Unaiumiza jamii unapovunja ndoa

Unaiumiza jamii unapovunja ndoa

mmisionary

New Member
Joined
Dec 12, 2019
Posts
2
Reaction score
4
Kimsingi NDOA ni takatifu. Ulipofunga ndoa kanisani ulidhibitisha yafatayo:

- Uliilinda imani. Unapovunja ni kinyume chake.
- Ulipofunga ndoa ulilieshimu kanisa. Unapovunja ni kinyume chake.
- Ulipofunga ndoa ulimuheshimu Mungu. Unapovunja ni kinyume chake.

Unapovunja ndoa unaumiza watu wengi sana. Taarifa ya Martha kuvunja ndoa imemliza mke wa mtu siku mbili. Ni shabiki wake na ndye alimfanya akabadili dini na kuokoka. Alipitia shida hadi kuokoka ila alitaka aishi kama yeye kwa kila kitu. Japo alifanikiwa kuokoka na pia kubadili dini. Martha ameyumbisha watu katika imani.

Ni vizuri mtu kuitambua nafasi yako katika jamii. Kuna watu mtadaiwa kuhusu wale mliowalea ktk Kristo. Martha anapaswa kutambua analea watu asiowafahamu. Naamini atadaiwa. Ila akiacha kiburi, akakomesha majivuno ya nafsi yake na roho, akomeshe kiburi cha account yake ya benki amruhusu roho mtakatifu amfinyange na kumuumbia roho mpya yenye upendo na unyenyekevu, akanyenyekea mbele za bwana Mungu, na kunyenyekea mbele za mumewe na amsihi Mungu ampe busara.

Hakika anayo nafasi tena kuanza upya maisha FURAHA tele na mumewe. Kimsingi, wanawake wanapaswa kuelewa unyenyekevu kwa mumeo ndio ticket ya maisha. Kwa unyenyekevu wanawake ndio walimhudumia yesu. Ndio hulitunza kanisa. Kwa unyenyekevu huitunza familia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ngoja Martha Mwaipaja aje atupe ushuhuda hapa maana ametangaza kuwa now yupo single
 
Ndoa ilikuwa ya Martha. Martha anajua magumu aliyopitia. Hii ya kumhukumu ameacha ndoa ni kinyume na maandiko ni kudanganya watu. Hebu tupeni pumzi ninyi mnaojiita watumishi wa Mungu.
Martha alikurupuka kuolewa na yule bwana yule bwana alitaka kupata umaarufu kwa kupitia uimbaji wa Martha. Martha alikuwa innocent girl hakujua lengo la yule bwana. Mapendo hayakutangulia yaliyotangulia ni kuwa maarufu sasa matokeo yake ni haya.

Hapa wa kmhurumia ni Martha hata ukimuangalia anaumia sana moyoni anajilaumu anajihukumu so wale by the name of watumishi wa Mungu msituchoshe. Acheni mtoto wa wenyewe
 
Kwani wakati mnakula kiapo kuwa umekubali kuwanaye kwenyeshida na raha ulikuwa unawaza nn?
 
Back
Top Bottom