Unaikumbuka soda ya Double Cola?

Unaikumbuka soda ya Double Cola?

Malyenge

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2012
Posts
6,658
Reaction score
3,662
Wakuu mnaikumbuka soda iliyokuwa ikizalishwa na kiwanda kimoja huko Mwanza iitwayo DOUBLE COLA?

Nakumbuka soda hiyo ilikuwa nzuri sana kiasi kwamba ilitishia soko la soda zingine zenye majina makubwa. Mafisadi watakuwa walikifanyia fitna ili waendelee kutunyonya na soda zao zinazotoa harufu mdomoni na ukakasi kibao.

images
images

images
images

images
images

images
$_35.JPG

images


Kazi kwako mkuu!
 
naikumbuka hiyo soda ilikuwa nzuri nilibahatika kuinywa kwa sababu baba yake na rafiki yangu alikuwa meneja wa hicho kiwanda
 
Mkuu enzi hizo nimeuza sana hizo soda Mwanza eneo la ghana kwenye stendi ya express
 
Mkuu enzi hizo nimeuza sana hizo soda Mwanza eneo la ghana kwenye stendi ya express

Mkuu huna picha ya chupa yake tuitundike humu? Itapendeza sana na itatukumbusha mbali sana....
 
Wale wa Tanga raha helto nimeimis sana hivi bado ipo?
 
Wala sio ufisadi, ni kuridhika mapema kwa Wahindi walikuwa wakimilki hicho kiwanda. Walikuwa na monopoly ya aina yake miaka ya 80, nakumbuka malori ya akina Paul Ngwani na Chacha nini cjui walikuwa yanapanga foleni pale kiwandani Arusha kwa hata wiki nzima kusubiria mzigo.

Shida ilianza Mengi alipoanzisha Bonite bottlers, akajaza Coke sokoni watu wakawa hawanunui tena Double cola, Wahindi baadae wakawauzia Pepsi kiwanda kikageuzwa godown.

Huo ndio ukawa mwisho wa Double cola, ilikuwa inatesa sana wakati wa kipaimara na Xmas wakasahau kujiendeleza kibiashara
 
Wala sio ufisadi, ni kuridhika mapema kwa Wahindi walikuwa wakimilki hicho kiwanda. Walikuwa na monopoly ya aina yake miaka ya 80, nakumbuka malori ya akina Paul Ngwani na Chacha nini cjui walikuwa yanapanga foleni pale kiwandani Arusha kwa hata wiki nzima kusubiria mzigo.
Shida ilianza Mengi alipoanzisha Bonite bottlers, akajaza Coke sokoni watu wakawa hawanunui tena Double cola, Wahindi baadae wakawauzia Pepsi kiwanda kikageuzwa godown. Huo ndio ukawa mwisho wa Double cola, ilikuwa inatesa sana wakati wa kipaimara na Xmas wakasahau kujiendeleza kibiashara
Uko vizuri kiongozi, umefafanua vizuri sana..
 
Hii hapa

attachment.php
 

Attachments

  • 1440704940482.jpg
    1440704940482.jpg
    22.5 KB · Views: 489
Duh Double cola umenikumbusha Tabora miaka ya '85 wakati huo Railway wameshika hatamu hasa!
 
Wakuu mnaikumbuka soda iliyokuwa ikizalishwa na kiwanda kimoja huko Mwanza iitwayo DOUBLE COLA? Nakumbuka soda hiyo ilikuwa nzuri sana kiasi kwamba ilitishia soko la soda zingine zenye majina makubwa. Mafisadi watakuwa walikifanyia fitna ili waendelee kutunyonya na soda zao zinazotoa harufu mdomoni na ukakasi kibao.......
Kama kuna mwenye chupa ya soda hiyo aitundike humu, itapendeza sana.....!

Mbona hiyo soda duniani huko ipo?

 
Back
Top Bottom