HorsePower
JF-Expert Member
- Aug 22, 2008
- 3,612
- 2,566
Jana kupitia ITV, nilisikia ushuhuda wa dada mmoja kwa jina la Zainabu kama sijakosea ambaye alikuwa anaishi na mchumba wake Mwanajeshi aitwa Hassan, huko Tanga na kuhamia Dar. Baada ya kusumbuliwa na matatizo ya kiafya kwa muda, walienda kupima na huyo dada kugundulika kuwa na Virusi vinavyosababisha UKIMWI wakati mumewe alikuwa safi.
Kwa upendo mwingi, kaka yule aliamua kufunga ndoa na mchumba wake huyo mwenye HIV, na Mungu aliwabariki mwaka jana wamepata mtoto asiye na maambukizi baada ya kufuata ushauri nasaha na kupima.
Swali langu: Ungekuwa wewe ni mume/mke na huna HIV unapata mchumba mwenye HIV, utakuwa tayari kufanya maamuzi ya kuoa/kuolewa kama alivyofanya mwanajeshi Hassan? Tafadhali nipe maoni yako!
Point to take: Tusiwanyanyapae wenye HIV na UKIMWI, kama jamii, tuna uwezo wa kuishi nao bila matatizo yoyote endapo tutawapa ushirikiano wa kutosha na kuondoa dhana ya ubaguzi na hofu ndani ya mioyo yetu.
Wenu,