Herbalist Dr MziziMkavu
Platinum Member
- Feb 3, 2009
- 43,114
- 34,957
Zungumza na watu wengi waliofanikiwa ndani na nje ya Tanzania, watakwambia kwamba mojawapo ya siri za kufanikiwa katika maisha ni kuwa na mikakati kwa vitendo; Ndiyo kusema kwamba kama hukuwa na malengo, unapaswa kuyapangilia sasa kisha kuanza kuangalia namna gani unaweza kufanya ili kutimiza malengo yako.
MSINGI wa kuwa na maisha yenye mafanikio ni pamoja na kuhakikisha unakuwa na malengo; Je, wewe kuna malengo yoyote uliyoyaandika kwamba unataka kuyatekeleza kwa mwaka 2013? Kama huna, hilo ni kosa kubwa.

Malengo yanaweza kuwa ni ya aina tofauti kulingana na unavyotaka, kwa mfano inawezekana unataka kuwa na biashara, kusoma zaidi, kujenga nyumba, kupata kazi sehemu nzuri zaidi; kufanya kazi sehemu kwa sababu umezoeleka badala ya kujali unachokipata, ni dalili kwamba akili yako haiko sawa.
Mwenye akili timamu haishi kwa sababu ya kumfurahisha mwajiri, bali anajiangalia mwenyewe pia anapata nini; Ndugu zangu maisha tunayoishi ni mafupi, ni lazima kwa kila tunachokifanya kuangalia tunafanya kwa masilahi au tunapoteza muda.
Je, wewe ukoje? Pata muda kujitafakari; Kuna watu kwa mfano wako wanafanya kazi kwenye ofisi zenye majina makubwa, wanakubali kuwapo kwenye ofisi hizo, siyo kwa sababu zinawalipa, bali kwa sababu ya sifa, kwamba yuko kwenye ofisi fulani ya Serikali, yuko benki au ofisi nyingine yoyote.
Tunapoingia kwenye mwaka mpya, ni lazima kutafakari kwa umakini mkubwa juu ya suala zima la kipato; Wengi wanakosea, wanaishi bila kupata muda wa kujitafakari. Angalia je, kipato unachopata kwa siku kinazidi Sh10,000? Ni rahisi kujua, chukua mshahara au kipato chako gawanya kwa siku 28 yaani mwezi, ona unapata shilingi ngapi? Kama unapata chini ya hiyo maana yake unakosea hasa kama ni mtu ambaye labda umesoma. Kwa sababu hata wabeba mikokoteni au waendesha bodaboda, wapo wenye kupata zaidi ya fedha hizi, inakuwaje wewe uliye na Stashahada au Shahada na kuendelea unapata kiasi hiki?
Msingi wa makala haya ni kukumbushana kwamba huwezi kufanikiwa kama hutathubutu kufanya mambo fulani yenye kukusaidia kwenda mbele, kama vile kubuni miradi hata kama ni midogo midogo.
Kusoma sana au kidogo, kuwa na rafiki waliofanikiwa au wasiofanikiwa, kwenda nje ya nchi au la, au kuzaliwa familia maskini au tajiri, bado sio tiketi ya kukufanya uwe na maisha bora.Kuna wengi wamekuwa wakijisifia kwa sababu ya umaarufu wao, kwa sababu walikwenda nje, hilo sawa, lakini maisha yako yanafafanaje? Maana kuna wengine wanachapwa bakora na maisha, halafu bado anajisifia aaah bwana nilikuwa Russia, aaah nilikuwa Sweden, kwa hiyo nini kama ulikuwaje nje wakati unapigwa na maisha? Msingi wa kuwa na maisha bora, ni kuangalia kwa umakini mkubwa staili ya maisha yako.
Unakuta kuna wanaume wanahangaika na wanawake, wengine wanafanya ngono kama dozi, wanawake kibao; wengine wakipata fedha zinamuua kwa kuhangaika zaidi na wanawake; huu ni ujinga, inavyotakiwa ni kwamba baada ya kuwa na fedha au hata kabla, ni wakati wa kuimarisha uhusiano wako katika ndoa. Kama ni ngono wengine wamefanya sana, umepata nini tangu uanze kufanya ngono na wanaume au wanawake wengi?
Kama ni wanaume wamedharau nyumba zao kwa sababu ya wanawake wa nje, watoto wao wameshindwa kuwasomesha, sababu labda fedha wamemalizia kuhonga; ndugu yangu vipi umelogwa? Somesha watoto wako ili angalau wawe na maisha mazuri, ukiwa mzee huenda wakakusaidia, hata wakiwa na roho mbaya, watasemwa na watu watakusaidia angalau kidogo, ni ngumu kahaba unayempapatikia akakujua utakapopigika kimaisha.
Msingi wa kufanikiwa ni kuthubutu kufanya jambo fulani, kwa mfano kufungua mradi na mambo mengine kama haya. Kuna watu kwa mfano unaweza kuona anakata tamaa kwa sababu labda amezaliwa katika familia maskini, kitu ambacho siyo sahihi. Usiishi tu ili mradi siku zinakwenda mbele, ishi kwa malengo. Kwa chochote unachokifanya, kifanye baada ya kutafakari na kuangalia faida au hasara yake.
Ugumu wa Maisha ni Kipimo cha Akili; Kitaalam kuna knowledge (elimu au ujuzi) na wisdom (namna ya kuihamisha elimu au ujuzi kwenda kwenye vitendo); Kuwa na knowledge bila wisdom ni sawa na kupoteza muda bure darasani. Jifunze namna ya kuhamisha ujuzi wako kwenye vitendo kwa kuthubutu kufanya mambo, kufungua miradi na hata kusoma zaidi au kuishi kwa kufanya mazuri, badala ya ulevi, ngono nk.