Uhakika Bro
JF-Expert Member
- Mar 29, 2022
- 2,398
- 3,071
Hivi paradiso italetwa? Au tutaileteleza wenyewe hapa duniani?
Watu wenye kusali hutusisitizia kila mara kwamba paradiso ni mahala pazuri saana π
Ni mahali ambapo kuna miti na maua mazuri ya kupendeza ππΊπΈππππͺ»πΉ
Kuna wanyama wazuri wasioumana wala kuumauma watu ovyo πππ¦ππ¦πΆπ¦π¦π¦
Yaani ni bustani moja nzuri sana watu wanajilia tu matunda ππππππ π«πππ na mito inaturirisha maji kila wakati.
Sasaa nimeanza kufikiria kwamba hivii kama tukiweka mikakati, hatuwezi kweli kujaribu kuikaribia hiyo hali?
Tunabadili tu tabia ndogondogo mfano;
1.Badala ya ukuta tunaweka fensi ya miba ile ya maua
2. Badala ya paving unaweka ukoka hasa zile sehemu ambazo sio njia
3. Badala ya kujaza jumba kiwanja chote. Unaweka tu nyumba ya kiasi sehemu inayobaki unaweka miti na matunda na maua.
Ukiitazama picha utagundua kuwa kuna maendeleo makubwa sana hapo, na bado pana hali nzuri tu ya kijijini. Tena kama ni picha ya kweli utakuta hapo wanaishi matajiri tu. Sema kitu kimoja hapo sijui wamewekeana sheria hakuna kumiliki gari yaani wao ni mwendo wa baiskeli tu!π€. Duh nao wamepitiliza asee. Ila fresh tu au we unaonaje?
Ukiweka mazingira ya nyumbani kwako hivyo utashangaa ndege na vipepeo wanajaa tu.
Na tukitaka kila familia iweze ku'afford' (kumudu bhanaπ€£) kuweka mazingira katika hali kama hiyo hapo inabidi kitu kinaitwa maji kiwe ni BWERERE kabisa. Yaaani nchi isambaze na kutiririsha maji kila kona ya nchi na vijiji. Vyanzo vya maji vipo tushindwe miundombinu tu na nia labda.
Eeh hali safi ya hewa ukirudi nyumbani unapumzika kweli.Kwani jamani ndugu zangu, kujenga majumba na mabarabaraποΈπππ€πποΈπ kila sehemu ndio maendeleo? Kwa nini tusije na tafsiri ya kiafrika ya maendeleo na sie?
Unafikiri ni kwa nini UNICEF wanachukulia maeneo kama Ngorongoro kuwa ni Urithi wa dunia. Si kutokana na uasili wake?
Sikia na hii;
Tena kutokana na udadisi na kufikiria. Ninadhani katika mazingira hayo, watoto wanaokulia humo wanakuwa na akili sana. Kwa nini? E eeh kwa sababu wakiwa hapo akili inakuwa imetulia saafi kabisa hivyo wanajihisi amani na wanakuwa wadadisi. Na udadisi ndio akili ujue. Masala ni Kulangwa.