Unahitaji Moyo wa Chuma kufikia maamuzi haya .....

HorsePower

JF-Expert Member
Aug 22, 2008
3,612
2,565
Jana kupitia ITV, nilisikia ushuhuda wa dada mmoja kwa jina la Zainabu kama sijakosea ambaye alikuwa anaishi na mchumba wake Mwanajeshi aitwa Hassan, huko Tanga na kuhamia Dar. Baada ya kusumbuliwa na matatizo ya kiafya kwa muda, walienda kupima na huyo dada kugundulika kuwa na Virusi vinavyosababisha UKIMWI wakati mumewe alikuwa safi.

Kwa upendo mwingi, kaka yule aliamua kufunga ndoa na mchumba wake huyo mwenye HIV, na Mungu aliwabariki mwaka jana wamepata mtoto asiye na maambukizi baada ya kufuata ushauri nasaha na kupima.

Swali langu: Ungekuwa wewe ni mume/mke na huna HIV unapata mchumba mwenye HIV, utakuwa tayari kufanya maamuzi ya kuoa/kuolewa kama alivyofanya mwanajeshi Hassan? Tafadhali nipe maoni yako!

Point to take: Tusiwanyanyapae wenye HIV na UKIMWI, kama jamii, tuna uwezo wa kuishi nao bila matatizo yoyote endapo tutawapa ushirikiano wa kutosha na kuondoa dhana ya ubaguzi na hofu ndani ya mioyo yetu.


Wenu,
HorsePower
 
Hassan ni mjeshi kwa hiyo tabia za mijeshi ujue kifo kiko mkononi.Ujasiri huo kwa raia ni vigumu.Jeshi wanabeba bomu mfukoni wewe na mimi hata kuliona tu kwa kujua ni bomu ni mbio!Kuishi na mwathirika na kuzaa nae huku ukijua ana virusi si tu ujasiri ni uendawazimu usiopimika.
 
Mimi siowi hata siku moja, sababu ukifa unakuwa kama wale wapalestin wano jirupua...ni watu wa motoni tu.

Sitaki kujiua na ngojea Malaika mtoa roho siku yangu ikifika atoe roho yangu, sababu kapewa kazi na Mungu.

Ukichukua uamuzi wa kuowa mwanamke amabaye unajua ana HIV, ni kama vile una commit suicide...kitu ambacho Mungu hakipendi na anaye fanya hivyo akifa kwa aids, haendi peponi hata siku moja.
 
Nimeshawahi kutibu couple ya aina hii (discordant couple), kwa kweli zipo nyingi...na mara nyingi ni mwanamke anakuwa HIV +ve na mwanaume ni -ve. Na mara nyingi pia wanaume huwa wanabaki na wanawake zao japo wengine huwa hawataki kushiriki nao tendo la ndoa.

Kuna couple moja niliwahi kuitibu nao walikuwa wachumba mwanamke akawa +ve na mwanaume -ve, wakaoana, lakini yule mwanaume hakuwa anasikiliza ushauri wetu wa jinsi ya kujikinga wakati wa kupata mtoto, baada ya miezi 6 ya ndoa mwanaume naye akawa +ve, alilia sana, lakini wakaendelea. Na sasa wana mtoto mmoja hasiye na maambukizi.
 
Kuhusu kuweza , nahitaji kuwa na Neema ya Kimungu juu ya hili

Kitu nachojifunza hapa ni kwamba kwa kukosa Elimu juu ya virusi vya ukimwi na Ukimwi ni rahisi sana unyanyapaa na ubaguzi kuwepo,

Huyu Bwana alipata elimu ya kutosha na ndio maana imekuwa Rahisi kwake kufikia hapo

Ukiwa na vitendea kazi sahihi na imara Kazi yoyote itakuwa rahisi kufanyika.

Langu la Tahadhari kwetu wote ni tufahamu kwamba Unyanyapaa una madhara Pande zote, kutokana na maamuzi atakayoyafikia anayenyanyapaliwa
 
Kuweza au kutokuweza kuna mambo yanayoweza kusababisha.

Kwa mtu mwenye elimu ya kutosha juu ya jambo hili atakua na uwezo mzuri wa kuamua na kutenda jambo

Huyu Bwana alipata elimu ya kutosha ndio maana ameweza kufanya hivy

Tukipata elimu ya kutosha tunaweza kufanya

Na ili kuondoa unyanyapaa Elimu ya kutosha inahitajika
 
Nimeshawahi kutibu couple ya aina hii (discordant couple), kwa kweli zipo nyingi...na mara nyingi ni mwanamke anakuwa HIV +ve na mwanaume ni -ve. Na mara nyingi pia wanaume huwa wanabaki na wanawake zao japo wengine huwa hawataki kushiriki nao tendo la ndoa.

Kuna couple moja niliwahi kuitibu nao walikuwa wachumba mwanamke akawa +ve na mwanaume -ve, wakaoana, lakini yule mwanaume hakuwa anasikiliza ushauri wetu wa jinsi ya kujikinga wakati wa kupata mtoto, baada ya miezi 6 ya ndoa mwanaume naye akawa +ve, alilia sana, lakini wakaendelea. Na sasa wana mtoto mmoja hasiye na maambukizi.

Hapo penye red pameniumiza sana roho, nasikitika kwa ajili ya huyo kaka, loh!
 
Kwa kuwa nilikuwa sijaapa kuishi naye kwa taabu na raha, mambo yetu yangeishia hapo.
 
Kwa kuwa nilikuwa sijaapa kuishi naye kwa taabu na raha, mambo yetu yangeishia hapo.

Fikiria kuwa hata wewe ingeweza kukutokea the same same situation, utajisikiaje kama yeye atachukua maamuzi sawa na fikra zako za leo?
 
Life is all about decisions, sometimes very tough decisions this is one of my favaurite quotes,

There is nothing beutifull in this world that true love feelings, hasa zikiingia kwa pande zote mbili, mnaweza kufanya kitu cha ajabu sana, kuna watu wanaoa hadi abnormal in the sake of love, kuna jamaa nilionaga dstv ni mtu mkubwa sana sony corpolation simkumbuki jina, alifosi kuoa mwanamke aliyepata matatizo ya ubongo kwenye ajali na akawa unsound mind, but jamaa aligoma kumuacha akampandisha church na akapata nae watoto wawili wazima japokuwa mke wake ni unsound mind... Dunian kuna watu wana feelings za ajabu
 
Hio si true love ni ukosefu wa akili.

Si hivyo! kama lingekutokea ww..? ungesema unanyanyapaliwa...?
Huo ndio upendo wa kiukweli, la muhimu wafuate ushauri wa madaktari tu.
Nawatakia maisha mema na baraka bw Hassan na mkewe.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom