Unaikumbuka sababu ya kuachana na mpenzi wako?

KV LONDON

JF-Expert Member
Jul 18, 2012
903
241
Ee bwana niliachwa na binti mmoja tulikuwa tunapendana sana, tulikutana shule ya sekondari majengo iliyopo Moshi mjini, yani tulipendana sana ila yeye alikuwa kidato cha tatu na mimi kidato cha nne. Tulikubaliana kutokuachana siku zote, nikamaliza kidato cha nne nikapangiwa kwenda kidato cha tano Kilosa boys Morogoro na yeye akabaki majengo kumalizia kidato cha nne. Akamaliza kidato cha nne na akarudi kidato cha tano palepale majengo.

Nikamaliza kidato cha sita na nikaomba kujiunga na kozi mbalimbali katika vyuo vikuu hapa nchini na kubahatika kupangiwa Makumira university Arusha kusoma education. Msichana wangu alipomaliza kidato cha sita na yeye akapangiwa kwenda kusoma chuo cha mzumbe Morogoro campus, wakati huo mimi nipo mwaka wa pili yeye ndo anaanza.

Vimbwenga vikaanza ukipiga simu haipokelewi, sms ndo kabisa hazijibiwi, serekali kupitia bodi ya mikopo ndo ikaloga kabisa ilipompa mkopo. Ukipiga simu anajidai yuko bize na vipindi hata saa nane za usiku. Siku moja nikamtext 'Do you still love me' akanijibu 'hivi unasoma kozi gani tena? Kana kwamba kasahau au hajui tena, nikamjibu si education mpenzi.

Nilichojibiwa nilikata tamaa. "siwezi kukupenda tena maana sijapanga kuolewa na mwalimu".Kisa yeye anasoma HRM (Human Resource Management) niliomba penzi lisivunjike mpaka button za simu zikaisha ila penzi likayoyoma kisa nasoma education, sitasahau asee. Sijui wengine mliachwaje au kuacha wapenzi wenu kwa sababu gani.
 
Mkuu @KV.LONDONI, ILIKUWAJE BAADA YA KUKUACHA, JE HAJAWI KUKUTAFUTA? NA KAMA ALIOLEWA HAKUOLEWA NA MWALIMU KWELI?

Maana kawaida unachokidharau ndicho kinachokuangusha. Tupatie majibu basi ili nasi tuweze changia vizuri
 
Yani ndo nimeanza kazi mwaka huu, na yeye ndo anamaliza mwaka huu, ila juzi kanicheki anauliza nilipopangiwa sikumjibu
 
KV LONDON

Same story asee ila mm nilikuwa naye kidato kimoja,then chuo nikabaki dar yeye akapelekwa bukoba wiki mbili baadae simu haipigwi,nikipiga nipo bize ,wakat anakesha fb heeh mwishowe akafunguka et we mshamba sikutaki ofcourse sikubisha nilikubalii tu na ikawaga mwisho aseee ila nikajiuliza miaka 3 yote ya mapenzi yetu nilikuwa mshamba au nimeuanza leo huo ushamba, baadae nikajua kwann mshamba kumbe etiii kwa vile niliheshimu ubikira wake .....ikawa noma kuona fb jina alilokuwa ananiita anaitwa mjanja mwngne hv thanks now am good asee
 
Last edited by a moderator:
Mkuu @kv.London umefanya vizuri kabisa kutomjibu mjuhimu mchunie amalize chuo aingie mtaani aone palivo pagumu trust me atakutafuta kwa udi na uvumba, we komaa upige kazi utafute pesa utimize malengo yako

Hapo sawa mkuu, alogwe arudi atajuta
 
walimu tuna hali ngumu! hamtuachi tukapumua?

Pole sana mkuu, umesabbabisha nimecheka sana. Baadhi yenu hamjiamini tu, mnajidharau kwamba nyie ni waalimu na mnachukulia kwamba mnadharaulika.

Tatizo linaanzia kwenu kisha jamii nayo inachukulia hivyo kumbe sio,sasa walimu ndio wana soko maana wakimaliza masomo wana kazi tayari wakati wengine bado wanahangaika na kutafta kazi
 
nilitaka tu ucheke ila sithamini ualimu wangu kwa sababu una fursa ya ajira. Wakati nachagua ualimu miaka 13 iliyopita haukuwa na fursa ya ajira kama sasa na nilipata upinzani toka kwa familia na marafiki. Wao walitaka nikasome sheria kwa sababu ni taaluma inayoheshimika na yenye hela na nilikuwa na maksi zaidi ya zinazohitajika kusoma sheria (sijui kama kuna ukweli kwenye hela). Kazi yako ukiipenda hata waseme nini utabaki unawashangaa tu maana hawajui raha unayoipata kwa kuifanya.
 
Sitosahau ewe kiumbe, tuliachana kisa nmekuambia naimba kwaya mda wa usiku. Saa mbili mpaka saa nne, niliporomoshewa matusi ambayo sitaki hata kuyakumbuka maana!. Wanaume tuna kazi sana! all the best popote ulipo

Huyo ni mfuasi wa satan
 
nilitaka tu ucheke ila sithamini ualimu wangu kwa sababu una fursa ya ajira. Wakati nachagua ualimu miaka 13 iliyopita haukuwa na fursa ya ajira kama sasa na nilipata upinzani toka kwa familia na marafiki. Wao walitaka nikasome sheria kwa sababu ni taaluma inayoheshimika na yenye hela na nilikuwa na maksi zaidi ya zinazohitajika kusoma sheria (sijui kama kuna ukweli kwenye hela). Kazi yako ukiipenda hata waseme nini utabaki unawashangaa tu maana hawajui raha unayoipata kwa kuifanya.

Exactly
 
Ee bwana niliachwa na binti mmoja tulikuwa tunapendana sana, tulikutana shule ya sekondari majengo iliyopo Moshi mjini, yani tulipendana sana ila yeye alikuwa kidato cha tatu na mimi kidato cha nne. Tulikubaliana kutokuachana siku zote, nikamaliza kidato cha nne nikapangiwa kwenda kidato cha tano Kilosa boys Morogoro na yeye akabaki majengo kumalizia kidato cha nne. Akamaliza kidato cha nne na akarudi kidato cha tano palepale majengo.

Nikamaliza kidato cha sita na nikaomba kujiunga na kozi mbalimbali katika vyuo vikuu hapa nchini na kubahatika kupangiwa Makumira university Arusha kusoma education. Msichana wangu alipomaliza kidato cha sita na yeye akapangiwa kwenda kusoma chuo cha mzumbe Morogoro campus, wakati huo mimi nipo mwaka wa pili yeye ndo anaanza.

Vimbwenga vikaanza ukipiga simu haipokelewi, sms ndo kabisa hazijibiwi, serekali kupitia bodi ya mikopo ndo ikaloga kabisa ilipompa mkopo. Ukipiga simu anajidai yuko bize na vipindi hata saa nane za usiku. Siku moja nikamtext 'Do you still love me' akanijibu 'hivi unasoma kozi gani tena? Kana kwamba kasahau au hajui tena, nikamjibu si education mpenzi.

Nilichojibiwa nilikata tamaa. "siwezi kukupenda tena maana sijapanga kuolewa na mwalimu".Kisa yeye anasoma HRM (Human Resource Management) niliomba penzi lisivunjike mpaka button za simu zikaisha ila penzi likayoyoma kisa nasoma education, sitasahau asee. Sijui wengine mliachwaje au kuacha wapenzi wenu kwa sababu gani.

Pole sana
 
Back
Top Bottom