Unajisikiaje unaposababisha vifo vya watu kwa ajali na kufanikiwa kukimbia?

george aloyce

JF-Expert Member
Aug 22, 2017
1,279
1,942
Sawa inatokea umesababisha ajali umeua binadamu mwenzako umekimbia kukwepa kwenda jela na umebahatika hakuna aliyekuona. Huko nyumbani kwako utaishije? Unaingia mtandaoni unaona maelfu ya watu wanalia kwa kuondokewa na mpendwa wao ambaye wewe ndio chanzo.

Huwezi kuwa na amani, utaishi uraiani lakini bado nafsi na roho yako vitaishi maisha ya jela, kiufupi ni utateseka maisha yako yote. Wapo watu wengi wa aina hii mtaani tunaishi nao, watu ambao walisababisha ajali walipoona wameua wakakimbia na mpaka leo hawajagundulika, wapo wengi mioyo yao imebeba hukumu nzito zinawatafuna.

Tujitahidi kuwa na hofu ya Mungu, ajali haina kinga lakini tunapojaaliwa kumiliki usafiri wetu au tunapoendesha jitahidini kuwa makini, usijali roho yako tu beba na roho za watu wengine, inaumiza sana kuondoa uhai wa binadamu mwenzako ambaye ni tegemezi kwa familia yake.
 
Mara kwa mara utakuwa ni mtu wa kuhisi hatia,, in short utakuwa umejifunga mwenyewe kifungo kibaya sana kuliko hata kupelekwa magereza 🤒😎
 
Sawa inatokea umesababisha ajali umeua binadamu mwenzako umekimbia kukwepa kwenda jela na umebahatika hakuna aliyekuona. Huko nyumbani kwako utaishije? unaingia mtandaoni unaona maelfu ya watu wanalia kwa kuondokewa na mpendwa wao ambaye wewe ndio chanzo.

Huwezi kuwa na amani, utaishi uraiani lakini bado nafsi na roho yako vitaishi maisha ya jela, kiufupi ni utateseka maisha yako yote. Wapo watu wengi wa aina hii mtaani tunaishi nao, watu ambao walisababisha ajali walipoona wameua wakakimbia na mpaka leo hawajagundulika, wapo wengi mioyo yao imebeba hukumu nzito zinawatafuna.

Tujitahidi kuwa na hofu ya Mungu, ajali haina kinga lakini tunapojaaliwa kumiliki usafiri wetu au tunapoendesha jitahidini kuwa makini, usijali roho yako tu beba na roho za watu wengine, inaumiza sana kuondoa uhai wa binadamu mwenzako ambaye ni tegemezi kwa familia yake.
Je, unajua kazi hasa zinazofanywa na wale jamaa wa 'Noah nyeusi'? Ungekuwa unazijua kazi zao Wala hata usingejisumbua kuandika uzi huu hapa Jf. Dunia hii no sehemu mbaya sana, Kuna watu ni wabaya kumzidi hata shetani. Jaribu kutafiti kidogo kuhusu kinachoitwa 'staged accidents' au 'targeted crimes,' nafikiri utaweza kujifunza kitu fulani.
 
Hua na mwisho mbaya sana
 
This is Tanzania,
Kuongea ni rahisi ila subir yakukute.

Siku jioni natoka kazini
Nakutana na wanafunz wanatoka twishen,Nyuma mwanafunz mmoja kadandia spea tairi, mi naendesha ata sijui kinachoendelea.

msamalia kapiga kelele Kuna Mtoto nyuma, ghafla nikashika breki, Mtoto yule kadondoka chini, kainuka katika kukimbia kaingia barabara kubwa, imekuja Noah imempitia Mtoto yule kafariki pale pale. Noah haikusimama imeondoka zake.

Mimi niliebaki pale NILIJUTIA SANA MAAMUZI YANGU TANGU SIKU ILE.
 
Hawana maisha malefu
Maisha marefu ni miaka mingapi? Sitetei mauaji ila nakukumbusha tu kuwa hii dunia si kila binadamu ana roho nyepesi. Watu wana roho ngumu wanaweza kula figo na maini yako huku watu wako wa karibu wanashuhudia na wakaishi kama hakuna lililotokea.
 
Back
Top Bottom