Unajivunia nini kuwa Mtanzania?

Yaani nikiwa nje na ndani ya Tanzania najivunia kila kitu! Ata kwa mabaya watakayosema kuhusu nchi hiii bado najivunia!!! Hamna nchi isiyokosa kasoro na tumshukuru Mungu kasoro zetu ni ndogo sana. Sijaona bado cha kunifanya nione aibu kuhusu Tanzania.
NAKUPENDA TANZANIA!!!!
 
Ninaona aibu nchi ya kusadikika,nchi ya viwanda,nchi ambayo katiba hukanyagwa na kutoheshimika,nchi isiyo na mipaka ya kazi kama Mkuu wa Mkoa kutoa kauli kama ni ya nchi nzima,nchi ambayo watu wake wana maswahiba ya ujinga uliopitiliza,umasikini uliokithiri,maradhi tena ya ajabu,ufisadi na maswahiba kibao toka nchi ipate uhuru watu wengi hawana uhakika wa mlo mmoja wa siku zaidi ya miaka 55 ya uhuru.
Ninapata aibu kwa Viongozi na Watu waliotufikisha hapa tulipo ambapo hata mlo mmoja wa siku ni msamiati kwa wengi wao watu au viongozi hao hulindwa na kuogopewa sana.
Acha tu maana ninapata machungu sana nikifikiria nchi yangu mambo yanavyokwenda kimsobemsobe...
 
Usijali mkuu hii ndiyo Tanzania yetu.
 
1.Kusikia kuwa tutaanza tena viwanda baada ya kuua vile vya mwanzo. Najiuliza, walioviua wameshahama nchi?
2.Kuona watu wakipeana vyeo kichama, sisi tusio na vyama, tufie mbali?? Jamani sisi sote nchi hii ni yetu. Unafiki tuache. Miiko ya chama inasema Sintambagua mtu awaye yote. Je, huu sio ubaguzi? Mmeniuliza msiseme ni mchochezi
 
Nikiwa nje ya nchi huwa naona aibu kujitambulisha ni mtz kwani twajulikana ni watu duni wasio na akili ya kutumia rasilimali zetu kututajirisha, wakenya wanatubeza kwa kutuita nduguze..
 
Bora paka aliyezaliwa ulaya kuliko binadamu wa Tanzania!
Wengi hawatakuelewa...but huu ndo ukweli...mfano mdogo wakenya tena wanakwaya walipata ajali ya bus binafsi, walifuatwa kwa ndege toka kenya...lakini watz hatuna thamani mbele ya watawala wetu hasa wakati wa majanga hakuna wa kujali zaidi ya kula vichapo mkiandamana kudai haki..cc tetemeko bukoba
 
Tanzania Tanzania, nakupenda Tanzania, jina lako ni tamu sana, nilalapo nakuota wewe. Sijawahi kujutia kuzaliwa Tanzania najivunia kuwa mtanzania. najivunia kila kitu katika nchi yangu zaidi zaidi amani. I love my beautiful Tanzania
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom