KV LONDON
JF-Expert Member
- Jul 18, 2012
- 903
- 241
Ee bwana niliachwa na binti mmoja tulikuwa tunapendana sana, tulikutana shule ya sekondari majengo iliyopo Moshi mjini, yani tulipendana sana ila yeye alikuwa kidato cha tatu na mimi kidato cha nne. Tulikubaliana kutokuachana siku zote, nikamaliza kidato cha nne nikapangiwa kwenda kidato cha tano Kilosa boys Morogoro na yeye akabaki majengo kumalizia kidato cha nne. Akamaliza kidato cha nne na akarudi kidato cha tano palepale majengo.
Nikamaliza kidato cha sita na nikaomba kujiunga na kozi mbalimbali katika vyuo vikuu hapa nchini na kubahatika kupangiwa Makumira university Arusha kusoma education. Msichana wangu alipomaliza kidato cha sita na yeye akapangiwa kwenda kusoma chuo cha mzumbe Morogoro campus, wakati huo mimi nipo mwaka wa pili yeye ndo anaanza.
Vimbwenga vikaanza ukipiga simu haipokelewi, sms ndo kabisa hazijibiwi, serekali kupitia bodi ya mikopo ndo ikaloga kabisa ilipompa mkopo. Ukipiga simu anajidai yuko bize na vipindi hata saa nane za usiku. Siku moja nikamtext 'Do you still love me' akanijibu 'hivi unasoma kozi gani tena? Kana kwamba kasahau au hajui tena, nikamjibu si education mpenzi.
Nilichojibiwa nilikata tamaa. "siwezi kukupenda tena maana sijapanga kuolewa na mwalimu".Kisa yeye anasoma HRM (Human Resource Management) niliomba penzi lisivunjike mpaka button za simu zikaisha ila penzi likayoyoma kisa nasoma education, sitasahau asee. Sijui wengine mliachwaje au kuacha wapenzi wenu kwa sababu gani.