empty..good hit sir, well said.
   
 6. Muke Ya Muzungu

  Muke Ya Muzungu JF-Expert Member

  #6
  Sep 12, 2012
  Joined: Jun 17, 2009
  Messages: 3,451
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  ~najivunia rais ombaomba
  ~najivunia rais mzururaji
  ~najivunia rais anayeongoza nchi kifamilia zaidi
   
 7. Kaitampunu

  Kaitampunu JF-Expert Member

  #7
  Sep 12, 2012
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 1,681
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Najivunia kuwa na rais dhaifu.
   
 8. atubariki

  atubariki JF-Expert Member

  #8
  Sep 12, 2012
  Joined: Oct 26, 2011
  Messages: 225
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Najivunia kuwa na viongozi mafisadi na wabadhirifu wa mali ya uma ambao hawana huruma
   
 9. STK ONE

  STK ONE JF-Expert Member

  #9
  Sep 12, 2012
  Joined: Dec 31, 2011
  Messages: 628
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nimesoma hiyo thread yako na wachangiaji. Zomba mbona hakuna uhusiano wa thread yako na hii ya sasa? Usitake kuleata siasa kwenye mambo ya msingi yanayowagusa watz wengi hasa masikini. Usilete Uccm wako hapa. Jaribu kuhusianisha mambo kabla ya kuchangia, after all unaweza kusoma na kupotezea tu.
   
 10. STK ONE

  STK ONE JF-Expert Member

  #10
  Sep 12, 2012
  Joined: Dec 31, 2011
  Messages: 628
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hongera. Lakini ungeweza kuchangia more positively ili wengi ambao hawawezi kuchangia wanufaike na mchango wako. Anyway, pengine ndiyo level yako ya u great thinker.
   
 11. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #11
  Sep 12, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Upo kwenye jukwaa la siasa na umetuuliza t"unajivunia" nini kama Mtanzania"?

  Mimi najivunia ubaguzi au maslahi ya kisiasa kinapotokea kifo cha mwanaharakati. Hukupenda nnachojivunia?
   
 12. STK ONE

  STK ONE JF-Expert Member

  #12
  Sep 12, 2012
  Joined: Dec 31, 2011
  Messages: 628
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  How? Can you explan more? Wengi hawaelewi vipi unajivunia kuwa na Rais Dhaifu kama JMK? Eleza kama great thinker.
   
 13. STK ONE

  STK ONE JF-Expert Member

  #13
  Sep 12, 2012
  Joined: Dec 31, 2011
  Messages: 628
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Siyo kwamba sikupenda unachojivunia, but I didn't see the clear relationship ya thread inayojadiliwa na link uliyonipa. Ungeweza kueleza mengi zaidi ambayo unajivunia kuwa Mtz ili ambao hawana access ya kuchangia wanufaike, japo wewe ni Kada wa ccm, lakini unajivunia nini kama MTz mbali na kuwa mwana ccm?
   
 14. Kaitampunu

  Kaitampunu JF-Expert Member

  #14
  Sep 12, 2012
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 1,681
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Umemjuaje?
   
 15. muonamambo

  muonamambo JF-Expert Member

  #15
  Sep 12, 2012
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 769
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 45
  Najivunia riz 1 kuendesha nchi wakati JK anatalii
   
 16. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #16
  Sep 12, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Wewe ulichokionesha unachojivunia ni nini? mimi najivunia ubaguzi au maslahi ya kisiasa vinapotokea vifo vya wanaharakati.
   
 17. STK ONE

  STK ONE JF-Expert Member

  #17
  Sep 12, 2012
  Joined: Dec 31, 2011
  Messages: 628
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nimemjuaje nani? JMK kuwa ni rais dhaifu? Sasa ki uhalisia, udhaifu wa rais ni jambo la mtu mzima kujivunia? Mbona mnaharibu maana ya GREAT THINKERS?
   
 18. STK ONE

  STK ONE JF-Expert Member

  #18
  Sep 12, 2012
  Joined: Dec 31, 2011
  Messages: 628
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Zomba unaonesha umesoma tu heading ukaanza kuchangia. Nilijua kuwa thread ni ndefu ndiyo maana nika bold na kukuza maandishi ili yasichoshe kusoma. Ungelisoma yote, usingeliuliza najivunia nini? Jaribu kusoma japo aya ya mwisho utapata jibu la swali lako.
   
 19. STK ONE

  STK ONE JF-Expert Member

  #19
  Sep 12, 2012
  Joined: Dec 31, 2011
  Messages: 628
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mbona avatar yako tofauti na contents ambazo unaandika? Usiwe vuguvugu, kuwa moto au baridi.
   
 20. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #20
  Sep 12, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Nimesoma na nimeona unajiyovunia, nami najivunia yangu, moja wapo nililokuwekea. Jee, unataka nami nijivunie yako? mimi sitaki ujivunie langu.
   
Loading...