Hebu wekea nyama unaonekana una mengi unayajua
Mara kwa mara watu wapole, na waliotayari kushuka wamekuwa wenye hisia za kinyonge na kutengwa, wakijihisi kutokuwa salama wakati mwingi. Kujijali, kujipenda na kujithamini kwa watu hawa siyo kwa kudumu, bali kunakuwa na nyakati za kuyumbayumba kutokana na mazingira. Hawa siyo watu wenye ujasiri ndani yao wenyewe na hata katika vile wavifanyavyo.
Mara mtu wa kundi hili anapokutana na mtu mjeuri na mtukutu, hofu na ujasiri wake hupungua sana, na anaweza kukubali kupingwa hata kama alikuwa ana haki. Kwa sababu mara nyingi watu wa jinsi hii wanajua kuwa kwa upole wao watu wengi wamekuwa wakiwatumia na kuwachezea, hii imewafanya wawe ni watu wenye vihasira vya mara kwa mara.
Kwa sababu wameunganishwa na hisia zao zaidi, ni rahisi wao kuzielezea hisia zao kwa mtu mwingine, hata kama hisia zao ni za kujutia kile walicho kifanya wenyewe. Mara nyingi husikia amani kwa yale wanayofanya au kuyaamua.
Ingawa mara nyingine mambo huwaendela tofauti na walivyopanga, watu hawa hufahamu kuwa hawanabudi kukubali kosa au na kuwa tayari kujifunza kutokana na yale makosa.
Mambo yanapowaendea vema hupenda kujisifia na kujiona walio juu. Mara nyingine misimamo yao huwashawishi na kuwavutia wengine watazame kama wao.
Muda mwingine huwa na hasira kali, lakini wewe sio rahisi kuziona. Huwa na jazba za kuanzisha vurugu na akianzisha ugomvi na ukaleta madhara, baadae hujutia na kuja kujishusha kwako